TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

ujumbe murua kabisa. bila shaka wew ndo wa kwanza kuuandika. Zaidi ya watu 20 nimeona wameweka status whatsup na wengine wengi wameuweka instagram.
Maisha haya ni mafupi,,Ukipata nafasi ya kumwambia mtu unampenda mwambie,akiumwa kampe pole,akikuomba msamaha samehe.,ukimkumbuka mjulie hali..Usiyape majivuno nafasi,tuna muda mchache duniani...
*Uhai ni zawadi, kifo ni lazima..* huu ujumbe utakusaidia sana kwenye Maisha yako

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inauma sana kwa kweli yaani ni mshituko ambao sijawahi pata

Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu Ephraim Kibonde mahali pema peponi
Pole sana mfiwa inabidi ukubaliane na hali halisi

.
 
WAJUZI WA MAMBO KUNA UKWELI NDANI YA HILI?? ..
PSX_20190307_131602.jpg
PSX_20190307_131602.jpg
 

Habari za hivi punde ni kuwa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Ndugu Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019.

Kibonde alianza kusumbuliwa na presha akiwa katika msiba wa marehebu Ruge Mutahaba huko Bukoba mkoani Kagera na kuhamishiwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambapo mauti yamemkuta.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa

Mwaka jana Ephraim Kibonde alimpoteza mkewe mama Sara Kibonde. Zaidi soma >TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde - JamiiForums

View attachment 1039958
Ephraim Kibonde akiwa na mkewe enzi za uhai wao​
Wapumzike Kwa Amani ! bwana Kawapenda Zaidi.....
 
Jamani alikuwa mc bukoba alimuaga ruge kwa uchungu dah.rip kibonde msalimie ruge mwambie yote alofanyiwa na wa tz
 
Kibonde ni mtu wa m
Ni kwa familia ya marehemu pekee ndio kunakuwa na tatizo, haitoki nje ya familia ya marehemu. Kwani Kimbonde alikuwa ndugu wa Ruge?

Kibonde ni mtu wa Mbeya hivyo sidhani kama wana undugu wowote.
 
Hivi yule Kibonde kwao ni wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Amekulia upanga opposite na muhimbili Primary,kwa sasa wazazi wake Mr & Mrs Samson Kibonde wako mbezi beach.ila asili yao ni wanyakyusa wa Tukuyu kuna kijiji kinaitwa Itete kipo Kyimo (K.K) babu yake mzee Job kibonde alihamia katika kijiji cha Ndolesi vuwwa wilaya ni Mbozi mkoa mpya wa Songwe na kuanzisha Mji wake huko miaka 1920 au 1930.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom