KERO Mtandao wa VODACOM umekuwa una shida sana poleni mnaotumia Voda pekee

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Jambo la mwisho; vodacom ndio mtandao wa wezi hasa kwa kutumia mikopo yao ya songesha na nipige tafu.

Ukikopa dakika hii na baada ya dakika moja ukiweka salio au kuweka mpesa unakatwa rejesho na riba kubwa.
Na kwa nini ukope ?

Acha wakukaange na mafuta yako mwenyewe!

Songesha, Nipige Tafu, Saccoss..... vimikopo kopo havina kichwa wala miguu....

sina hela maisha haya, lakini sijawahi kukopa kampuni ya simu... NEVER ONCE

data zikiisha nasubiri nikipata shilingi elfu tatu nyingine naweka kifurushi.....

una chatije na demu kwa data za kukopa ?????
 
Usijua Mzee wangu huwezi kua mwanaume kamili km hujui kukopa, kuna sehemu ukienda kuchukua jiko unaulizwa umeshawahi kukopa? Siku hio ndio unachumbia unatwangwa swali hilo halafu wanakusikiliza unavyojikanyaga
 
Umejipataa😂
 
Siku hizi hatushobokei mademu wewe pimbi🤣
 
Ukiacha Voda,mtandao gani mwingine una internet yenye Kasi na ambayo haisumbui?

Hii kampuni ya majizi imekuwa shida sana
 
Usijua Mzee wangu huwezi kua mwanaume kamili km hujui kukopa, kuna sehemu ukienda kuchukua jiko unaulizwa umeshawahi kukopa? Siku hio ndio unachumbia unatwangwa swali hilo halafu wanakusikiliza unavyojikanyaga
Wanasemaga mtu ambaye hajawahi kudaiwa anashida kwenye ubongo.
Siwezi nikawa nimeishiwa MB na nipo sehemu mbaya au labda usiku sana na kuna document natakiwa kutuma halafu nikasema mpaka nifike mjini au mpaka kukuche ndio nitume kwa sababu sitaki kukopa.

Hicho kichwa kinakuwa kinaitesa sana shingo.
 
@vodacom
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…