Mtandao wa Jumia wafunga biashara yake nchini Tanzania

Mtandao wa Jumia wafunga biashara yake nchini Tanzania

Bidhaa zao mbovu wapuuzi hawa na customer care yao ni ya kikuda..kikuu na Aliexpress hawajawai kuniangusha..
Mkuu naitaji nami maelekezo vizuri ili nitumie hii mtandao nachoitaji kuwa nacho na ujazajiwake wa form mpaka nipokee mzigo wangu na vipi kuhusu utapeli?
 
Dah, hawa jamaa nilikuwa nataka nianze kutumia huduma zao lakini kuna kitu kilinistua nikasita,nikawa tu mtazamaji wa ofa zao tu
Nilipata ofa yao ya subwoofer. Ikiwa na sifa kede kede sijui wireless speakers, bluetooth n.k.

Nikanunua . Sasa nilimtuma mtu kuichukua kwenye pickup station. Aisee alivyofikisha nyumbani niliona kama kachozi kananidondoka.
 
Bithaa ndiyo vitu
Besta Mlagila,

Hili nilijua.. Kwanza kabisa wana huduma mbovu sana

Naweza kutolea mfano kuna bithaa nilihitaji nyingi sana ambazo nilizikuta kwenye web yao Ila kutokana kua ni mgeni wa huduma zao nikaona niagize vichache kama sampo.. Niliagiza vichache ila nilivyo agiza na nilivyo letewa ni tofauti kabisa na vikiwa havina ubora kabisa. Nikatoa taarifa kua nimepokea bithaa tofauti siku iyo iyo nilipo vipokea wakasema watavifata.

Nizilipo pita siku mbili nikauliza vip maana nna siku saba za return wakasema kwa sababu umesha toa taarifa hilo lisikupe shaka.. Baada ya siku 7 kupita bila msaada nikawafata nikaambiwa return inafanyika ndani ya siku 7 hivyo hawana la kunisaidia. Nisema so militia taaria siku ile ile nilipopokea mzigo? Jibu lao ni kua kama nilitoa taarifa basi hazikuingizwa kwenye taarifa zao hivyo hawana la kunisaidia.

So sad
Kwa mtu mwenye akili sidhani kama atarudia tena kutumia huduma zao
Bithaa ndiyo vitu gani mkuu????? Bila shaka utakuwa maana ccm tu.
 
Dah!! Kwahiyo walioagiza bidhaa zao pesa yao imeliwa🤨
 
Kila nikifungua site yao tokea jana sipati kitu, nilkuwa nataka nitelemke hii friday na black friday yao lakini mambo si mazuri. Nini kinaendelea? Mwenye taarifa atujuze.
 
Kwa hapa Tanzania watafeli tu.Maana watalazimika kuajiri watu kutoka hapa hapa.Sasa kwa akili za watanzania wengi,huwa za kipuuzi puuzi tu.
Wengi suala la kutojitambua linasumbua.Kazi ni ujuaji mwiingi,uaminifu kidogo,na akili za wizi wizi tu na kuwaona watu wengine wajinga.
Utakutana na mtu graduate wa Chuo kikuu,ila anawaza kutumia ukondoo wa watanzania kama fursa ya kuwaumiza.Hawazi namna ya kuleta suluhu.
Naamini wangeajiri watu wa nchi nyingine wangefanikiwa sana.Sijui watanzania tutabadilika nini tuanze kuona uaminifu kama kitu cha thamani na uhuni unaoitwa "dili" kuonekana wizi na utapeli.
 
Hawa wafunge tu, nimewahi agiza simu kwao mara mbili nikaambulia patupu
 
Niliacha kuitumia baada ya nilichoagiza kuletwa kingine nikakikataa, halafu walivyokuwa wapumbavu, picha ya nilichokiwa nimeagiza ikabadilishwa, ila ile ya kwanza kabisa ikawa kwenye order nloifanya, sasa mleta bidhaa nikamuonesha nilichokiagiza akaangalia alichokileta akatikisa kichwa ila alikuwa mstaarabu, akavirudisha ile order akaikanseli
Kama Watumishi ni Wabongo wala sitoshangaa kampuni kukwama.

