Mtanzania aliyeuawa na Hamas alikuwa sehemu ya jeshi la Israel? Serikali itoe tamko Watanzania wangapi wameingizwa kwenye jeshi la Israel

Mtanzania aliyeuawa na Hamas alikuwa sehemu ya jeshi la Israel? Serikali itoe tamko Watanzania wangapi wameingizwa kwenye jeshi la Israel

Hamas ni wapuuzi fulani hivi tena hawana akili kabisa.
Nenda kalime kwenye mashamba ya Israel wakuoneshe moto si ndio mnadangangwa.

Ukweli ni kwamba wanapenda Israel kwenye kozi za shamba wapo ila humo humo wanapachika watu wanaoenda kujifunza mambo ya kijeshi akiwemo huyu dogo.
 
Hii kitu inafichwa fichwa sijuwi Kwa maslahi ya nani.Kwa sababu kwenye video wale Hama wanamuhoji kuwa we Sio Muyahudi Kwa nini umekuja kuuwa ndugu zetu??Hebu tueleze ukweli .Yule alipewa visa kuwa anaenda kusomea kilimo ila tamaa ya pesa ikamfanya akaingia jeshini na kauwa raia wengi sana huko Gaza.Ila mihemko ya wabongo utadhani wanachambua mpira hawataki kutafuta ukweli.
Ukiletewa ushahidi Kama hiyo visa ilikuwa geresha utakuwa tayari kurekebisha post yako ?
 
Kwani Tz watu hawauawi??
Tunapinga ni kwa sababu mauaji hayo siyo ya haki. Hata kama yangetokea Tz, lazima pia tungeyapinga.
"Injustice somewhere is the threat to Justice everywhere."
Martin Luther King Jr.
Kwani kinachopigiwa kelele ni mtanzania kuuliwa au mtanzania kuuliwa na HAMAS? Ni mtanzania kuuliwa na HAMAS hio ndo sababu

Ukitaka HAMAS wasikuue, baki au rudi Tanzania
 
We ndio umesema ukweli Sasa umetufumbua macho.
Hio boxer ya Mollel ya rangi ya jeshi la nchi Gani.
Na kwann avae nguo ya kijeshi hali si mwanajeshi uenda hio nguo ndio imemponza
 
Kumekua na hamaki na sitofahamu nyingi sana baada ya clip ya mauaji ya Mtanzania anaefahamika kama Molel kusambaa mitandaoni.

Katika clip husika,wauaji mwanzoni walionekana wakimhoji kwa gadhabu Mtanzania huyo na baadae aliuawa kikatili na sehemu yake ya nguo ya ndani (boxer) ilionekana ikiwa rangi ya kijeshi,well tufanye nguo tu.
View attachment 2847773

Gazeti moja wapo maarufu huko Israel limeripoti kua Watanzania ni miongoni mwa waafrika wanaoingizwa jeshini na kupewa mafunzo wakasaidie jeshi la Israel.
View attachment 2847770

Hali ya Waafrika kuingizwa kwenye jeshi la Israel nimeona hata South Africa ikionya raia wake na kua itawavua uraia kwani haiungi mkono matendo hayo.
View attachment 2847772

Watanzania wangapi wanakumbuka mwanzoni mwa vita ya Urusi na Ukraine kuliripotiwa Mtanzania mwanafunzi ameuawa na Ukraine kwenye mapigano?!!

Taarifa zilitoka kweli alikua Mtanzania na mwili uliletwa,je watu walihamaki kama hivi sasa?!! Hakua Mtanzania?!! Kwa nini sasa hivi watu wamehamaki sana?!!

Mtanzania alieuawa na wanajeshi wa Ukraine akiwa kwenye jeshi la Urusi alikua mkristo na mwenyeji wa Moshi pia kama huyu wa sasa wa Israel,,kwa nini watu hawakuahamaki?!! Ama kwa vile huyu ameuawa na HAMASI na alikua upande wa Israel?!
View attachment 2847884View attachment 2847793View attachment 2847794View attachment 2847795

Tazama vizuri picha zifuatazo,je ni yeye ama sio yeye?!! Je alieuliwa vitani Ukraine akiwa na Urusi na huyu wa sasa kuna tofauti gani?!! Kwa nini kwa sasa hamaki ni kubwa na chuki baina yetu Watanzania?! Alieuawa Urusi serikali ilisema kwa nini alikua na jeshi la Urusi baadala ya kusema tu mwanafunzi?!! Huyu wa sasa serikali imetoa taarifa zaidi kwa nini aliangukia maeneo ya mpakani na HAMASI hadi akatekwa?!! Hamaki na kulaani ni kwingi kwakua huyu Molel ameuawa na HAMAS ambao ni kikundi cha kiislamu huku Molel akiwa sehemu ya Israel (Taifa teule?) Ili hali mwanafunzi ambae aliuawa Ukraine akiwa na jeshi la Urusi watu hawakuahamaki kwa kua ilikua mauaji baina ya wakrsito kwa wakrsito?!!

