Mtangazaji Maulid Kitenge ahamia WASAFI FM akitokea EFM

Mtangazaji Maulid Kitenge ahamia WASAFI FM akitokea EFM

pigo kubwa kwa E FM, alikuwa anaibeba E FM, hats hivyo muosha huoshwa, walimuondoa radio one, wakajua wamewin, so mchezo hauitaji hasira. mond tuletee osca osca, Edo kumwembe, Jeff laya, ediga kibwana. hapo umemaliza redio zote
A. Mchomvu aka baba john
 
Sorry kaka, Sammisago yuko wapi?.Nadhani unajua taatifa nyingi
 
Punde atawasiri na Edo Kumwembe pamoja Maestro hapo ni upande wa kuchambua na kudadavua michezo

Kitenge na Masoud haziivi Kivile ( na hata Uhusiano wao ulikuwa ni wa Kinafiki zaidi ) kwani pamoja na kwamba Masoud ' Maestro ' ana Kipaji cha Utangazaji ila ni Mtu wa Majungu mno na mpenda mambo ya ' Kiutamaduni / Kienyeji ' sana kwa Wenzake ili Yeye tu ndiyo awe juu na mwenye Sauti sababu ambayo pia ilimgharimu alipokuwa CMG na kupata wakati mgumu kutoka kwa Watangazaji aliokuwa nao kule. Na pia ana Sifa ya Ugombanishi kwa Wenzake, Mbaguzi na Mdini mno.
 
Na ni ' bai bai ' kweli Mkuu kwani Maulid Kitenge huwa ana ' Nyota ' kali sana ya ' Kimvuto ' na Utangazaji wa ' Kiushawishi ' kuliko Watangazaji wote wa Michezo nchini Tanzania. Kwa tunaoijua vyema hii ' Tasnia ' na tukiwa ' tumetukuka ' nayo pia vile vile tunasema rasmi kuwa Maulid Kitenge ameacha Msiba wa Kiutangazaji Habari za Michezo hapo Efm na sijaona bado mbadala wake japo najua kuwa Mtangazaji mwenzie na mwana Simba mwenzangu Ibrahim Masoud ' Maestro ' ndiyo sasa atakuwa ' Boss ' wa Dawati la Michezo Efm ila hana ' Ushawishi ' na ' Mvuto ' kama aliokuwa nao Maulid Baraka Kitenge na hicho Kipindi chao cha ' Sports Headquarters ' na kile cha ' E Sports ' kitaanza Kukosa Mvuto labda Efm na ' Maestro ' waje na ' Strategy ' mpya. Ngoja nami GENTAMYCINE nianze sasa Kujilazimisha na Kuzoea Kusikiliza Wasafi fm Radio ili hadi Jumatatu ijayo niwe nimeizoea na Maulid Kitenge akianza Kutangaza nitiririke na niserereke nae kama ambavyo ilivyokuwa akiwa na Efm.
Watamchukua Haji Manara kuziba pengo kwani wote ni waandishi wa habari walioanzia mchangani,Maulidi alianzia gazeti la Mfanyakazi,kama umewahi kulisoma gazeti hili basi wewe ni mhenga kama Maulidi Kitenge.
 
Ila hawa wakawaida sana si kama pengo aliloacha Maulidi! Jamaa amekuwa vizuri sana tangu enzi zile akiwa redio one! Kila la kheri kocha mchezaji sijui huko Wasafi utakuja na jina gani?
 
Ila sijui kwanini mpaka leo wasafi fm hawapo online.? Kama wapo naomba link tafadhali
 
ID yako ni Yusuph Hashim na unayemuongelea hapa ni Yusuph Mkule. Wenye Akili pana na Wazoefu wa ID's hapa Jamvini tayari tumeshajiongeza na labda tu na Mimi nianze Kukupa Pongezi zako Yusuph kama nawe utamfuta huko Wasafi fm aliyekuwa Bosi wako hapo Efm Maulid Kitenge. Je, baada ya Wewe Kuwaaga hapo Efm nawe tukutegemee lini Kutangaza rasmi kuwa umetua hapo Wasafi fm? Nitashukuru ukinijibu Mkuu kwani Saa 1 na Robo ( yaani na dakika 15 ) nitakuwa natoka hapa ( Log Out ) hadi tena Saa 4 Kamili Usiku baadae ambapo nitarejea tena Kuliendeleza hapa JamiiForums.
[emoji23][emoji23][emoji23] Sheikh Ni Yule Yule
 
Hana ubora wowote zaidi ya kelele tu.
Kitenge atazunguka weeee ila sehemu pekee atayotulia ni AZAM TV trust me! Hapo anafanya kumvutia tu bakhresa ili siku akimtajia dau la 6+ million per month mzee wetu asichomoe.
 
Huko wasafi wangeanza na watoto wadogo wanaoweza kufanya mambo ya kijinga kijinga yanayopendwa na visichana vidogo visivyojielewa,ambavyo vina ndoto ya kuja kupiga picha za utupu siku moja na kuziweka insta.
Visichana hivyo vina wafuasi wengi wanaume waliokwisha kuwa brainwashed na ujinga wa wazungu na mfumo wa maisha wa leo duniani.

