Mtangazaji wa Clouds alalamikia kutishiwa na Haji Manara

Acheni kushabikia mambo ya kijinga,nje ya Simba na Yanga sote ni Watanzania,sote ni binadamu.Alichokifanya Haji si cha kiungwana. Michezo ni furaha na Upendo si uadui.
Safi sana. Umeongea kama great thinker na aina ya mtu sahihi kuwepo JF. Bahati mbaya JF inabeba kila aina ya taka. Kuna comments mpaka unashangaa.
 
Ukiwa msemaji hautakiwi kuwa na hasira.

Kwani jamaa (Manara) ana taaluma ya uandishi wa habari au taaluma yoyote inayohusiana na mawasaliano ya umma?
 
Manara hana professionalism..... Huwezi ku-attack mwandishi tena ukisema nilikuwa nakutafuta wewe na nitakudhalilisha. Huwezi kuleta mambo personal kwenye press conference ya taasisi. In short anaikosea adabu Simba.
 
Acheni kushabikia mambo ya kijinga,nje ya Simba na Yanga sote ni Watanzania,sote ni binadamu.Alichokifanya Haji si cha kiungwana. Michezo ni furaha na Upendo si uadui.
Mkuu hivi umesoma vyema kweli maelezo tokea mwanzo mpaka mwisho? Haji kaanza kupanic kabla hata ya kuongea huyo Prisca. Lilipoulizwa swali juu ya wastani mzuri wa Yanga kupata matokeo kwa kuangalia mechi tatu za mwisho ndipo Haji akachafukwa
 
Ukiwa msemaji hautakiwi kuwa na hasira.

Kwani jamaa (Manara) ana taaluma ya uandishi wa habari au taaluma yoyote inayohusiana na mawasaliano ya umma?
Mimi sijui taaluma yake hilo swali wangeulizwa waliomuajiri vigezo vyao, mimi nasema haijalishi wewe umesomea nini lakini unapowakilisha taasisi kubwa basi ni lazima ujiheshimu na uheshimu wengine ni simple logic wala haihitaji degree.
 
Ipo shida hapa hii nafasi ya Hajji inahitaji hekima, busara, ukomavu na ustahimilivu, angeweza kujibu hilo sijibu ni swali la uchokozi, sipo tayari kukuudhi kwenye hadhara. Kama mwana Simba this has been outright thoughts. Japo nyuma ya pazia kama kuna namna ni maadui wa Simba angewachana nyie ni chawa wa Utopolo bora nisijibu nikikujibu utaudhika. #Hajji_Manara_Reform_Behave_Professionally_with_Perseverence.
 
Manara ni kielelezo kuwa kuna watu wasio sahihi kwenye nafasi muhimu.

Pia uongozi wa Simba kushindwa kuchukua hatua yoyote kwa Manara muda wote inaonyesha wao ni wa ovyo pia.

Madhaifu ya ki-uongozi ya hizi timu zetu yanafichwa sana na matokeo ya uwanjani zaidi ya hapo hakuna jipya wanafanya.
 
Leo Haji Yupo EFM Radio live kwenye kipindi cha Sports HQ
 
Ukiwa msemaji hautakiwi kuwa na hasira.

Kwani jamaa (Manara) ana taaluma ya uandishi wa habari au taaluma yoyote inayohusiana na mawasaliano ya umma?
Mawasilianao ya madrasa
 
Hivi ni kweli mechi tatu za ligi za mwisho yanga aliibuka kinara?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…