Mtanzania, Alphonce Simbu ashika nafasi ya tatu Marathon IAAF LONDON

Mtanzania, Alphonce Simbu ashika nafasi ya tatu Marathon IAAF LONDON

Asante sana
Mimi nakumbushia tu kabla ya kwenda Rio jinsi alivyokuwa akiishi.
Mtindo wa maisha ulibadilika baada ya kutoka Rio,ila kabla ya Rio huo ndio ulikuwa mtindo wake wa maisha.
Mungu amsaidie siku moja awe namba moja.!
 
Huyu jamaa namkubali toka muda ni vile tu serikali inawakumbatia wajingawajinga inaacha watu kama hawa mpaka tuwapigie kelele
 
Kweli angekaza angechukua silver.. Ila yule mu Ethiopia aliyeshika ya kwanza ni nyoko kawaacha mbali sana

Had wazungu wanashika shika miguu yake labda wanajua plstik

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
Wa kwanza Mkenya...Goeff Kirui.
 
View attachment 559506 View attachment 559506
Huyu Kirui ni kama anatumia diesel,mapafu gani ya binadamu muda unavyozidi kwenda ndio anaongeza mwendo?

Ila Simbu kamkosa kosa sana yule Muethiopia nafasi ya pili,ni kama point 49 kwa 51.Si haba...Hela atakayopata inatosha sana sana kwa kuanzia maisha,maana jamaa alikuwa anakaa chumba kimoja tu na sebule kule Arusha.

Wakati ule majirani pale Arusha hawakujua kama ameenda Rio de Jeneiro kwenye Olympic,walishangaa kumuona na kumfananisha kwenye TV wakati anakaimbia.Mkewe akiwa nyumbani hana hata Tv kujua nini mume wake anafanya huko Brazil.

Mungu amtie nguvu,amzidishie na siku moja ampe medali ya ushindi ya dhahabu kwa moyo wake wa kujituma.Anatoka Singida vijijini sana,katikati ya jamii masikini.Kwa kipaji chake,Mungu atamjalia.

Kama namuona jamaa yangu Gidabudayi,mzee wa Shirikisho la Riadha Tanzania
Gidabudayi alishasema siku nyingi tatizo la riadha TZ,ameingia tumenza kuona wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6a556eae78c3600bf653587ac8d0a970.jpg

Uhuru ameshampongeza mtu wake, sina uhakika hata kama mheshimiwa anajua kuwa leo simbu amekimbia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hawa wakenya huwa wanakula mizizi gani? isitoshe wanatumia mitishamba ya kuzunguka mount kilimanjaro afu sisi wa Tz tuna zubaa tu wakati sisi ndio wenye mlima.

Hongera kwa Mtanzania mwenzetu, nafasi ya3 si haba. Special bigUp kwa team nzima iliyofanikisha jamaa kushinda nafasi ya3
 
Nashukuru sana ,shirikisho la riadhaa la dunia lilianza kuwapima mkojo Jirani zetu, kumbe siku za nyuma walikuwa wanatumia dawa za kuongeza nguvu.
Ndugu Simbu hongera sana, nakushauri sasa utusaidia kuwapata vijana wengine ili tuwaandae kwa ajili ya siku zijazo!!,
Tena ikiwezekana Serikali ikubali kuwa kuna mikoa ina vipaji(Manyara, Singida, Arusha).twende tukaanzishe shule za riadha,baada ya miaka michache tutakuwa sawa na Ethiopia na Kenya.
 
Back
Top Bottom