Mtandao wa Quora unawezekana ukawa sababu ya wakristo wengi wa Ulaya kusilimu na kuwa Waislamu

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hizi habari huwa mnazipata wapi yani wazungu mambo ya dini hawataki kabisa.. Kama ingekuwa hivyo leo wangeruhusiwa kupiga makelele yale ya adhana
 
Ahueni ya maisha inatokana na rasilimali na matumizi mazuri ya rasilimali,haitokani na imani
Mkuu
Hapa tunajadili nini.
Labda ni dadavue
Nimeandika middle east,na afrika magharibu kuna waislamu wengi kuliko wakristo na wengi maeneo hayo huzamia ulaya na america kwenda kutafuta pesa sasa unafikiri wakifika huko makundi kwa makundi unadhani ukristo utaongezea au utapungua
 
QURAN ILIANDIKWA NA WALEVI NA WANYWAJI POMBE NA HAO WALEVI WALIKUWA WAMEKALILI QUR'AN HUKU WAKIWA WAMELEWA CHAKALI NA WENGINE WALIKUFA KWA ULEVI WAANDISHI WA MUHAMMAD

SWALI AYA ZIPI ZILIANDIKWA MASWAHABA WAKIWA HAWAJALEWA POMBE KATIKA SURA 114 ZA QUR-AN YENU?

✔Quran 5:93. Si dhambi juu ya walio amini na wakatenda mema kwa walivyo vila (zamani) maadamu wakichamngu na wakiamini na wakitenda mema, kisha wakachamngu, na wakaamini, kisha wakachamngu na wakafanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao mazuri

Aya ya 5:93 Aya hizi za kukataza ulevi Kwa kashididi hii hizi zimeteremka mwaka wa sita wa Al-hijira baada ya kuwa maswahaba wengi WAMEKUFA na hali ya kuwa WAKILEWA POMBE. Basi maswahaba wengi wenziwao wakawahofia nini itakuwa hali yao siku ya Kiyama [TAFASIRI YA ABDULLAH SALEH AL-FARSY ]
 
O NIMEGUNDUA KUWA WANAOMCHUKIA PAULO NA YESU NI KWA SABABU SHETANI NAYE NI MWISLAM

 
Kwa hiyo hofu yao ni kuenea kwa Uislam au? Na kama ni hivyo wanaogopa nini ?
 
Sipo tayari kupoteza muda kubishana na wewe, mimi nimeleta taarifa iliyohakikiwa nimemaliza. Kama unazani ni utani watume ndugu zako waislam waende Italy kama wahamiaji watakupa mrejesho kamili.
Zimehakikiwa wapi, kijiweni au kwenye kahawa???
weka chanzo cha huu utopolo....
Ndiyo maana nchi nyingine Ulaya zikiongozwa na Italy zimeshtuka na kutunga sera mpya za uhamiaji dhidi ya Muslims.
Hebu weka hizo sera tuzione za Italy zinasema hazitaki wahamiaji waisilamu au pia hizi zimehakikiwa kijiweni ?????
 
Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1








KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)



Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.



Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi. Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...



Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...



Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.



Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.



Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq



Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.



Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.



Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.



Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.



Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.



Hatimaye mwaka 1980 baada ya ukisoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.



Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi yaliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2






Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.



Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.



Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.



Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.



Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.



Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia



RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif




Source : Asadiqmedia
 
Ukiristo haupingui kwa kuongezeka watu wa Imani nyingine
 
[emoji2] Polygamy inasababisha birth rate ya waislamu iwe juu na ndo mnavoongezeka sio kwamba watu wa dini zingine wanahamia kwa wingi. Halafu hatuwezi kuamini hivo vitabu vyenu sababu Sahih al- Bukhari 3175 iko wazi Aisha anahadithia kuwa mtume alirogwa akaanza kuwaza kwamba kafanya mambo ambayo hata hakufanya. Tunawezaje kuiamini akili iliorogwa
 

Source : Trust Me Bro.
 
Quran haikuandikwa na walevi iliandikwa chini ya usimamizi wa mtume kwa masahaba alio wachagua ,Idadi ya waandishi wa Qur-an aliowateua Mtume (s.a.w) ilikuwa 42.

