Mtaandika vitabu na vitabu, ila hamtaweza kubadili chochote juu ya Hayati Magufuli

Wanaangaika sana na mradi wa kumchafua muzilankende muyango ila wapi. Izi ela wanazopewa na mafisadi watazikumbuka badae wanavyozichezea. Wenzao kina mbowe washapata mfereji wa asali. Kuna kagenge ka waandishi wanajionaga wao ndio top manyota kumbe usanii na uchumia tumbo. Muda utaongea.
 
Naunga mkono hoja, kwa yote aliyofanya Magufuli ndani ya kipindi kifupi hawezi kuwa disqualified na kijipeperushi kinachoitwa kitabu....
 
Hata kama MAJIZI wataandamana Nchi nzima kwa lengo la kufuta nyayo za JPM, kamwe kamwe kamwe hawataweza.

Kinyume chake, wanapojaribu kufuta nyayo za JPM, ndipo wanapomuimarisha zaidi JPM.
 
Tangu lini mwamba apendwe na mafisadi? Wafoji vyeti? Wezi na wauza dawa? Wazembe! Hii haiwezi kutokea kamwe! Hata wewe utakuwa mpumbavu ukimkubali jambazi wewe
Teh teh teh!
Kiko wapi sasa!
Yaani sisi tumpende Marehemu!!
Ok mfateni aliko kuonyesha mwampenda sana mfu
 
Mbona huyu naye alimnanga Magufuli wenu ila mkajifanya hamkumsoma

 
Ata= hata
Awawezi= hawawezi
Anaitajika= anahitajika
Jiifunze kwanza lugha adhimu ya kiswahili
 
I quote,"kuna wajinga wachache wanadhani eti ni rahisi kusahau mema uliyotuachia Magufuli," unquote.Sio rahisi,they better know.Wataandika vitabu na kuandika,lakini haitasaidia.
 
"Kuna wajinga wachache wanadhani eti ni rahisi tusahau mema uliyotuachia Magufuli,"sio rahisi,they better know.Wataandika vitabu na kuandika,lakini haitasaidia.
Mungu Ibariki na Tanzania na watu wema wa nchi hii
 
Taifa la Tanzania lilimpoteza Rais bora sana kuwahi kutokea tarehe 14.03.2021 😢
 
Kikubwa ulichoachiwa ni Chato International Airport. Tangu huyo kipenzi chako aondoke ndege ngapi za kimataifa zimetua?
Tangu mwendazake alipochukua Biliocana na mashamba ya Mbowe ni muendelezo upi umeuona?
Tangu mwandazake awaweke akina Ruge na Seth ni maendeneo gani yalipatikana mapaka akakitoa?
Tangu Azole apotee ni taarifa gani zilitumwa kwenye jeshi la polisi kuhusu huyo mtuhumiwa?
Tangau Ben Saa Nane amtuhumu kuwa na vyeti feki na akapotea, ni wapi kwenye magereza ya nchi hii amepatikana akiropoka?
Tangu mashamba ya Mbowe ambaye ni kiongozi mkuu wa upinzani anyang'anywe mashamba yake ni lini tulisikia kesi zinanguruma?
Tangu biashara ya fedha ilipositishwa, ni lini serikali litutangazia pasa zilizookolewa.
Tumesikia akina MO wanapotea tena wanapatikana, je walikubaliana kikombozi kiasi gani na watekaji? je na watekaji hao walikuwa nani?
Alipotea Mkatoliki hapa baada ya kuteswa kule shimo jipya la ununio, aliokotwa na hali mbaya na akaamua kusepa lakini Roma Mkatoliki ni wale vijana wa kizazi kipya wenye uelewa na ambao wapo tayari kufa kuliko kukaa kimya na vijisenti vilivyopelekwa kwenye of shore bank account. Tunaomba tujulishwe ni vijisenti kiasi gani wakati wa mzee wa bagamoyo?
Nashukuru kwa majibu hayo from the direct person siyo hawa malimpyoto.
 
Kabla ya kila kitu kufanyika, kinachotangulia ni maono, ukiwa mtu wa maono, unauwezo wa kuyaona mambo yako mbele mita nyingi zisizohesabika! Hii inawahusu werevu peke yake, kama na wewe ni miongoni mwao utaelewa

Mbuga ya wanyama Burigi, Hospital ya kikanda na ya kimataifa Chato' vitu hivi viwili, vinatosha kabisa kumlazimisha mtu yeyote mwenye afya ya akili kumwambia kwahitajika uwanja wa ndege

Ni wapumbavu na watu wasiokuwa na maono ambao watapingana na hilo

Na Magufuli hakuwahi kujitengenezea kitu Chake mwenyewe, alivyokuwa ukilenga, ni Tanzania mpya ya miaka 100 ijayo

Unapoanzisha miradi mingi ya kimkakati, haiwezi kukupa matokeo ya miaka miwili" SGR, JKNHP, na shirika la ndege, mambo haya hayawezi kutoa matokeo ya muda mfupi!

Narudia tena hapa, licha kwamba Karibu asilimia kubwa ya watanzania ni watu wanaopenda vitu walivyowekeza kwa gharama kubwa vitoe matokeo leoleo, huu ujinga ndio unaolila Taifa letu

Huwezi kuanzisha biashara leo halafu kesho tu unataka likuzalishie maduka matano mengine!

Ni upumbavu,
 
Unataka kusema Nyrerer alikuwa mchafu ndiyo maana hademwi?
 
Unataka kusema Nyrerer alikuwa mchafu ndiyo maana hademwi?
Utamsema Nyerere ulikuwepo?

Kipindi Chake kulikuwepo upinzani?

Yatambue majira ndugu hutapata tabu mkuu
 
Wizara ya habari imeishiwa Sera Sasa hivi Bali imegeukia maneno ya kwenye kanga na vijembe vinavyoshadadia kumchafua magufuli,wakisimamiwa na mnyapara wao mzee lomo lomo,vijembe hivyo havimsaidii mtanzania wa lyambamigongo kupata mlo wake wa siku
 
Wanapambana na marehemu

Magufuli alitusaidia sana kujua taaisisi na wanasiasa wa nchi hii

Kiufupi wengi ni matapeli mno , kuanzia waandishi wa habari Hadi wanasiasa

Sent from my CPH2217 using JamiiForums mobile app
 
Wanapambana na marehemu

Magufuli alitusaidia sana kujua taaisisi na wanasiasa wa nchi hii

Kiufupi wengi ni matapeli mno , kuanzia waandishi wa habari Hadi wanasiasa

Sent from my CPH2217 using JamiiForums mobile app
Pesa za wanasiasa mafisadi huwa hazina mahali pa kwenda na kwa kuwa huwa hawazitolei jasho, basi tuwaache zitumike kijinga kama walivyo wao!

Hata iweje, mwenye haki hawezi kupotezwa na waovu!

Ni suala la muda tu, kuna kina Magufuli wengi Mungu atawatokeza muda wake ukifika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…