Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

VITU VYA KUZINGATIA KATIKA UTEUZI WA ENEO LA KUFUGIA SAMAKI

Leo ningependa kuzungumzia vitu muhimu kabla huja amua ku launch project yako ya samaki katika eneo husika hivyo basi wewe kama mfugaji ambaye una malengo ya kunufaika na ufugaji wa samaki vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia katika uteuzi wa eneo la kujengea bwawa lako la samaki;
  1. Water supply (upatikanaji wa maji)
Maji ni kitu muhimu sana katika uanzishaji wa ufugaji wa samaki kwa sababu maji ndio uti wa mgomgo wa samaki coz bila maji hakuna samaki, hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukachagua eneo ambalo lina upatikanaji wa maji katika misimu yote hapa nazungumzia either kiangazi or masika.

Maji hutumika kwa shughuli mbali mbali kama vile; kujaza mabwawa, kujazilishia mabwawa ka maji yaliyopotea kwa njia ya evaporation or transpiration na mwisho katika suala zima la flushing ( ni njia inayotumika ku restore quality ya maji)

2. Slopping of the area (mwonekano wa ardhi)

Eneo la kujenga bwawa linapaswa kuwa gentle slope in nature (mteremko kiasi) ili kusaidia katika suala zima la flushing (kuondoa maji) katika bwawa na kuwezesha ujazaji wa maji katika bwawa.

3. Nature of the soil (Udongo)

Katika suala zima la ujengaji wa bwawa la samaki udongo ni kitu muhimu sana , na udongo unaoshauriwa ni ule ambao una uwezo wa kushikilia maji kwa muda mrefu hii huwa ni faida coz huepusha usumbufu wa kuzaja bwawa mara kwa mara hivyo basi udongo unaohitajika hapa ni aina ya clay (ufinyanzi) or clay-loam soil udongo wa kichanga haufai,

njia ambazo hutumika ili kuweza kutambua udongo mzuri unashauria kuchimba kishimo cha mita 1 then kijaze maji yaache kwa muda wa saa24 ukirudi ukikuta kiwango cha maji hakijapungua then jua ya kwamba udongo huo ni mzuri na ukikuta kiwango cha maji kimepungua jua udongo huo si mzuri kwa ajili ya bwawa.

4. Uwe na Guarantee ya land ownership

Hili pia lina umuhi u sana katika suala zima la uanziswaji wa ufugaji wa samaki ni vyema uapate eneo ambalo halina mgogoro wa aina yoyote na itapendeza sana iwapo utakuwa na hati miliki ya eneo husika ili kuepuka hasara usiyo itarajia, coz hakuna kitu kinachouma kama kuanzisha mradi wako kwa gharama afu mwisho wa siku kila kitu kinafutika kwa muda mfupi tu hivyo basi suala zima la ardhi lina umuhimu wake katika project nzima ya samaki.

5. Labour availability (upatikanaji wa wafanyakazi)

Katika project yoyote ile ili kuweza kusonga mbele kunahitaji la kuwa na wafanyakazi both skilled and unskilled labour, kwa nchi yetu ya tanzania suala zima la unskilled labour is not a big deal wapo wengi tu kusaidia shughuli fulani za shamba na pia ishu ya kuwa na skilled labour hapa nazungumzia daktari ambaye atakuwa na majukumu ya kuhakikisha hakuna kitu kinaharibika na mradi unaleta faida ya kutosha.

6. No risk of floods

Eneo husika la kuanzisha mradi lisiwe na historia yoyote ya mafuriko pindi mvua zinaponyeesha, hivyo basi unashauriwa kufanya research ya kutosha katika eneo unalotaka kuanzisha mradi wa samaki ili kuweza kuepuka hasara zisizo na ulazima.

7. Potential market area and area free from social taboo restriction

Kuwekeza shamba lako karibu na mjini itakuwa na faida kwako kwani walaji wengi wa samaki ni watu wa mjini coz ndio wenye uwezo wa kumudu gharama za samaki na pia kuepuka different social taboos ambazo mara nyingi huwa zipo sana maeneo ya vijijini ( thou hili liko rarely sana kwa nchi yetu).

8. Natural and alignment of other social activities

Ni vyema eneo unalofugia likawa na mwingiliano na shughuli nyingine za kilino kama vile ufugaji wa kuku ama bata na pia horticulture activities (kilimo cha mbogamboga) huu mfumo kwa kitaalamu inaitwa intergrated farming system.

9. Peace and Order

Eneo husika linapaswa kuwa na amani muda wote, hii ni kuepukana na wizi wa hapa na pale coz unakuta maeneo mengine yamezungukwa na wivu ambavyo hupelekea mfugaji kutokuwa na amani usiku kwa sababu unaeza amka asubuhi ukakuta hakuna kitu katika bwawa la samaki (wezi washafanya yao)

Pia kuwa mtu wa amani sana na kila mtu coz kuna watu wengine huwa na vinyongo wanaweza kukutilia sumu katika bwawa lako ambayo huweza pelekea samaki wote kufa katika bwawa.