Mimi huwa napenda sana kufuatilia huduma kila niingiapo Ofisi, Mgahawani, Duka au Usafiri...ninachogundua mara nyingi ukiona huduma ni nzuri na ya kujali Mteja basi anayekuhudumia mara nyingi ndiye mmiliki wa hiyo Ofisi/Duka/Mgahawa n.k.

Ni juzi tu nimeingia Bar moja kubwa tu A town, nikaagiza vinywaji Muhudumu akaleta kisha akakimbilia kuketi meza ya pembeni na kuanza kuchezea simu yake ili hali ile meza ilikuwa chafu..nikamuangalia kwa muda nikiwa nimekasirika sana kisha nikamuita, nikagomba kwamba "hivi huna uwezo wa kuona hii meza ni chafu?" basi akaenda kuchukua kitambaa huku amevuta mdomo utasema nimemtukana tusi la nguoni.

Inashangaza sana Mtu hajui hata kama mimi kuja pale ndio kampuni yake wanapata pesa ya kumlipa mshahara wake.

Ndio ile unakuta Mtu anawekeza kwenye usafirishaji, ananunua Mabasi ya gharama kubwa lakini anaishia kuajiri Wapuuzi watupu kutoa huduma...Wabongo tuwajinga sana.
 
Hawana uhusiano na mabeberu?
JUMIA imeanzishwa na jamaa ninayemfahamu, alikuja kwenye ofisi za IBM Nairobi kwenye chuo cha kikatoliki cha CUEA na kutoka semina kwa wanafunzi kuitangaza JUMIA

Ni Mkenya kabisa ila aliyekulia USA tangu akiwa na umri wa miaka 17, amemuoa mdada wa kihindi...mzuri sana na figured.

Ni Mshikaji wa kama late 30's au early 40's sio mkubwa sana.

Ndio Mwanzilishi wa JUMIA nahisi alipata support kutoka kwa marafiki wa marekani pia.
 
Kama Watumishi ni Wabongo wala sitoshangaa.

Mimi huwa napenda sana kufuatilia huduma kila niingiapo Ofisi, Mgahawani, Duka au Usafiri...ninachogundua mara nyingi ukiona huduma ni nzuri na ya kujali Mteja basi anayekuhudumia ndiye mmiliki wa hiyo Ofisi/Duka/Mgahawa n.k.

Ni juzi tu nimeingia Bar moja kubwa tu A town, nikaagiza vinywaji Muhudumu akaleta kisha akakimbilia kuketi meza ya pembeni na kuanza kuchezea simu yake ili hali ile meza ilikuwa chafu..nikamuangalia kwa muda nikiwa nimekasirika sana kisha nikamuita, nikagomba kwamba "hivi huna uwezo wa kuona hii meza ni chafu?" basi akaenda kuchukua kitambaa huku amevuta mdomo utasema nimemtukana tusi la nguoni.

Inashangaza sana Mtu hajui hata kama mimi kuja pale ndio kampuni yake wanapata pesa ya kumlipa mshahara wake.

Ndio ile unakuta Mtu anawekeza kwenye usafirishaji, ananunua Mabasi ya gharama kubwa lakini anaishia kuajiri Wapuuzi watupu kutoa huduma...Wabongo tuwajinga sana.
Kiukweli tuna safari ndefu sana kuja kupiga hatua. Wiki kadhaa zimepita niliagiza chakula kutoka kwa dada mmoja hivi huwa anapika. Kile chakula kilivyokuja kilikuwa kimewekwa maharage, mchuzi, mbogamboga, nyama, huo ni wali umeletwa hivyo. Nilikifunua nikamrudisha aloniletea nikamwambia hivyo siwezi kula akaja nacho aliyepakua. Maneno aloyazungumza nikamkatisha tu nikamwambia usipate tabu, hiko chakula siwezi kula na nitakilipia urudi nacho. Nilikilipia kile chakula.
 
Back
Top Bottom