humphrey_on_th_forum
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 278
- 233
Ni kweli aiseee...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu Kitenge mbona anahamahama sana vituo vya kazi?. Mwisho wa siku atajikuta anarudi Redio one. Ila namtakia mema huko alipohamia. Hajaacha pengo kubwa kwa kuwa Efm kwa sasa inajimudu imeifunika sana Clouds na kiuchambuzi wapo vizuri.
Acha kumlinganisha Koffi Charles Olomide na huo upumbavu wako.. Mtusi wewe.Mkuu Akili zako timamu ziko Likizo ya Kudumu au? Hivi kama kule Radio One labda alikuwa akipewa Mshahara wa Tsh 500,000/= alivyohamia Efm akawa labda analipwa Mshahara wa Tsh 3,000,000/= na huenda hapo Wasafi fm atakuwa analipwa Mshahara wa Tsh 5,000,000/= kwahiyo Wewe ulimtaka asihamehame ili azidi Kufanana ' Kiumbayuwayu / Kiumasikini ' na Wewe au?
Hoja yako kuwa Kuondoka Kwake hapo Efm hakutaacha Pengo lolote lile kwakuwa wameshajidhatiti kwa kuwa na Wachambuzi wengi si kweli. Kumbuka hata Mwanamuziki Nguli Afrika Koffi Olomide alikuwa juu Kimuziki hasa pale alipokuwa na Waimbaji ' Mafundi ' kabisa na wenye Mvuto akina Fally Ipupa na Ferre Gola ila baada ya Kuondoka katika Bendi yake ya Quarter Latin hivi sasa Koffi anapata taabu mno Kimuziki na hata akiwa anahojiwa mara kwa mara huwa haachi kuwataja hawa akina Fally na Ferre kuwa walikuwa wakimbeba Kimuziki.
Sikatai kuwa hata hao Watangazaji waliobakia hapo Efm ni wazuri ila tusifichane hata katika Timu mnaweza mkawa Wachezaji wote ni wazuri ila kuna Mmoja wenu ndiyo huwa anakuwa amebeba ' Nyota ' nzima ya Kikosi chenu na kwamba bila Yeye huwa mnaona ni kama vile hamjatimia kabisa. Kuna Watu wengine Mwenyezi Mungu huwa anakuwa amewaumba na Shani zao ( Charismatic ) tu hivyo popote pale wakiwepo lazima kutakuwa na Mvuto fulani na Maulidi Kitenge ana hiyo ' Charm ' kataa uwezavyo.
Namalizia kukupa Mfano mwingine halisi wa Bendi yangu pendwa kabisa ya Kikongo ya Wenge Musica BCBG chini yake Kipenzi changu Mwanamuziki Jean Bedele Tshituka Mpiana ( JB Mpiana ) Ni bendi ambayo ina Waghani ( Marapa ) Kikongo wanawaita ' Atalakus ' na Kifaransa wanawaita ' Animateurs ' ambapo hii Bendi inao Marapa kama Watano hivi kuanzia na Rapa Kiongozi aitwae Pishou Lisimo a.k.a GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ( ambaye hata hii ID nimechukua Jina kutoka Kwake ) kisha kulikuwa na Marehemu Faustine Nzinga Yankobo a.k.a CELLULAIRE kisha akawepo Noah Mukendi Kilimandjaro, kisha yupo Fusee De Gaire, yupo Pajo na anamalizia kuwepo Bin Laden lakini katika Wote hao Bendi hii haijakamilika na huwa haijazi Watu popote pale ikienda Kupiga iwe hapa hapa Barani Afrika au Ulaya kama haiambatani na huyu Rapa Pishou Lisimo ( GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ) na ndiyo maana hata baada ya JB Mpiana kulijua hilo ndiyo Mwanamuziki anayemlipa Pesa nyingi ndani ya hiyo Bendi yake akifuatiwa na Mpiga Drums wake Seguen Mignon Maniata kisha Mpiga Gitaa la Solo wake Ficarre Mwamba ( baada ya Mpinzani wake mkubwa kwa Upigaji Gitaa la Solo Shevchenko Patou Solo Kuacha Muziki na Kumfuata Mkewe Mlokole huko nchini Ufaransa ) na wa mwisho kulipwa juu ni Mwimbaji wake ambaye pia ni Mwalimu wa Chuo Kikuu Kinshasa wa Somo la Kifaransa na Muziki aitwae Jules Kibens a.k.a Molongeshi a.k.a Le Professeur.
