Mtambo wa pili bwawa la Nyerere kuwashwa, kumaliza kabisa mgao wa umeme nchini

Mtambo wa pili bwawa la Nyerere kuwashwa, kumaliza kabisa mgao wa umeme nchini

Serikali inatarajia kuwasha mtambo wa pili wa kufua umeme kwenye bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere pamoja na changamoto ya kuzidi maji katika bwawa hilo. Mkurugenzi wa Tanesco kanda ya mashariki, Kenneth Boymanda amesema majaribio yanaendelea ambapo mtambo huo unaojulikana kama mtambo namba nane majaribio yamefanyika kuupa njia ya kuwashwa.

Mwezi uliopita uliwashwa mtambo wa kwanza wa megawati 235 na kupunguza kwa kiwango kikubwa mgao wa umeme, inatarajiwa kuwashwa kwa mtambo huu wa pili kutamaliza kabisa mgao wa umeme.
Umeme unakatika kila siku tunaambiwa mitambo mitambo kuweni wakweli nani anahujumu umeme nchini na kwanini anaogopwa na serikali?
 
Hivi objectives ilikuwa ni KUMALIZA MGAO au Kuhakikisha UMEME unakuwa Affordable yaani hili la Mgao ni tatizo walilolileta hapa Katikati...

Issue ya Sisi wananchi kuingia kwenye Madeni ilikuwa ni Bwawa likiisha Umeme ushuke Bei...., Waache Kuhamisha Magoli....
 
Siwavunji moyo, tatizo lililopo sasa hivi siyo kuwa hatuna umeme wa kutosha.

Tatizo hatuna ukanja wa kuendesha shirika kubwa namna hilo kiufanisi.

Kinyerezi I, II, III, IV na vyanzo vingine vya umeme vya zamani vinatutosha kabisa kutokuwa na tatizo la umeme tulilonalo.

hivi kwa nini waislamu siyo partriotic? Je, kwenye uislamu kuna sehemu yoyote nation au taifa imetajwa? uislamu unafundisha nini kuhusu nation? kwa sababu waislamu hawaamini kabisa katika kitu kama taifa …
 
Shirika muwape tena wakina ami wa uarabuni kama bandari hao ndo wanaweza
 
Au shirika nalo inabidi tuwape wakina ami wa Oman
Tika tuoate uhuru hatujawahi kuweza kuendesha shirika lolote la Umma kwa ufanisi.

Imetushinda BRT tutaweza shirika kubwa kama TANESCO?

Fikiri.
 
hivi kwa nini waislamu siyo partriotic? Je, kwenye uislamu kuna sehemu yoyote nation au taifa imetajwa? uislamu unafundisha nini kuhusu nation? kwa sababu waislamu hawaamini kabisa katika kitu kama taifa …
Neno "taifa" lenyewe ni la Kiislam.

Uzalendo kwenye uharo?
 
Neno "taifa" lenyewe ni la Kiislam.

Uzalendo kwenye uharo?

la asili ya kiarabu siyo kiislamu haujaijua tofauti mpaka leo hii? Lugha ya kiarabu ilikuwepo kabla ya uislamu isitoshe haujaelezea kama uislamu unafundisha chochote khs taifa na partriotism kwa maana kwenye Biblia Taifa limetajwa na hata partriotism imepewa kipaumbele …
 
Havielewekiii juzi walizima sababu mafuriko vijiji jiraniii
Uwe unasoma na kuelewa. Maji yalizidi kwenye bwawa wakazima mtambo na 9 wakafungulia maji kuyapunguza yakasababisha mafuriko vijiji 23 vya jirani.
 
Hebu acheni nyenyenye! Hatuna umeme huku!! Mtambo mtambo,mtambo wa nyoko?
Tatizo la umeme Tanzania halitaisha.

Tuna matatizo 2 ya msingi.

1. Majizi, wahujumu, majitu majinga yanayosifia kila kitu pasi kushirikisha bongo zao lakini pia wataalamu uchwara wasio na weledi kwahiyo kila kitu kinaenda hovyo hovyo.

Asikudanganye mtu. Tanzania watu wanaopata huduma ya umeme 43% hivi. Hata nusu ya population haifiki.

Kelele zote unazosikia tunapeleka umeme sijui wapi ni vile wanafahamu wanawaambia watanzania wasio fahamu lolote kwahiyo ni ujinga ujinga tu.

Tanzania power cut inatokea muda wowote tena hakuna taarifa wala baba yake taarifa utapata. Achilia mbali umeme wa Tanzania kuunguza kifaa chako cha umeme ni dk 0. Inabidi utumie device yakuregulate umeme.

2. Uzalishaji mdogo sana wa umeme. Sasa hivi installed capacity ni 1700MW na vile idadi ya watu inaongezeka sasa ikifika 2025 pengine tutahitaji 5000MW hivi ili umeme upatikane kweli bila mgao. Julius Nyerere Hydropower plant iko installed capacity ni 2200MW if im not mistaken.

Sasa umeme wa uhakika utapatikana vipi?

Wananchi vilaza wataendelea kupigwa sound hadi akili ikae sawa.

3. Watanzania waendelee kukaa kwa kutulia. Wale konokono gizani. Kwasababu hayo ndiyo maisha halisi ya danganyikans.
 
Serikali inatarajia kuwasha mtambo wa pili wa kufua umeme kwenye bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere pamoja na changamoto ya kuzidi maji katika bwawa hilo. Mkurugenzi wa Tanesco kanda ya mashariki, Kenneth Boymanda amesema majaribio yanaendelea ambapo mtambo huo unaojulikana kama mtambo namba nane majaribio yamefanyika kuupa njia ya kuwashwa.

Mwezi uliopita uliwashwa mtambo wa kwanza wa megawati 235 na kupunguza kwa kiwango kikubwa mgao wa umeme, inatarajiwa kuwashwa kwa mtambo huu wa pili kutamaliza kabisa mgao wa umeme.
Wanatuona manyani😂😂
 
Back
Top Bottom