Mtanzania aliyeuawa na Hamas alikuwa sehemu ya jeshi la Israel? Serikali itoe tamko Watanzania wangapi wameingizwa kwenye jeshi la Israel

Huyo kaka awe MTz au sio mtz hakustahili kuuawa vile
 
swali langu ni rahisi sana, waliouwawa kwenye mashambulizi ya Hamas ndani ya Israel ni wengi sana, kwanini hili la mtanzania ndio linaonekana kubwa na kusambaa mno?
Nafikiri sababu ni "War Propagandas" zinazofanywa na wafuasi wa kundi la kigaidi la Hamas ili kujaribu kuhalalisha uovu wao waliofanya huko Israel. Nothing more nothing less!
 
Swali langu ni moja tu!
Kwanini avae Boxer ya Jeshi?
Hasa kwenye nchi yenye vita?
 
Hata kama hakuwa na silaha yoyote ukikamatwa kwenye battlefield ukiwa na nguo za kiraia wewe ni jasusi na jasusi hukumu yake ni kuuawa. Yule angekuwa askari halisi wa Israel asingeuawa bali wangemchukua mateka.
 
Hata Tarimo watu walijua yupo Urusi kama mwanafunzi lakini alipouawa kule Bakhmut ndipo ukweli ulipodhihiri kuwa alikuwa akipigana upande wa Urusi.
Nimeeleza kwa kukumbushia sababu ya yeye kukutwa na umauti uwanja wa vita na ilielezwa .

Pia Tarimo alikuwa mwanafunzi kweli na sio mwanajeshi

Baada ya kwenda kusoma alipatakana hatiani na kuwekwa gerezani

Ipo option ya wafungwa kuachiwa kwa baadhi ya nchi kama wakiamua kuingia vitani na yeye ndii alichagua na pia hakuwa jeshi la urusi bali wale huitwa mercenaries wa Wagner group .
 
Wagner ni professional soldiers na wanapigana upande wa Urusi. Pia, wapiganaji wake wapo huru kujiunga na jeshi la Urusi wakitaka. Kwahiyo, Tarimo alikuwa anapigana chini ya bendera ya Urusi na alikuwa mwanajeshi wao umauti ulipomkuta.
 

Ebu acheni upotoshaji hizo picha sio Joshua Mollel......ni edited
Angalia sura ilivyopachikwa na anaonekana kabisa ni mtu mwenye uso mpana na wakati kijana wa Kimasai alikuwa na uso wa kawaida tu

Mkono unaoonekana hapo ni wa mtu mweupe yaani Mzungu na wakati kijana alikuwa ni mweusi.....kwahiyo,Acheni ujinga,yani kijana wetu kauwawa na Waarabu halafu sisi tunashangilia na tunaungana na Waarabu ku-edit picha??

Je,kama angekuwa ndugu yako ungejisikiaje??
 
Wagner ni professional soldiers na wanapigana upande wa Urusi. Pia, wapiganaji wake wapo huru kujiunga na jeshi la Urusi wakitaka. Kwahiyo, Tarimo alikuwa anapigana chini ya bendera ya Urusi na alikuwa mwanajeshi wao umauti ulipomkuta.
Hakuna mahali nimesema alipigana upande wa Ukraine au Wagner ni mercenaries wa Ukraine.

Mercenaries ni wanajeshi kamili ila ni wa kukodi ndio Urusi alichofanya mtu ukimkodi lazima atakuwa upande wako na si vinginevyo.
 
Eti "Utadhani wanachambua mpira"

Sasa wewe na hao ambao huwa kama wanachambua mpira wana utofauti gani!!!

Haya tuseme aliingizwa Jeshini, mtu aliyeenda Israel mwezi wa 11... Wewe leo unaongea kwa kujiamini kabisa eti "Aliuwa Watu wengi..!"

Ulikuepo wakati anaua hao watu wengi...!!!

Yani Waswahili ni waswahili tu.
 
Mwanzoni nilijiuliza kwanini watu wameshindwa kufanya utambuzi rahisi wa kwanza kabisa.
 
Nafikiri sababu ni "War Propagandas" zinazofanywa na wafuasi wa kundi la kigaidi la Hamas ili kujaribu kuhalalisha uovu wao waliofanya huko Israel. Nothing more nothing less!

huo uovu mbona wameufanya kwa watu wa mataifa mengine pia ikiwemo Israel pia, kwanini iwe clip ya Mtanzania peke yake?
 
Israel haina shida ya wanajeshi,
Ina wanajeshi active 169,500 na wa akiba 465,000.
Kuku wewe. Vile vita wanaviogopa. Kama huamini piga simu waambie unataka uje kuwasaidia ktk vita uone kama hutoletewa ndege ya kukodi uwahi mstari wa mbele
 

Vigezo vya kujiunga na Aliyah (in Jewish) perspective ili uweze kwenda Israel au kujiunga na jeshi lao.

Sio rahisi kwa kila mtu hasa non-Jews; huko Israel kwenyewe raia wao ambao non-Jews (Christian) sio takwa la lazima kupata mafunzo ya kijeshi.

Halafu mtu awasili kwenye nchi hata miezi miwili ana na ndio anaenda Israel mara ya kwanza hayo mafunzo kayapata saa ngapi ya kuweza kupigana.
 
Kwa hilo Hamas wako sawa kabisa 100%
 
swali langu ni rahisi sana, waliouwawa kwenye mashambulizi ya Hamas ndani ya Israel ni wengi sana, kwanini hili la mtanzania ndio linaonekana kubwa na kusambaa mno?
Linasambaa kwasababu ni mtanzania mwenzetu hao wengine sio watanzania .kila mtu analia msiba wa ndugu yake.hata wewe ukifa Tutalia sisi siyo hamas sawa ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…