Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Za asubuh mkuu.... nina mpango wa kufuga kuku elfu 1 kwenye eneo moja.... wa kienyeji.

Naomba ushauri mkuu wa kitaalamu... vitu gani vya kuzingatia katika ukuaji na utagaji wao....

Na eneo ukubwa gani kitaalamu wanatosha.
Na chanzo gani muhimu na rahisi kwa woote kujikinga na magonjwa....?

Sent from "La -Vista"
 
Kuna ugonjwa wa kuku unafahamuka kama coryoza na pia huu mwingine unajulikana kama Chronic Respiratory Disease (CRD) ... ni nini kinga pamoja na chanjo na tiba ya magonjwa haya?
 
Mkuu Dr. tunashukuru kwa utayari wako wa kutaka kutusaidia. Sorry, nina ng'ombe dume mzuri chotara ambaye nia yangu ilikuwa kumtumia kwa mbegu ili kuendeleza mbegu lakini cha ajabu dume huyu mzuri hataki kuwapanda majike kutwa kucha ana attempt kuwapanda madume wenzie. Hii hali kitaalamu huwa inatokea? Sababu yake ni nini? Na dawa yake ni nini?
Ng"ombe basha huyoo
 
mkuu kwa maelezo yako hapo juu.... ng'ombe wako ana ugonjwa unaoitwa downer's syndrome ambao ni ugonjwa pacha wa milk fever ambao husababishwa na upungufu wa madini ya calcium katika damu hivyo kupelekea ulegevu wa misuli na hivyo kupelekea ng'ombe kukaa chini kwa muda mrefu bila kunyanyuka

treatment yake inakuwa inasumbua tofouti na milk fever ambayo hutibika kirahisi embu fanya yafuatayo;
  • Mchome Calicium borogluconate kwa kiasi cha 800-1000ml nusu mwekee IV (mshipa wa damu jugular vein) na nusu nyingine mweke subcutaneous (chini ya ngozi)
  • Jaribu kumpa maji yaliyochanganywa na glucose
  • afu jitahidi sana kumnyanyua kama sehemu ya mazoezi ili aanze kuzoea kusimama tena
Nshukuru ngombe ameamka baada ya siku 14! It was hard work and despair! Kazi kubwa niliyonayo ni kurudisha afya yake. Doctor, nimlishe vipi aweze ku gain weight haraka. asante sana kwa ushauri wako. santetena.
 
Wote wana umri mmoja miaka mitatu mkuu!
Mkuu samahani kuingilia. Lakini nina swali/maoni kwanini usifanye uhamilishaji kwa chupa (Artificial Insermination) tu kuliko kufuga dume kwa gharama na bado hafanyi kazi.

Mbegu bora ni cheap na process nzima itakayo guarantee offspring uitakayo ni rahisi tu.

Daktari atanisaidia kama nimekosea mahali
 
Ni wapi kati ya mikoa ya kanda ya Kati na Pengine na ziwa naweza pata ng'ombe wa kisasa wenye uwezo wa kutoa Lita kati ya 10 na 20 kwa siku? Nasisitiza hapo Daktari Lita 10 au 20! Unajua kuna kuwa na maneno mengi ya hamasa nane nane na kwenye baadhi ya mashamba .Kuna jamaa yangu ana ng'ombe hao , hawatoi maziwa kama alivyoambiwa wakati akinunua licha ya marisho na care! Anapata 4 na iwe mapema baada ya kujifungua zinapungua kadri muda unakwenda! Ufugaji wa kibiashara nautamani, mfano unajikunja unapata ng'ombe say 4 ,Lita 10@ sawa 40 ltrs @ 1000= 40,000/ perday x 30 per month= 1,200,000/.Huku mikoani kwa DSM ni twice. Ushauri wako tafadhali, aina gani ya ng'ombe haswa! Mpwapwa hybrid kuna jamaa yangu kachukua,aliambiwa 8ltrs perday, anapata 4 ,
Ndugu nina swali nisaidie kumuuliza huyu rafiki yako mfugaji.

Je
1. Anazingatia malisho kwa kilograms? Au anawajaza tu kila waliapo?
2. anawapa concetrates?
3. Anawapa japo nafasi ya kufanya mazoezi au ni 100% zero grazing?
4. Amewawekea lile jiwe la chumvi?
5. Vitu kama makiliki(sifahamu spellings zake) anawapa kuongeza joto?
6. Ratiba ya muda wa ukamuaji inazingatiwa?
7. Mlishi na mkamuaji wana uniforms? Hapa utajiuliza kwanini lakini naamini Dokta atakuelewesha zaidi ni kwanini, na wafugaji wengi wanafeli hapa ng'ombe anakata maziwa na wengine kuugua mastitis
8. Usafi wa mwili na malazi ya mifugo hayo yako?

Mkuu hayo yanachangia sana kwa mfugo huyo kutoku perform anavyotakiwa kuperform

Daktari nisaidie nilichosahau au nilichotia chumvi
 
Shukran kwa wazo zuri mkuu. Mm nafuga kuku wa kienyeji, ila kuna ugonjwa wa vifaranga kutokwa na vidonda mdomoni unanimalizia sana vifaranga wangu sana.

Kuna batch fulani waliugua huo ugonjwa nikamuona dr akaniambia unasababishwa na virus na hakuna tiba zaidi ya chanjo, ikanibidi batch iliyofuata nikapiga chanjo lakini vifaranga vyote vilikufa. Sasa sielewi nifanye nini na hivi karibuni kuku atatotoa vifaranga wengine. Je nini ushauri wako na tiba kabla ya hao wengine nnaotarajia kuwapata.
 
