Capt Tamar
JF-Expert Member
- Dec 15, 2011
- 12,340
- 16,383
Ulitegemea kupata huduma nzuri kwenye baa ya Arusha?????!! Shukuru Mungu sana kama huyo mhudumu hakukubandika Tusi moja matata sana
Kama Watumishi ni Wabongo wala sitoshangaa kampuni kukwama.
Mimi huwa napenda sana kufuatilia huduma kila niingiapo Ofisi, Mgahawani, Duka au Usafiri...ninachogundua mara nyingi ukiona huduma ni nzuri na ya kujali Mteja basi anayekuhudumia mara nyingi ndiye mmiliki wa hiyo Ofisi/Duka/Mgahawa n.k.
Ni juzi tu nimeingia Bar moja kubwa tu A town, nikaagiza vinywaji Muhudumu akaleta kisha akakimbilia kuketi meza ya pembeni na kuanza kuchezea simu yake ili hali ile meza ilikuwa chafu..nikamuangalia kwa muda nikiwa nimekasirika sana kisha nikamuita, nikagomba kwamba "hivi huna uwezo wa kuona hii meza ni chafu?" basi akaenda kuchukua kitambaa huku amevuta mdomo utasema nimemtukana tusi la nguoni.
Inashangaza sana Mtu hajui hata kama mimi kuja pale ndio kampuni yake wanapata pesa ya kumlipa mshahara wake.
Ndio ile unakuta Mtu anawekeza kwenye usafirishaji, ananunua Mabasi ya gharama kubwa lakini anaishia kuajiri Wapuuzi watupu kutoa huduma...Wabongo tuwajinga sana.