Mtanzania aliyeuawa na Hamas alikuwa sehemu ya jeshi la Israel? Serikali itoe tamko Watanzania wangapi wameingizwa kwenye jeshi la Israel

Ukisoma chuo cha kilimo sehemu fulani huwezi kupelekwa mahala pengine kujifunza kwa vitendo? Lakini nani alikwambia hao vijana walipelekwa chuoni, hasa hicho chuo unachokisema? Tanzania yenyewe tunayo SUA na vyuo vingine vidogo vidogo vya kilimo kama vile Ukirigulu, Ilonga nk, unataka kutuambia Israel inacho chuo kimoja tu cha kilimo?
 
Hapana sina maana hiyo ila Vyuo vipo vingi ila hicho ni International
Unajua sisi tunachangia na kubishana bila kujua ukweli
Ni hearsay tu
Kama mataifa yaliyoendelea kwa sasa ukweli wote ungewekwa wazi
Lakini sisi tunaishia kubishana kana kwamba tunajua kitu bali unoko tu nothing else
Kama wao hawataki kusema yote sisi ni kuchambua tu mengine ni mawazo tu
Tutabaki kusema Labda hivi labda vile
 
Ina make sense kimtindo, likely mtu anaenda kusoma Kilimo kweli ila akifika huko anaona fursa nyingine anajilipua jeshini.

Inawezekana hata serikali isihusike naye kwenye mafunzo ya kijeshi ila ni mamluki tu.

Yule aliyefia Urusi ni Tarimo hawa wa Gaza ni Mollel&Mtenga maybe ni coincidence tu au ndiyo hustlers wetu hawa.
 
Nimekwambia raia wa nchi moja akitaka kujiunga au kufanya kazi na jeshi la nchi nyingine lazima apate ruhusa ya nchi yake tofauti na hapo ni uhaini
Siyo kweli, it depends.
Raia wote wa South Africa waliojiunga na Jeshi (JWTZ ) hapa Tz kule kambi za Jeshi Mazimbu na Dakawa Morogoro hawakuwa na ruhusa kutoka kwa Serikali au Mamlaka za nchi ya Afrika ya Kusini, hawakuwa na ruhusa kabisa. Nalifahamu Jambo hili fika kabisa na Nina ushahidi/uthibitisho wa kutosha kuhusu hili. Niliwahi kuwa na urafiki wa karibu na baadhi ya Wanajeshi hao kule Mazimbu Morogoro miaka hiyo ya nyuma ya 1990s. Nilikuwa nawafahamu baadhi yao kwa undani kwani wengi walioa wa-Tz au kuwa na mahusiano na wanawake wa ki-Tz mitaani kule Morogoro, nilifahamu hili wakati huo nilipokuwa naishi huko. Mfano mzuri Mwanajeshi mmoja wa SA aliyeitwa Chris Hani mara kwa mara alikuwa akija Mtaani kwetu nilikokuwa naishi wakati huo. But, all in all, raia wote wale wa SA ambao walikuwa Wanajeshi kule Morogoro hawakuwa na Hati za Kusafiria za nchi ya Afrika ya Kusini wakati ule, wote walikuja bila Passports.
Kwa hiyo hoja yako siyo ya kweli kwamba kujiunga na Jeshi la nchi nyingine basi moja kwa moja ni Uhaini. Ni uongo, it depends.
Na wengi wa wanajeshi wale wa SA waliokuwa kule Mazimbu & Dakawa, sasa hivi baadhi yao ni Viongozi wa ngazi za Juu sana Serikakini kule nchini Afrika ya Kusini. Endapo kama wangekuwa wahaini, basi wasingeweza kuajiriwa ktk taasisi za Serikali huko SA leo hii.
Therefore, "No research no right to speak." (Mao Zedong).
 
Sawa kabisa, lakini mtu akiamua kukaidi na kwenda kujiunga na jeshi la nchi nyingine kinyemela, wakumlaumu ni Nani, mtu mwenyewe au serikali? Kuna vijana walijiunga na El Shabab lakini hatukuilaumu serikali, na bado juzijuzi kuna mwingine aliuawa akipigana upande wa majeshi ya Urusi uko Ukraine. Yawezekana wapo vijana wengi ktk majeshi ya nchi za kigeni lakini serikali haijuhi. Si busara kuipa serikali lawama kwa jambo tusilokuwa na uhakika nalo. Kutuletea clip za watu wenye asili ya Africa kwenye Kombat za majeshi ya Israel hakuwezi kututhibishia kuwa hao ni Watanzania.
 
Raia wengi wa Urusi hawataki kupigana katika vita vya Putin, na pia strategy kubwa ya Urusi katika vita vyake siku zote imekuwa kutumia wanajeshi kama Cannon fodder.
 
Huu Uzi utawapata watu wajinga wajinga mnaofanana akili ila kwa mtu mwerevu atakuona Umeandika upumbavu tu hapa.