Kizazi cha akina Maulid sioni wakisikiliza hiyo redio wasafi.Mimi ni mmoja wapo.

Nina kumbu kumbu nzuri na watangazaji wa awali wa FM redio ikiwemo akina Charlz Hilary,Abdalah Majura,marehemu Misanya Bingi,na wengineo wengi ambao najua wana mvuto kwa watu wa kizazi kile zaidi.Maulid kitenge ni mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho.
Sasa najiuliza huko wasafi,na falsafa yao ya muziki wa matusi unaovutia visichana,nani atamfuata huko?
Ila kama ni maslahi namtakia kila la heri.
 
Umeambiwa naishi nae au? Umeuliza Swali Kinafiki na ndiyo maana nami sasa nakujibu Kisela, hivyo hapa ngoma ni ' droo ' tu sawa?
Sifaham chochote ndio maana nikaanza na samahani, sababu kubwa nafahamu unajua mambo mengi kuhusu media za bongo
 
Bila Shaka wasafi FM wata heshimu Trip za nje ya nchi za kila wiki za Edo na Kitenge.Kule mavingu FM aka Wafu FM hali Ina zidi kuwa mbaya baada ya wasafi kutikisa EFM sasa itakuwa zamu ya Wafu FM.
Vipi Wasafi fm wameweza kuwazima Wafu fm.?
 
Nakuaminia mzee wa kutoa point aka IQ kubwa utababiri wako wa kitenge kwenda wasafi umetimia dah kwa investment wanaofanya wasafi naona itakuwa media kubwa Sana imagine wanafanya haya ikiwa hata miaka 2 hawajafikisha.
Vipi tayari wamekuwa wakubwa!?
 
Maulid Kitenge ni mtangazji mwenye mbwembwe lakini si mchambuzi mahiri...

Kama kutangaza tu habari za michezo kwa mikogo, jamaa yupo vizuri...

Lakini si mahiri katika kuchambua sayansi na ufundi wa michezo kwa mapana yake...

Wasafi wakitaka kuteka masikio ya wadau wa michezo basi hawana budi kutafuta pia akili za watu wenye kuchambua michezo kama Edo (soka) au yule bwana mdogo Geff (michezo yote) n.k.
Edo sio mchambuzi mzuri wa soka. Yeye ni mahiri kwa historia ya soka ila sio kuchambua kinachotokea kwenye pitch.
 
View attachment 1236665

"Kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo nitakuwa nafanya Kipindi cha Sports Arena ambacho kitakuwa hewani kuanzia saa mbili hadi saa tano asubuhi, lakini pia nitakuwa nasoma magazeti kwenye kipindi cha asubuhi saa moja na nusu" Maulid Kitenge, @mshambuliaji Akitangaza kuhamia Wasafi FM

Chanzo Taarifa: Mtandao wa Darmpya

GENTAMYCINE namtakia Kila la Kheri huko japo naona wazi ' Anguko ' la Efm hasa katika Vipindi vyake vya Michezo na najua kuwa Wachambuzi ' mahiri ' wa Michezo nchini kama mwana Simba mwenzangu Oscar Oscar nae atamfuata huko na huenda hata Mwanadada mwana Simba na mwana Liverpool mwenzangu Tunu Hassan Shemkome nae akaungana nae na wengineo.

Ukiachia mbali kuwa Maulid Kitenge huwa ananikera kwa Mahaba yake Kupitiliza kwa Yanga SC yake ila Kiutendaji ni Mtangazaji wa Michezo bora kabisa na mwenye Kipaji cha hali ya Juu na Mvuto wa Kipekee kabisa ambao unamfanya kila awapo awavutie Wasikilizaji wengi.
A
Na ni ' bai bai ' kweli Mkuu kwani Maulid Kitenge huwa ana ' Nyota ' kali sana ya ' Kimvuto ' na Utangazaji wa ' Kiushawishi ' kuliko Watangazaji wote wa Michezo nchini Tanzania. Kwa tunaoijua vyema hii ' Tasnia ' na tukiwa ' tumetukuka ' nayo pia vile vile tunasema rasmi kuwa Maulid Kitenge ameacha Msiba wa Kiutangazaji Habari za Michezo hapo Efm na sijaona bado mbadala wake japo najua kuwa Mtangazaji mwenzie na mwana Simba mwenzangu Ibrahim Masoud ' Maestro ' ndiyo sasa atakuwa ' Boss ' wa Dawati la Michezo Efm ila hana ' Ushawishi ' na ' Mvuto ' kama aliokuwa nao Maulid Baraka Kitenge na hicho Kipindi chao cha ' Sports Headquarters ' na kile cha ' E Sports ' kitaanza Kukosa Mvuto labda Efm na ' Maestro ' waje na ' Strategy ' mpya. Ngoja nami GENTAMYCINE nianze sasa Kujilazimisha na Kuzoea Kusikiliza Wasafi fm Radio ili hadi Jumatatu ijayo niwe nimeizoea na Maulid Kitenge akianza Kutangaza nitiririke na niserereke nae kama ambavyo ilivyokuwa akiwa na Efm.
Naambiwa karudi tena Wasafi
 
Back
Top Bottom