Mtangazaji na DJ wa East Africa Radio, Baba T atimiza miaka 81

Mtangazaji na DJ wa East Africa Radio, Baba T atimiza miaka 81

Moja ya vitu vinavyo inspire wengine ni appreciation kwa watu kama hawa. Ukiangalia MTV au BET jinsi wenzetu wanavyothamini legendary kama hawa ni baraka tosha na inspiration kwa wengine. How kitu kikubwa hivi kinapita kirahisi hivi tena kwa mtu wa media? Hivi hawa watu wa media wasipokumbukana nani awakumbuke kwanza?

CC pasco na wadau wengine ...
Huyo si ndo ktk nyimbo "Rasta km Baba T"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Happy birthday Legendary Baba T. Lovers rock tunaipenda sana! Tena sana. Rudisheni basi Road block ya Gotta Irie na Reggae asylum ya 'Sis Dread hizo show zilinifanya nikawa crazy wa East Africa Radio
 
Kutoka EATV facebook wall,

Kwa mara nyingine tumebarikiwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mfanyakazi mwenzetu mwenye umri mrefu zaidi hapa ofisini. Jina lake halisi ni Emsly Smith maarufu kama Baba T.

Baba T ni Dj wa muziki wa Reggae na pia ni mtangazaji wa kipindi cha 'Lovers Rock' cha East Africa Radio. Leo ametimiza miaka 81 na bado ana nguvu kama unavyomuona kwenye picha.

Baba T ni mtu mwenye upendo kwa kila mmoja, kila siku asubuhi anapofika ofisini huwagawia wafanyakazi wa kike wote biskuti za chocolate, na wanaume huwa anawapa vipande vya nazi.

Happy Birthday Baba T. Live long Rasta Man.

View attachment 1393114

My take;

Kiukweli nimemfahamu Baba T miaka mingi kidogo nikiwa mfatiliaji wa vipindi vya burudani enzi hizo lakini sikuwahi ku note his age. Nimeshtuka mno kama kwenye media, tasnia ya utangazaji, na kama DJ wa muziki wa raggae Baba T anatimiza miaka 81 akiwa bado active kwenye industry alafu ni kama wadau wa media na entertainment wanachukulia poa mno. Hata hii birthday yake inapita kirahisi mno

Watanzania tujifunze kukubali vyetu! Tunahitaji kuonesha heshima na appreciation kwa huyu mzee akiwa hai. Wadau wa media na burudani kama mnapita hapa ...please tumuenzi huyu mzee

Happy birthday Baba T
Dah! mmoja wa watu ninaowakubali sanaa haswa kwenye mambo ya Reggae! kuna siku alipiga mix moja hivi ya "Lovers Rock" sikaa niisahau. Long Live Rasta Man!
 
Ndio faida za kula mboga za majani na matunda kwa wingi, kuepuka njaa, pombe na masigara...
Happy Bday Baba T...
A true legend
 
Back
Top Bottom