Mtangazaji Maulid Kitenge ahamia WASAFI FM akitokea EFM

Mtangazaji Maulid Kitenge ahamia WASAFI FM akitokea EFM

Kusaga hawezi haribu redio yake.
Bila Shaka wasafi FM wata heshimu Trip za nje ya nchi za kila wiki za Edo na Kitenge.Kule mavingu FM aka Wafu FM hali Ina zidi kuwa mbaya baada ya wasafi kutikisa EFM sasa itakuwa zamu ya Wafu FM.
 
Watu wanaangalia mpunga mwingi sio kingine na kwa taarifa yako sio yy tu wako wengine wamehamia hapo wasafi achana na pesa baba kitu kingine ngoja kuanzia j3 utamsikia akiunguruma kupitia mawimbi ya wasafi fm
View attachment 1236321
View attachment 1236296

Je kwa umri alionao yawezekana akavunja rekodi ya kuhama ?
tapatalk_1571336594996.jpeg
tapatalk_1571336034495.jpeg
5d46a8b9a8474321a6528dadf9aa1c38.jpeg
Screenshot_20191017-193316_Chrome.jpeg
Screenshot_20191017-193326_Chrome.jpeg
 
Huyu Kitenge mbona anahamahama sana vituo vya kazi?. Mwisho wa siku atajikuta anarudi Redio one. Ila namtakia mema huko alipohamia. Hajaacha pengo kubwa kwa kuwa Efm kwa sasa inajimudu imeifunika sana Clouds na kiuchambuzi wapo vizuri.
hizo radio kongwa mtu akishatoka ametoka, huwa hana hamu ya kurudi tena. Hata radio zenyewe huwa hazifanyi usajili wa kutisha, zenyewe zinawaibua tu watangazaji.
 
Kitenge atazunguka weeee ila sehemu pekee atayotulia ni AZAM TV trust me! Hapo anafanya kumvutia tu bakhresa ili siku akimtajia dau la 6+ million per month mzee wetu asichomoe.
 
Tunu ameondoka nae n official ila Oscar bado sijajua
 
pigo kubwa kwa E FM, alikuwa anaibeba E FM, hats hivyo muosha huoshwa, walimuondoa radio one, wakajua wamewin, so mchezo hauitaji hasira. mond tuletee osca osca, Edo kumwembe, Jeff laya, ediga kibwana. hapo umemaliza redio zote
 
Tunu ameondoka nae n official ila Oscar bado sijajua

Hakuna Mchambuzi ambaye anapendwa na Maulid Kitenge kama Oscar Oscar na kama haitoshi pia Wawili hawa ni Marafiki Wakubwa mno nje ya Kazi. Kama kuna Mtu ambaye Mchambuzi Oscar Oscar anamshukuru kwa Kumbadilishia Maisha yake kutoka yale aliyokuwa nayo ya Taabu ( Msoto ) kutokana na kuwa ni Mwalimu Kitaaluma huku akiwa anafundisha Shule Moja Wilaya ya Kinondoni basi ni Maulid Kitenge. Bila Kitenge Kumbeba ' Kiutendaji ' Mchambuzi Oscar Oscar hadi hivi leo angeendelea kuwa na Maisha yake yale yale ya ' Msoto ' na Ualimu wake na huko Kupanda zake Ndege mara kwa mara na Kutembea nchi mbalimbali kama South Africa, England, Spain na United States angekusikia tu Redioni au huko Kwao Kaliua Mkoani Tabora au hata tu Kupata Kwake pia Kazi ya Utangazaji / Uchambuzi huko Super Sports ( Dstv ) pia angekusikia katika ' Bomba ' tu. Mafanikio ya sasa ya Kimaisha ya Mchambuzi Oscar Oscar kwa kiasi Kikubwa yamechangiwa na Urafiki wake mkubwa na Kusaidiwa mno na aliyekuwa ' Boss ' wake hapo Efm Maulid Baraka Kitenge.

Sishangai kusikia kuwa Mtangazaji Tunu Hassan Shemkome amemfuata Maulid Kitenge huko Wasafi fm kwani tokea alipokuwa Chuoni ( Ilala ) Tunu Shemkome alikuwa ' akimuhusudu ' mno Kiutendaji na hata Kimahaba Maulid Kitenge na haikushangaza kuona hata pale Tunu alipokuwa akifanya Kazi Uhuru fm ( akitangaza hasa Kipindi cha Michezo akishirikiana na Mtangazi wa Michezo wa Clouds fm na Clouds tv Fatma Likwata ) alijiweka Kiukaribu hasa wa ' Kiumahaba ' na Maulid Kitenge kiasi kwamba Kitenge alipohamia tu Efm na kuwa ' Boss ' wa Dawati la Michezo hakutaka Kupoteza muda na haraka sana alimtoa Tunu Uhuru fm na akamsajiili hapo Efm huku akianza Kumtengeneza vyema ili ' afiti ' kisawasawa katika hicho Kipindi Jukumu ambalo alifanikiwa nalo na sasa Tunu Hassan Shemkome yupo vizuri. Nje ya Kazi Wawili hawa pia wana ule Uhusiano wa ' Kibaiolojia ' japo mwanzoni walijitahidi Kuficha ila walisahau kuwa Siku zote Mapenzi hata uyafiche vipi hayafichiki na kuna Siku tu yatagundulika.

Nina mengi juu ya hawa Wawili na Maisha yao mengi nje ya Kazi ( Majukumu ) ila kwa leo naomba niishie hapa tafadhali.
 
Punde atawasiri na Edo Kumwembe pamoja Maestro hapo ni upande wa kuchambua na kudadavua michezo
 
Back
Top Bottom