-Unadai IDF inawachukua watanzania na kuwaingiza jeshini kusaidia Israel huo ni uongo umeambatanisha na ushahidi wako ila kwakuwa elimu ya madrasa imekujaa kwenye ubongo mpaka Ile common sense haipo tena umeshindwa kuona kwamba wanaokuwa trained Hapo sio Tanzanian Bali Tanzanian Soldiers yaani JWTZ na hiyo taarifa nimeifuatilia vizur ilichapishwa March 4 2019 8:13 am hao IDF walikuwa wanawa train JWTZ tena hapa hapa Tanzania na huo ni utaratibu wa kawaida wa IDF kwa ajili ya kudumisha mahusiano mazuri ya kidiplomasiana baadhi ya nchi za Africa na ukiacha Tanzania pia IDF wanafanya kwa Rwanda,Kenya,South Africa,Ethiopia,Cote D'Ivoire, Zambia, Malawi,Nigeria , Cameroon Ghana na Togo.
- Ukija kwenye hizo picha unazodai ni za Marehemu Mollel akiwa na gwanda za jeshi ni uongo mtupu maana zinaonekana kabisa ni Photoshop huitaji hata elimu ya darasa la 4 kugundua hilo sasa sijajui ni ujinga wako au umefanya makusudi kupotosha ila ndio nimekueleza utawapata wajinga wajinga kama wewe

- Unapozungumzia kifo Cha Mtanzania aliyeuwawa Ukraine na huyu aliyeuwawa Israel huoni kwamba ni vifo tofauti? Japo vyote vinatakiwa kukemewa,
Mmoja alienda Urusi kusoma akafanya makosa akafungwa gerezani baadae akaelezwa namna ya kupata msamaha akakubali kwenda vitani Ukraine akafia huko akiwa anapambana Frontline.

Huyu Mollel alikuwa ana week 3 Toka aende Israel na ni mara yake ya kwanza akiwa ameenda kujifunza kilimo na ufugaji Oct 7 akiwa anarud kwenye shughuli zake za kawaida anaendesha baiskeli yake akakutana na hao wapumbavu Hamas wakiwa wanakamata na kuua Kila raia waliyekuwa wanamshuku kuwa tofauti na wao, mnasema kakutwa kwenye Kambi ya jeshi nami niwaulize mfano hapo mlipo mmevamiwa na watu wenye silaha tena wanaua Kila wanayekutana naye alafu pembeni yenu Kuna Kambi ya jeshi je sehemu salama ya kukimbilia ni wapi? Huyo kijana kakamatwa akiwa Hana silaha yyte mbaya zaidi haelewi hata anachoulizwa wameishia kummimininia risasi kama vile muhalifu wakati yule wa Urusi lilipigwa kombora likamkuta yeye na askari wengine wa Wagner wakiwa Frontline akafariki bado tu unataka kufananisha hivi vifo viwili?

Israel haina shida na waafrica kujiunga na IDF juzi tu wameita reservist karibu lakin 3 hapo bado hujajumlisha na wale waliyo active jeshini sasa ukachukue waafrica wa nini?
Kingine Israel anajua kwamba kila Kona kazungukwa na maadui Leo hii waje wamchukue kijana ambaye hawamfahamu ndio kwanza ana week 3 Toka aingie Israel na ni mara yake ya kwanza!! Bro MOSSAD, SHIN BET sio sawa na TISS ya Uvccm.

Vifo vyote hivyo watu wenye ubinadamu, Imani na akili timamu tumevilaani ni wajinga tu ndio hamkuvilaani ukiwemo mtoa mada, pia kutolaani kuuliwa kwa kijana wa kitanzania huko Ukraine sio kigezo Cha kuhalalisha mauaji ya Mollel.
 
Nendeni tena si mumesema mnaenda Mashambani kulima?

Mliambiwa hizo ni geresha mnabisha.Haya Sasa yamewakuta.
 
Israel haina shida ya wanajeshi,
Ina wanajeshi active 169,500 na wa akiba 465,000.
Hujui mambo yalivyo huko Israel, na wala hakuna haja ya kutumia nguvu sana kukuelewesha. Siku hizi teknolojia imekuwa, ukweli utafahamika tu. Na kwa taarifa yako Mwili wa marehemu upo, umehifadhiwa na waisrael, bado hawajui wautowe vipi. Maelezo ya awali waliyoyatoa hayawaridhishi wenyewe, ndugu wa marehemu wala sisi watanzania, ndio maana wanasubiri moto upoe.

Heri Warusi walikuwa wazi toka awali kwa yule kijana aliyeuawa vitani, ndugu wakapata mwili na kuupumzisha kwa amani, yakauma lakini yakaisha. Ila kwa hawa Waisrael, mtasubiri sana.

Kitu ambacho hukijui ni kwamba, Muisrael mmoja akiuawa ni janga kubwa sana la kitaifa. Taifa nzima linatikisika, haijalishi wana wanajeshi milioni au zaidi. Hivyo mstari wa mbele au chambo mara nyingi wanakuwa vijana wa mataifa mengine. Kumbuka, Israel ni time bomb, security yake iko matatani sana kila siku.
 
Siwezi kuamini hizo picha siku hizi Kuna Artificial intelligence ni balaa. Unaweza kuwekwa sehemu ambayo hujawahi kuwepo
 
Kwani Tz watu hawauawi??
Tunapinga ni kwa sababu mauaji hayo siyo ya haki. Hata kama yangetokea Tz, lazima pia tungeyapinga.
"Injustice somewhere is the threat to Justice everywhere."
Martin Luther King Jr.
Sio ya Haki? Nani alimwambia akatumikishwe Jeshini Kwa mgongo wa Mafunzo ya Kilimo?
 
Hamas ni wapuuzi fulani hivi tena hawana akili kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…