Mtume (s.a.w) alikuwa akiwaamuru waandishi wake wa Qur-an waandike kile alichowasomea, pia aliwaamuru wamsomee walichoandika na alifanya marekebisho pale walipokosea .

Zaidi bin Thabit amesema: "… Kila nilipomaliza kuandika
(Wahyi) Mtume aliniamuru nisome nilichoandika na nilikuwa ninamsomea. Kama palikuwa na kosa alilisahihisha kishaaliwapa watu (kunakili na kuhifadhi vifuani).


Pia Mtume (s.a.w) ndiye aliyewaelekeza waandishi wake
wa Qur-an wazipange aya na sura kama zilivyo katika msahafu tulionao hivi leo kama inavtosema Hadith ifuatayo:

'Uthman bin Affan (r.a) ameeleza: "Ilikuwa kawaida ya
Mtume wa Allah kila aliposhushiwa aya za sura mbali mbali(za Qur-an) au kila aya iliposhuka alimuita mmoja wapo wawaandishi wa Qur-an na kumwambia, "Andika aya hizi katikaSura kadhaa baada ya aya kadhaa."


Kwahiyo hayo unayasema ni kinyume na uhalisia hakuna sahaba aliyekuwa katika Hali ya ulevi wakati wa uandishi wa Quran kwa sababu ulevi ni Haram na mtume asingeruhus haya yatokee na akitokea hiko kitu
QURAN ILIANDIKWA NA WALEVI NA WANYWAJI POMBE NA HAO WALEVI WALIKUWA WAMEKALILI QUR'AN HUKU WAKIWA WAMELEWA CHAKALI NA WENGINE WALIKUFA KWA ULEVI WAANDISHI WA MUHAMMAD.
Hakuna aya zilizo andikwa masahaba wakiwa wamelewa ,labda utuambie aya gani ziliandikwa wakati masahaba wakiwa wamelewa ,pia hio sura 114 sijajua inahusiana vp na mdai yako
SWALI AYA ZIPI ZILIANDIKWA MASWAHABA WAKIWA HAWAJALEWA POMBE KATIKA SURA 114 ZA QUR-AN YENU?
Swala la ulevi ulikuwa ni moja ya maasi makuu na hata baada ya kuja Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayh wa aalihi wa sallam) , baadhi ya Maswahba walikuwa bado wakilewa. Hii ni kwa sababu ilikuwa ni ada na desturi zao walizozirithi, kama zilivyo desturi nyinginezo walizokuwanazo mfano kuwaua watoto wa kike, kuwanyima urithi wanawake n.k..

Akaja mtume na kuondosha dhulma zote hizo. Hivyo jambo kama ulevi lilihitajika hikma ya kuukataza kwa pole pole na ndio maana tunaona kwamba kuna Aya tatu zinazohusiana na makatazo ya ulevi ikianza kwanza kwa kutaja madhara yake na manufaa yake, kisha pole pole hadi kukataza kabisa.

'Umar ibn Al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye alikuwa mmoja wa Maswahaba aliyekuwa akilewa, siku moja alisema: "Ewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)! Tupe hukmu kuhusu Al-Khamr (ulevi), hapo ikateremka Aayah:


((Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake))
[Al-Baqarah: 219]

Wakaendelea kunywa ulevi hadi siku moja katika Swalah, Swahaba mmoja alikosea kusoma Suratul Kaafiruun ndipo ikateremshwa Aayah:


((Enyi mlioamini! Msikaribie Swalah, hali mmelewa, mpaka myajue mnayoyasema))
[An-Nisaa: 43
]

Wakaacha kulewa nyakati za Swalah na wakaendelea nyakati nyingine hadi kukatokea maovu mengine ndipo 'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema tena: 'Ewe Allaah! Tupe Aayah iliyo wazi kabisa
l-Khamr. Ndipo Aayah ya mwisho kuhusu makatazo ya ulevi ikateremshwa
[Tafsiyr ibn Kathiyr]

(
((Enyi mlioamini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shaytwaani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa))
[Al-Maaidah: 90]

Na aya ya mwisho uliyoitoa haizungumzii ulevi na hio sio tafsiri yake ,aya inazungumzia Mwenyezi Mungu kuwasamehe waislamu madhambi waliyokuwa wanayafanya kabla kuwa waislamu kutokana tayari wameshapata uokovu