Mziki wowote ule wa Sebene ( Kuchangamka na wa Haraka ) ukipigwa wa Bendi ya Wenge Musica BCBG kisha upande wa Kughani ( Kurapu ) akisimama Mwenyewe GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ( Pishou Lisimo ) ni lazima tu hata Wewe utaamka Kitini na hutakaa kwani ana Kipaji Kikubwa cha Kuchangamsha muda wote na Kuwaamsheni huku mkitamani muda wote tu awe anarapu ( anaghani ) hali ambayo humfanya JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG Kukubalika na Kupendwa na Watu wengi wanaoujua Mziki na Wapenzi wa Miziki hii ya Kongo duniani kote.
Nyota ya Mtangazaji Nguli wa Michezo nchini Maulid Baraka Kitenge ilikuwa ni Kali na ndiyo iliibeba mno na sana tu hiyo Efm Radio na hata Wao wenyewe wanajua hilo.
Kijitonyama wameingia na huko sasa
This is Tanzania
Huyo ni kma Pepe Gadiola kenye soka... Ukitaka Huduma yale yazima mfuko utoboke.Huyu Kitenge mbona anahamahama sana vituo vya kazi?. Mwisho wa siku atajikuta anarudi Redio one. Ila namtakia mema huko alipohamia. Hajaacha pengo kubwa kwa kuwa Efm kwa sasa inajimudu imeifunika sana Clouds na kiuchambuzi wapo vizuri.
Ni kweli aiseee...View attachment 1236291
Kijitonyama wameingia na huko sasa
This is Tanzania
Hata Yusuph Mkule naye atakuwa anaelekea huko huko. Maana alishaaga pale Efm
Kwa mkuuuHivi kuna mtu huwa anasikiliza hiyo wasafi?
HujaelewekaaaKijitonyama wameingia na huko sasa
This is Tanzania
Kikubwa maslahi.
Hujaelewekaaa
Nakuaminia mzee wa kutoa point aka IQ kubwa utababiri wako wa kitenge kwenda wasafi umetimia dah kwa investment wanaofanya wasafi naona itakuwa media kubwa Sana imagine wanafanya haya ikiwa hata miaka 2 hawajafikisha.ID yako ni Yusuph Hashim na unayemuongelea hapa ni Yusuph Mkule. Wenye Akili pana na Wazoefu wa ID's hapa Jamvini tayari tumeshajiongeza na labda tu na Mimi nianze Kukupa Pongezi zako Yusuph kama nawe utamfuta huko Wasafi fm aliyekuwa Bosi wako hapo Efm Maulid Kitenge. Je, baada ya Wewe Kuwaaga hapo Efm nawe tukutegemee lini Kutangaza rasmi kuwa umetua hapo Wasafi fm? Nitashukuru ukinijibu Mkuu kwani Saa 1 na Robo ( yaani na dakika 15 ) nitakuwa natoka hapa ( Log Out ) hadi tena Saa 4 Kamili Usiku baadae ambapo nitarejea tena Kuliendeleza hapa JamiiForums.
Kumbe Maulid wa Kitenge ni mtu wa Usalama wa Taifa!!!!!!!!!!!Najua wengi hapa hawajakuelewa ila tunaomjua vyema Maulid Baraka Kitenge na Kazi yake nyingine huko Wasafi fm wawe makini. Naomba niishie hapa tafadhali.
Kumbe Maulid wa Kitenge ni mtu wa Usalama wa Taifa!!!!!!!!!!!
ni kweli mkuuKikubwa maslahi.