Mtambo wa pili bwawa la Nyerere kuwashwa, kumaliza kabisa mgao wa umeme nchini

Utawashwa lini mtambo huo? Mlisema ungewashwa mwezi March, leo hi April bado mnasema utawashwa, utawashwa lini?
 
Hili neno "KUMALIZA KABISA MGAO WA UMEME" linatumika vibaya sana aisee.
 
Jamani hawa tanesco sasa wanatuchukuliaje si walisema wamezima mtambo uliowashwa sababu ya maji kuzidi wakaogopa ungeburst sasa huo mwingine wanauwashia wapi mro wami au..??
 
Naibu waziri mkuu mh Dr Biteko amesema Mtambo namba 8 na 7 Bwawa la Umeme la Nyerere itawashwa Hivi Karibuni Baada ya Majaribio kwenda vizuri

Biteko amesema kuwashwa kwa mitambo hiyo kutamaliza kabisa tatizo la Umeme nchini

Tutampata wapi sisi Mtu kama Magufuli ambaye Mungu wa Mbinguni anakaa ndani yake?

Mlale Unono πŸ˜„πŸ˜„πŸ”₯
 
Kwa hili la UMEME naipongeza Serikali,sasa tunaweza jiita Serikali ya ViWANDA,KUDOS!...twende na mengine hasa Usafiri wa Umma Dar Es Salaam + Miundombinu ya barabara
 
Mkuu unapohusudu ya mwendazake kumbuka na madhila wanayopitia wakaazi wa Rufiji. Tusifurahie tu, tuwatetee na wenyeji wa Rufiji in equal measures.
 
Makamba angebaki wizarani mpaka Leo angekuwa anapiga danadana
 
Kwaiyo miaka ya nyuma mafariko yalikuwa yanasababishwa na bwawa?
Mkuu ya sasa chanzo chake ni bwawa ili kulinusuru lisibomoke. EIA - (Environment Impact Assessment) Ilitakiwa ioneshe namna ya kushughulikia athari hiyo.

Mkuu mafuriko ya asili na maafa mbali mbali ya ya asili yanatokea sehemu nyingi tu nchi na watu wanaathirika.
 
Mkuu unapohusudu ya mwendazake kumbuka na madhila wanayopitia wakaazi wa Rufiji. Tusifurahie tu, tuwatetee na wenyeji wa Rufiji in equal measures.
Kwamba tukuamin wewe mpiga kelele wa mitandaoni na sio serikali kuwa ? Serikali imekanusha zaudi ya mara 10 kuwa bwawa limesaidia kidogo kupunguza madhira ya mafuriko wewe unasema bwawa ni chanzo cha mauriko
 

Attachments

  • 434475529_846896627480901_3139416211912675353_n.jpg
    88.4 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…