Wizara ya mambo ya nje,imetoa tamko lolote la kuwataka Watanzia wanafunzi waliopo Israel kuondoka ama taarifa za kifo tu zinatosha?!!

Ikiwa Israel inalipa mamilioni ya hela kwa waafrika ili wakafanye kazi kwenye mashamba je haiwezi kulipa mamilioni ya hela watumikie jeshi?!!

NB- video ambayo anahojiwa baada ya kukamatwa ipo. Mtu anaweza kuitazama na kutafsiri mazungumzo yao kabla hajauawa,moja ya nukuu ya mtu alieiona.
View attachment 2847814
Wafia dini za Waarabu mnatafuta kila justification kuonyesha Mtanzania hakuwa Mwanafunzi: Nyie ni wapuuzi tu, Mnwakubali mababii wenye asili yapo jirani na palestina ila hamwakubali manabii wa nyumbani akina Mwamposa na wenzie.
 
We ndio umesema ukweli Sasa umetufumbua macho.
Hio boxer ya Mollel ya rangi ya jeshi la nchi Gani.
Na kwann avae nguo ya kijeshi hali si mwanajeshi uenda hio nguo ndio imemponza
Hizo nguo za jeshi ni wanajeshi wenu tu wasiojielewa ndio wanakataza kuvaa ila nchi nyingi hayo ni mavazi ya kawaida tu.
 
Nenda kalime kwenye mashamba ya Israel wakuoneshe moto si ndio mnadangangwa.

Ukweli ni kwamba wanapenda Israel kwenye kozi za shamba wapo ila humo humo wanapachika watu wanaoenda kujifunza mambo ya kijeshi akiwemo huyu dogo.
Nipo tayari kulima mashamba
 
Sheria ya matumizi ya mtandao Inatakiwa itumike hasa Kwa mleta mada. Anatakiwa athibitishe hizi tuhuma nzito kuwa serikali ya Tanzania imepeleka mamluki kujiunga na Jeshi la Israel. Ili iwe fundisho Kwa yeyote anayeleta habari za kuchafua na uchochezi.
 
itakuwa Hamas wana taarifa za kijana kwamba labda anatumiwa na wayahudi kwenye unyama wao dhidi ya wa palestina...watu wakienda nje wanjihusisha na mambo mengi sana ya hovyo,namjua dogo mmoja katoka huku 2014 akiwa fresh tu,yupo USA sasa hivi limekuwa shoga tena halijifichi
 
itakuwa Hamas wana taarifa za kijana kwamba labda anatumiwa na wayahudi kwenye unyama wao dhidi ya wa palestina...watu wakienda nje wanjihusisha na mambo mengi sana ya hovyo,namjua dogo mmoja katoka huku 2014 akiwa fresh tu,yupo USA sasa hivi limekuwa shoga tena halijifichi
Hata yule mtza aliyeuwawa Ukraine alikuwa sehemu ya jeshi la Urusi.
Wabongo wakiwa nje ufanya chochote
 
Ninachoona hapa ni mehemko tu ambayo imetokana na propaganda zilizochanganywa na itikadi za kidini.
 
Why unarudia maneno yale yale badala ya kuweka maoni yako ????
Jamaa Huwa anashangaza sana, halafu nimeona Kuna sehemu wanamsifia eti na yeye ni mmoja wapo wa wale wanaoitwa magreat thinkers wa humu...🤣🤣
 
Israel haina shida ya wanajeshi,
Ina wanajeshi active 169,500 na wa akiba 465,000.
Urusi ina shida ya jeshi? Mbona ilitumia Wagner kwenye frontlines? Same to USA ina shida ya jeshi? Ila ilitumia Blackwater na PMC zingine huko Iraq na Afghanistan.

Mercenaries wanatumika dunia nzima wakati wa vita hasa kwenye frontlines ili kuminimize vifo vya raia wa nchi husika.
 
Wabongo buana! Tunapenda kutunga nadharia mbali mbali hata kwa mambo yaliyo wazi. Mtoa post, unapata faida gani ya kufanya editing na kutunga vi maamdishi vya uongo hivyo? HAMAS is not synonymous to ISLAM, ndio maana hata nchi za Kiislam kama Saudia na Qatar hawawaingi mkono. Na Israel sio Ukristo. Chuki yako dhidi ya Dini ya Ukristo ambayo alikua anasali marehem Joshua isiwe sababu ya kutunga uongo. Vijana walienda kusoma na sio kujiunga na Jeshi. Wale waliosoma SUA wanaelewa utaratibu huu wa wanafunzi kwenda kufanya internship Israel na kujifunza Zaidi kilimo cha Kisasa.
 
Mtanzania akitekwa au kuuwawa nchi ya ugenini jukumu la kuhakikishiwa usalama wake liko chini ya nani?
 
Back
Top Bottom