Hitimisho
Vijana wenzangu nawahamasisha sana muingie katika ufugaji wa samaki ambao gharama yake huwa ni ya chini mno na hukupa faida ya juu sana.... for more information about fish tuwasiliane kupitia pm
 
Leo naomba tuuangazie ugonjwa wa Newcastle (kideli) na madhara ambayo hutokana na ugonjwa huu hatari kwa jamii ya ndege....

Utangulizi
Ugonjwa huu huenenezwa na kirusi ambaye hujulikana kama Avian paramyxovirus type 1 ambaye hushambulia jamii ya ndege wafugwao na wasiofugwa kama vile kuku wa umri wowote pamoja na bata mzinga na jamii zaidi ya mia mbili ya ndege. Kirusi huyu huwa anakuja na strain 3 kama ifuatavyo;
  • Lentogenic form- Huyu huathiri mfumo wa upumuaji wa kuku but katika kiwango cha kawaida
  • Mesogenic form- Huyu huathiri mfumo wa upumuaji pamoja na mfumo mzima wa ufahamu wa kuku
  • Velogenic- ambaye amegawanyika katika sehemu mbili ya kwanza ni viscerotopic velogenic ambao hushambulia mfumo mzima wa chakula hasahasa utumbo mdogo na sehemu ya pili ni Neurotropic velogenic ambao hushambulia mfumo wa upumuaji na mfumo wa ufahamu.
Njia ya uenezaji wa ugonjwa huu
  • Direct contact baina ya kuku ambao hawana ugonjwa na kuku wenye ugonjwa kupitia matemate na kinyesi cha kuku alieathirika na ugonjwa huu. Pia kuku kugusa vyombo ambavyo vimetumiwa na kuku ambae ameathirika na ugonjwa huo.
  • Pia mayai yaliyotagwa na kuku ambaye ameathirika na ugonjwa huo pia yanaweza kueneza ugonjwa huo pindi vifaranga wanapoangulia na hivyo kupelekea vifaranga kuwa na ugonjwa huo.
  • Pia kwa njia ya hewa au kula chakula kilichokuwa na virusi hao.
Dalili za ugonjwa ni kama ifuatavyo
  • Matatizo katika upumuaji kuku kukohoa,kutoa sauti ya kukoroma anapokuwa anavuta hewa.
  • kuku kuharisha
  • sehemu za macho kuvimba na kuwa nyeusi
  • kutoa ute unaonata nata katika macho na sehemu za upumuaji kama pua na mdomo
  • kifo hutokea siku mbili hadi tatu
  • Iwapo kuku wakipona huonesha dalili zifutazo; kukamaa, kukunja shingo na kichwa na pia atakuwa na dalili za ku paralysis
Jinsi ya kuzuia ugonjwa huo;
  • Njia ya kwanza ni kwa kutumia chanjo nadhani nishaelezea jinsi ya kuchanja ugonjwa huu kwenu nyuzi hapo nyuma
  • Pili zingatia usafi na kuwatenga kuku wote wanaoonesha dalili za ugonjwa ili wasiendelee kueneza ugonjwa huu na pia waweza kutumia antibiotic changanya tylosin na sulphonamide kuzuia secondary bacteria infection kumbuka hii sio tiba bali ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi zaidi.
Hitimisho

Epuka kuwapa kuku chanjo wakiwa wagonjwa kwa sababu utaendelea kuwapa stress na hivyo kupelekea kuongezeka kwa vifo katika shamba lako... hivyo bhasi jaribu kuwapa chanjo katika muda muafaka ili kuepeuka hasara zisizo na msingi ..

Siku zote kumbuka ya kuwa kinga ni bora kuliko tiba.....
 
Dr NGURUWE wangu wanajikuna sana kuna dawa ya kuwaogesha
Mkuu unaweza waogesha kwa kutumia Amitraz 0.1% waogeshe mara 3 kila baada ya siku 10 pia waweza tumia Lindane 0.06% rudia kila baada ya siku 10-14 au waweza tumia Phosmet 25% rudia kila baada ya siku 14.

Pia waweza kuwachoma Ivermectin subcutaneously rudia baada ya siku 14 na pia kumbuka unaposafisha banda lako la nguruwe tumia maji ya moto ili kuweza kuua hao bacteria wanaosababisha sarcoptic mange mkuu

Hope umenielewa na karibu tena.....
 
Mkuu unaweza waogesha kwa kutumia Amitraz 0.1% waogeshe mara 3 kila baada ya siku 10 pia waweza tumia Lindane 0.06% rudia kila baada ya siku 10-14 au waweza tumia Phosmet 25% rudia kila baada ya siku 14.

