msaada dr kuku wangu hawatagi kabisa kwa mwaka sasa
Mkuu vitu vifuatavyo vinaweza pelekea kuku wako kutokuta;
kwa kawaida kuku huanza kutaga afikishishapo umri wa miezi mitano ambazo ni sawa na week 18-22 na mara nyingi hutaga mayai kwa peak ya 90% kwa week nane za kwanza na baada ya hapo trend ya utagaji huanza kupungua na wakifikisha umri wa mwaka mmoja uzalishaji wao hupungua na kufikia 65%
kwa kawaida kuku hutakiwa kupewa balance diet, hasahasa huwa tunaangalia ingrideints kama vile carbohydrate (wanga), protein na madini kama vile calcium na phosphorus huwa na msaada mkubwa sana kwa kuku ambao hutaga mayai
kwa mfano kuku huitaji kiwango cha 16% tu ili kumwezesha yeye kutaga na pia huitaji madini kama vile sodium ambazo hutumika sana katika suala zima la uzazi, calcium hutumika kutengeneza egg shells baada ya mayai kutengenezwa na pia hutumika katika suala zima la ukuaji wa mifupa, vitamin D hutumika sana sana katika reabsorption of calcium ili isipotee na hivyo hutumika sana katika uzalishaji wa mayai.
Na pia kwa kuku wanaotaga huitaji maji mengi safi na salama nadhani kila mmoja hujua umuhimu wa maji.
Mwanga ni muhimu sana katika suala zima la utagaji wa mayai katika kuku.... the more you expose them to light the more they laying egg and vice versa is true....
so kwa hali ya kawaida kuku wanaotaga inashaulika ya kwamba wapewe mwanga atleast kwa masaa 16 kwa siku ili kuweza kutaga mayai mengi.
Magonjwa ni tatizo sugu sio kwa kuku wanaotaga tu bali hata kwa jamii ya ndege nyingine na hivyo hupelekea hasara katika suala zima la ufugaji wa kuku, magonjwa kama ndui huathiiri ukuaji na hivyo hupekekea uzalishaji wa mayai kupunga na vile vile magonjwa mengine kama coccidiosis na infectious bronchitis pia yaweza pelekea kuku kutokutaga kabisa
Hivyo kama mkulima unashauriwa kuwakinga kuku wako kwa kuwapa chanjo katika muda muafaka na pia ku maintain Biosecurity measure katika shamba lako.
Hitimisho
kwa maelexo yako hapo juu nahisi tatizo linaweza kuwa suala zima la chakula or tatizo la mwanga katika banda hivyo basi nakushauri jaribu kubadili chakula unachowapa kwa kuwanunulia chakula kingine ambacho kiko well balanced na kama unachanganya chakula chako hapo nyumbani jaribu kubadili formular nzima ya chakula na ujitahidi kuwapa chakula kingi kadli iwezekanvyo kama unavyojua hao kuku wasiposhiba hawawezi kutaga kamwe mkuu.
Na kama tatizo ni mwanga jaribu kuwapa mwanga wa kutosha atleast 16hrs exposure to light per day, ni hayo tu na karibu tena mkuu