Mtandao wa Jumia wafunga biashara yake nchini Tanzania

Mtandao wa Jumia wafunga biashara yake nchini Tanzania

Kwaiyo vyuma vimekaza bongo ila cameroon biashara mbaya? Mshazoea kusema mabaya tuuuu elezeni ukweli basi.
 
Ndio maana biashara za shopping malls huko huwa hazifaulu, utawekeza jengo kubwa lenye maduka lakini ubaki na wahudumu wako kila siku miayo tu, Mtanzania na hela yake hata taxi hataki kutumia, bora abanane kwenye daladala na wamama wanaokwenda kuuza samaki Kivukoni, hajali shombo.
Tanzania tuna utamaduni wetu, mambo ya malls sijui kununua nyanya supermarket sisi (wengi wetu) hatuyafagilii kiivyo. Wabongo tunapenda kwenda sokoni, wale wa kununua kibaba kimoja na nguru huenda sokoni kila siku, wale wakununua vyakula vya mwezi mzima nao huenda sokoni jumamosi.

Na kukuonesha tunavyopenda kununua vitu sokoni tulijenga soko kubwa la kariakoo mwaka 1974 (hakuna kitu kama hicho Afrika). Na kudhihirisha zaidi utamaduni huo ulivyotushika kama luba, serikali hii ya awamu ya 5 inajenga masoko kila wilaya. Wewe utatuambia nini bana?
 
Usilazimishe tufanane mzee.
Unatakiwa ufanye research kwanza kabla ya kuanza businesses.

Kuna vifaa vinauzwa kila kona. Unatakiwa ufa utafiti kwanza kabla ya kuingia biashara.
Biashara zinazofaa online:-
1. Nguo
2. Spear parts
3. Hotel and apartment
Biashara ya chakula TZ utaangukia pua.
Huwezi ukauzwa biscuit, soda, juice, unga, sukari, nyama nk onlie. Uta fail tu.
IMG_20191202_081529.png
Uliisoma taarifa yenyewe? Shida hio hapo wala hamna chakula kimetajwa! Chakula hapa Jumia hakipiti asimilia 5 ya mauzo yao.
Screenshot_2019-12-02-08-13-32.png
These here are items that I have ordered from Jumia. You know what? No food item!
 
Kama hujafanya research huna haki ya kuongea.

Kilichofungwa ni Jumia Market na sio Jumia Food
Mambo ya kununua vitu mitandaoni ni tamaduni ambazo bongo hatuna.

Waswahili tunapenda kushikashika bidhaa kabla ya kununua, tunapenda "kubisha bei", manunuzi ya vitu ni zaidi ya kufanya biashara, kwetu ni "social event". Hayo mambo huwezi kufanya mtandaoni.
 
Kuna wafanya Biashara wengi sana wa Online na hata wengine wapo humu.Kwa ndani ya DSM ukihitaji kitu kwa muda au ndani ya siku husika unakipata.
Nguvu ya Online Marketing kwa Upande wa Insta,Whatsapp na FaceBook na JF.
Kama unakuwa mfanyabiashara halisi na usiye na tamaa..utauza sana.
Shida si kuwa na Daraja la watu wenye kipato kikubwa.Kuna vitu huwa kwa Dunia inavyokimbia na watu wanavyojua mambo.Vitu vikiwa vizuri na vikawa vina akisi bei na ubora wake..kila aina ya watu watakuja tu kwako

1.Uhalisia wa bei za vitu vyao na Ubora wake.

2.Muda wa kupata Mzigo uliohitaji au kuagiza kwa sehemu za karibu pia ilikuwa changamoto.

3.Kitu kikiwa kibovu namna ya kurudishiana ni usumbufu mno.

Customer care ikikosekana kwenye huduma yoyote ile impact yake ni kukimbiwa na watu taraatibu.
Ongeza na Tamaduni zetu ambazo nyingi huona kama anasa kununua vitu online.
Ni kuwasoma wateja na kuelewa mahitaji yao kwa kadri ya taratibu zao.

Teknolojia kwetu inakuja taraatibu na inafanya mageuzi taraatibu hasa kwa nyanja hizo za kibiashara.

Mifano huko nyuma maofisini kutumia Systems tu ilikuwa hatari..lakini angalau kwa sasa watu wengi wamekuwa na msukumo mkubwa sana.
Ni baadhi ya mambo yetu huku Africa..
 
View attachment 1279028Uliisoma taarifa yenyewe? Shida hio hapo wala hamna chakula kimetajwa! Chakula hapa Jumia hakipiti asimilia 5 ya mauzo yao. View attachment 1279033These here are items that I have ordered from Jumia. You know what? No food item!
Kha!! Kijana usitutake tufanane sawa!?
Hatuna mambo hayo TZ. Kila kona kuna maduka na vibada vya kuuza vitu.
Huwezi order kitu online wakati within 100m kinapatikana.

Jifunze kujua culture za sehemu husika.
Usitake tufanane.
 
Mkuu hata ulichoandika hapa kuhusu MABASI YA MWENDOKASI, SHOPPING MALLS na TAX inaonyesha kuna udhaifu mkubwa kwenye tafiti zako, kwa sababu hakuna ukweli hapo. Na kwa maana hiyo kunaweza kuwa na mapungufu pia kwenye hizo tafiti za makampuni ya nje unayoongelea

Tahadhari - usikosee kutumia majibu ya tafiti zilizofanyika Uganda kufanya maamuzi au utelezaji wa miradi Kenya au Tanzania ukidhadhi itakua sawa sababu ya kuwa zote ni nchi za Afrika mashariki. Kila nchi ina tofauti kubwa sana kihistoria na hilo linajenga jamii yenye tofauti flaniflani.....
Amekuelewa ila anahitaji kubisha tu !!!...

Soko la Tanzania ni gumu kiujumla haswa kwa online business. Bahati mbaya wengi wanaangalia hizo figures quantitatively bila kujali consumer behaviour ambayo ndicho kiini...

Ukisema watanzania wana purchasing power ndogo kama sababu nadhani utakuwa hujafanya utafiti kujua ni bidhaa ngapi zinauzwa na kununuliwa kupitia facebook, instagram na whattsap kwa watu binafsi....

Tatizo ni "CONSUMER BEHAVIOUR".
 
Back
Top Bottom