View attachment 559506 View attachment 559506
Huyu Kirui ni kama anatumia diesel,mapafu gani ya binadamu muda unavyozidi kwenda ndio anaongeza mwendo?
Ila Simbu kamkosa kosa sana yule Muethiopia nafasi ya pili,ni kama point 49 kwa 51.Si haba...Hela atakayopata inatosha sana sana kwa kuanzia maisha,maana jamaa alikuwa anakaa chumba kimoja tu na sebule kule Arusha.
Wakati ule majirani pale Arusha hawakujua kama ameenda Rio de Jeneiro kwenye Olympic,walishangaa kumuona na kumfananisha kwenye TV wakati anakaimbia.Mkewe akiwa nyumbani hana hata Tv kujua nini mume wake anafanya huko Brazil.
Mungu amtie nguvu,amzidishie na siku moja ampe medali ya ushindi ya dhahabu kwa moyo wake wa kujituma.Anatoka Singida vijijini sana,katikati ya jamii masikini.Kwa kipaji chake,Mungu atamjalia.
Kama namuona jamaa yangu Gidabudayi,mzee wa Shirikisho la Riadha Tanzania