GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
"Kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo nitakuwa nafanya Kipindi cha Sports Arena ambacho kitakuwa hewani kuanzia saa mbili hadi saa tano asubuhi, lakini pia nitakuwa nasoma magazeti kwenye kipindi cha asubuhi saa moja na nusu" Maulid Kitenge, @mshambuliaji Akitangaza kuhamia Wasafi FM
Chanzo Taarifa: Mtandao wa Darmpya
GENTAMYCINE namtakia Kila la Kheri huko japo naona wazi ' Anguko ' la Efm hasa katika Vipindi vyake vya Michezo na najua kuwa Wachambuzi ' mahiri ' wa Michezo nchini kama mwana Simba mwenzangu Oscar Oscar nae atamfuata huko na huenda hata Mwanadada mwana Simba na mwana Liverpool mwenzangu Tunu Hassan Shemkome nae akaungana nae na wengineo.
Ukiachia mbali kuwa Maulid Kitenge huwa ananikera kwa Mahaba yake Kupitiliza kwa Yanga SC yake ila Kiutendaji ni Mtangazaji wa Michezo bora kabisa na mwenye Kipaji cha hali ya Juu na Mvuto wa Kipekee kabisa ambao unamfanya kila awapo awavutie Wasikilizaji wengi.