Tafsiri ya aya
"93. Walio mkubali Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakatenda mema, hawana dhambi kwa vyakula vya halali na vizuri wanavyo kula, wala vya haramu walivyo wahi kula zamani kabla hawajajua kuwa ni haramu, ikiwa wanamkhofu Mwenyezi Mungu na wakajitenga navyo vyakula hivyo baada ya kujua kuwa vinakatazwa. Kisha ikawa wao wakaendelea kumkhofu Mwenyezi Mungu na kuzikubali sharia zake, na kisha wakadumu katika khofu yao ya kumwogopa Mwenyezi Mungu katika kila hali, na wakawa wanafanya a'mali zao kwa usafi wa niya, na kwa njia ya ukamilifu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu huwalipa wenye ikhlasi katika vitendo vyao kwa kadri ya ikhlasi yao na a'mali yao."
Mwisho ukija kijibu comment yangu naomba uje na majibu ya hizi hoja ulizo leta

1.Sahaba gani aliyekufa kwa sababu ya ulevi ?
2.Aya gani ziliandikwa na masahaba wakiwa wamelewa

Ushahidi wa hadithi na historia uzingatiwe
 
Thibitisha Mungu yupo, thibitisha roho ipo.

Thibitisha habari za kuwapo Mungu na roho si hadithi za kutungwa na watu tu.

Hujathibitisha lolote kati ya hayo.
 
Hapana polygamy haina impact kwenye kuongezeka idadi ya watu, nchi zinazoongoza Kwa idadi kubwa ya watu ni china na India na Wala sio za middle east kwanini? Hata Africa ingekuwa ishu ya polygamy basi Tunisia,Morocco,Sudan zingeongoza, hii mikoa ya pwani Kwa hapa Tanzania ndio inayoongoza Kwa waislam lakini nenda Lindi ni Napoli tu watu hamna population inazidi pungua, na kama Iko kingekuwa kigezo basi mtwara ingekuwa na population twice ya Kilimanjaro au mara ambapo waislam unawatafuta
 
Sijamaliza kusoma post yako sababu naona unadanganya. Hapo tu kwenye wanawake na haki umesema uongo kabisa. Nani asiyejua vurugu na mauaji yanayotokea duniani sababu ya imani ya kiislamu? Nani asiyejua wanawake wanavyonyanyasika na kubaguliwa katika uislamu?
 
Umeandika pumba tupu
 
Thibitisha Mungu yupo, thibitisha roho ipo.

Thibitisha habari za kuwapo Mungu na roho si hadithi za kutungwa na watu tu.

Hujathibitisha lolote kati ya hayo.
Sijapanga kukuthibitishia. Mimi ninaamini na nimethibitisha kwamba Mungu yupo na roho ipo, hilo linanitosha.
 
Kijana utaendelea kuonekana kituko, hizo hadithi hazionyeshi ya kuwa watu hawaingii katika Uislamu au hawaukubali au hawashawishiki na Uislamu.

1. Hadithi ya kwanza inaelezea namna Uislamu ulivyo anza kuingia ulikuwa unaonekana ni kitu kipya yaani mgeni, na utarudi ukiwa katika hali hiyo hiyo ya ugeni kama ulivyoanza. Kisha Mtume akasema bishara njema kwa wale watakao onekana wageni, hii inamaanisha ya kuwa hao ndiyo watakuwa sahihi, leo hii Waislamu wako wengi lakini hawaufati ule uislamu sahihi na wale wanao ufata wanaonekana kuwa wameleta dini mpya na hii ndiyo maana ya Hadithi.

Lakini katika mapokezi mengine anasema mtume ya kuwa, hao watakao onekana wageni ni kwa sababu wanatengeneza yale ambayo wameyaharibu watu.

2. Hadithi ya pili inaonyesha zama za mwisho zinapokaribia watu watakuwa na imani haba, na imani itarudi kule ilipoanzia.

3. Hadithi ya tatu ina maana sawa na hadithi ya kwanza.

Sasa hoja yako hapo iko wapi kijana ? Mpaka najiuliza kwanini umetumia hadithi hizi ambazo ziko dhidi yako, ila nahitimisha ni kwa ujinga wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…