Ahsante Dokta kwa utayari wako kutuelimisha. Naomba kuuliza: Je, vifaranga wanatakiwa wakae siku ngapi ili wapate chanjo baada ya kutotolewa?, Je ni aina gani ya chanjo inafaa? (kuku wa kienyeji).
 
Kuna ugonjwa wa kuku unafahamuka kama coryoza na pia huu mwingine unajulikana kama Chronic Respiratory Disease (CRD) ... ni nini kinga pamoja na chanjo na tiba ya magonjwa haya?
Magonjwa hayo yote husababishwa na bacteria na yote husambulia mfumo mzima wa upuaji yaani respiratory system..

Coryza husababishwa na Haemophilus paragallinarum na bacteria huyu huenezwa kwa njia ya direct contact kupitia kuku anaeumwa ugonjwa huu na kuku ambao hawana ugonjwa huu or Indirect kupitia vyombo vya usafi vyenye bakteria hao...

Chronic respiratory disease ugonjwa huu Husababishwa na Mycoplasma gallisepticum huenezwa kwa njia ya transiovarian route kutoka kwa mama kwenda kwa vifaranga kupitia mayai na hii yaweza kupelekea wewe kununua vifaranga wenye huo ugonjwa na pia kwa wakubwa ni kupitia njia ya direct contact kama nilivyokwisha elezea hapo mwanzo....

Tiba yake ni kwa kutumia Antibiotic na pia kwa CRD yakupasa kununua vifaranga vilivyopewa chanjo ya kuzuia ugonjwa huo na vilevile hakikisha suala zima la management linazingatiwa vilivyo katika banda lako mkuu
 
Ahsante Dokta kwa utayari wako kutuelimisha. Naomba kuuliza: Je, vifaranga wanatakiwa wakae siku ngapi ili wapate chanjo baada ya kutotolewa?, Je ni aina gani ya chanjo inafaa? (kuku wa kienyeji).
Mkuu kwa day 1 old chick chanjo zinazotakiwa kuwakinga vifaranga wako dhidi ya magonjwa hatari ya bacteria na virus ni kama ifuatavyo ; Chanjo dhidi ya Chronic respiratory disease, salmonellosis, avian leukosis, avian encephalomyelitis na avian influenza thou kwa local breed wetu ni nadra sana kupata magonjwa hayo but kama uko ki commercial zaidi ni vyema ukawakinga mkuu coz siku zote wanakuambia Kinga ni nzuri zaidi kuliko tiba.... kila la kheri mkuu
 
Shukran kwa wazo zuri mkuu. Mm nafuga kuku wa kienyeji, ila kuna ugonjwa wa vifaranga kutokwa na vidonda mdomoni unanimalizia sana vifaranga wangu sana. Kuna batch fulani waliugua huo ugonjwa nikamuona dr akaniambia unasababishwa na virus na hakuna tiba zaidi ya chanjo, ikanibidi batch iliyofuata nikapiga chanjo lakini vifaranga vyote vilikufa. Sasa sielewi nifanye nini na hivi karibuni kuku atatotoa vifaranga wengine. Je nini ushauri wako na tiba kabla ya hao wengine nnaotarajia kuwapata.
labda ungeniambia unatumia system gani ya ufugaji mkuu.... either free range system or intensive system na ukiacha hiyo dalili ya vifaranga kutoka vidonda mdomoni ni dalili nyingine ipi wanaonesha tena mkuu? tuanzie kwanza hapo
 
Vipi magonjw ya bata mzinga ni yapi
Mkuu yapo magonjwa mengi tu kama vile Newcastle, typhoid, coryza, hemorrhagic enteritis, avian encephalomyelitis na infectious bursa disease....

sasa sijajua ulikuwa unataka maelezo ya ugonjwa gani hapo juu mkuu....
 
Za asubuh mkuu.... nina mpango wa kufuga kuku elfu 1 kwenye eneo moja.... wa kienyeji.

Naomba ushauri mkuu wa kitaalamu... vitu gani vya kuzingatia katika ukuaji na utagaji wao....

Na eneo ukubwa gani kitaalamu wanatosha.
Na chanzo gani muhimu na rahisi kwa woote kujikinga na magonjwa....?

Sent from "La -Vista"
mkuu swali lako liko ki upana zaidi waweza nicheki pm for more detail
 
Mkuu kwa day 1 old chick chanjo zinazotakiwa kuwakinga vifaranga wako dhidi ya magonjwa hatari ya bacteria na virus ni kama ifuatavyo ; Chanjo dhidi ya Chronic respiratory disease, salmonellosis, avian leukosis, avian encephalomyelitis na avian influenza thou kwa local breed wetu ni nadra sana kupata magonjwa hayo but kama uko ki commercial zaidi ni vyema ukawakinga mkuu coz siku zote wanakuambia Kinga ni nzuri zaidi kuliko tiba.... kila la kheri mkuu
Mkuu hizi ni chanjo ama dawa ya kuwapa wakiwa na day1. Mimi navyojua chanjo ya Day 1ni Malek, then zingine zinafuata wiki kwa wiki ( Gombolo na Newcastle);

Kama ni chanjo je zinapatikana wapi?
 
Back
Top Bottom