Pia waweza kuwachoma Ivermectin subcutaneously rudia baada ya siku 14 na pia kumbuka unaposafisha banda lako la nguruwe tumia maji ya moto ili kuweza kuua hao bacteria wanaosababisha sarcoptic mange mkuu

Hope umenielewa na karibu tena.....
Asante mimeelewa Mkuu asante ntafanya hivyo pia vipi hizi dawa upatikanaji wake na bei zake ni sh ngapi?
 
Asante mimeelewa Mkuu asante ntafanya hivyo pia vipi hizi dawa upatikanaji wake na bei zake ni sh ngapi?
bei ni za kawaida sana jaribu kutembelea katika maduka ya pembejeo na kilimo kuulizia na kununua mkuu
 
Vipi kuhusu dawa ya kuwaogeshea hawa watoto na mama pia ili kukomesha viroboto na kuhusu chanjo pia ni lazima aje doctor au hata mwenyewe naweza kuchoma
Mkuu waweza tumia Amitraz ambayo inafahamika kama Taktic .. Kuhusu Chanjo Daktari ni muhimu kuhusika mkuu kuna suala zima la vaccine chain ni muhimu kuzingatiwa

And kwa watoto usiwaoshe kwanza mpaka atleast wafikishe 3-4 weeks of age mkuu.....
 
Doctor habari yako nimeenda duka moja la pembejeo nimeambiwa wanadawa ya kuogesha inaitwa paramex hizo zingine ulizoniambia wamesema hawana.je hi itanifaa?
Ungejaribu kuitafuta kwa maduka mengine pia inajulikana kama Taktic incase ukiikosa kabisa itakubidi uitumie hiyohiyo na imani itakupata positive results....

Afu ni vyema pia ukawachoma Ivermectin baada ya kuwaosha ili ku control hao external parasite kama nilivyokuelekeza kwa post ya kwanza kule juu.....

Kila la kheri mkuu....
 
Kuku wangu hapa naona macho yao yavimba then wanakuw hawaoni ukipasua unakuta kama uvimbe flan hiv

Je ni ugonjwa upi huu
 
Ndg mganga,kuku wangu chotara ila sehemu zao za siri zimekuwa too wet na wanataga,sijajua sababu,nilimwita mtaalam akachek akasema atatafuta tiba ila ni muda japo alisema haina madhara ila binafsi inanikera kuona nyuma kuna mavi yamewaganda yaani hawako smart
 
Habari Mkuu Theriogenology!....Mkuu nakupongeza kwa hiki unacho kifanya Mungu akuabriki na endelea kutupa elimu na maarifa juu ya ufugaji wenye tija.

Shida yangu kuu nikupenda kujua namna kuku wa mayai na wa nyama wanavyo patikana (wanazalishwa vipi)?...Je kuna mayai ambayo ukinunua unaweza kuzalisha kuku hawa wa mayai na nyama? Kama jibu ndio mayai hayo yanatoka wapi au yanazalishwaje na nani?
 
Habari Mkuu Theriogenology!....Mkuu nakupongeza kwa hiki unacho kifanya Mungu akuabriki na endelea kutupa elimu na maarifa juu ya ufugaji wenye tija.

Shida yangu kuu nikupenda kujua namna kuku wa mayai na wa nyama wanavyo patikana (wanazalishwa vipi)?...Je kuna mayai ambayo ukinunua unaweza kuzalisha kuku hawa wa mayai na nyama? Kama jibu ndio mayai hayo yanatoka wapi au yanazalishwaje na nani?
Nimelipenda swali lako
 
Mkuu mimi niko Dar, ninampango wa kuanzisha mradi wa kati wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. naweza kupata mawasiliano yako tafadhari.
 
Habari Mkuu Theriogenology!....Mkuu nakupongeza kwa hiki unacho kifanya Mungu akuabriki na endelea kutupa elimu na maarifa juu ya ufugaji wenye tija.

Shida yangu kuu nikupenda kujua namna kuku wa mayai na wa nyama wanavyo patikana (wanazalishwa vipi)?...Je kuna mayai ambayo ukinunua unaweza kuzalisha kuku hawa wa mayai na nyama? Kama jibu ndio mayai hayo yanatoka wapi au yanazalishwaje na nani?
nitakujibu baadae swali lako mkuu kwa undani zaidi.... but kwa ninavyojua kupata mayai ya parent stock ni issue ingine mkuu na inasemekana ni nchi 4 tu duniani zenye uwezo wa kuzalisha hao pure stock breed ya broiler/layers na wanafanya siri sana mtu kugundua technology yao...ndio maana umeona ni nchi chache zenye kuweza kuzalisha hao parent stock...

Ila ukihitaji vifaranga unapata bila shida mkuu but not mayai yao....
 
Back
Top Bottom