Mtanzania, Alphonce Simbu ashika nafasi ya tatu Marathon IAAF LONDON

Mtanzania, Alphonce Simbu ashika nafasi ya tatu Marathon IAAF LONDON

Sasa hivi amejifungulia milango. World Championship Bronze Medallist sio mtu mdogo, ameingia kwenye historia ya riadha duniani.

Hata Usain Bolt mwaka huu kaishia bronze medal!

Kabisa Mkuu na nimefarijika jinsi unavyobainisha kwa msisitizo kuwa mbio hizi ni za Ubingwa wa Dunia za Shirikisho la Riadha Duniani yaani IAAF World Championship 2017 zilizokusanya wakimbiaji bora wa masafa mbalimbali ikiwemo hii ya marathon. Hivyo siyo mchezo mchezo mashindano ya Ubingwa wa dunia.
 
alphonce-simbu-from-tanzania-wins-the-standard-chartered-mumbai-2017-picture-id631719960


Mtanzania Alphonce Simbu muda huu kwenye mashindano ya dunia ya riadha ya marathon amefanikiwa kumaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba.

Ikumbukwe kuwa Simbu katika mashindano ya Olympics 2016 alifanikiwa kumaliza wa tano

Mwezi wa kwanza 2017 katika mashindano ya Mumbai Marathon Simbu aliibuka mshindi kwa kumaliza wa kwanza

Katika mashindano hayo ya dunia Mkenya Kirui alishinda kwa kumaliza wa kwanza

Hongera sana Simbu kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania vizuri
VIVA SIMBU

VIVA TANZANIA
 
Jamaa ametimua mbio yaani nimefurahi sana kuona mtanzania kajaribu namna hii....Simbu amemweza Kipketer wa Kenya ambaye amemaliza ktk nafasi ya nne...Tanzania is now in the medal table...infact most EA nations except Somalia, Burundi and Rwanda are on the medal table...congrats to the man Simbu!!! a true hero
CqZSHCWWAAAdGTO.jpg
Shukran mkuu,
 
Wakenya,Ethiopia,Tanzania ladies wapo kwenye kundi moja....
 
Kwa miaka ijayo jamaa atafanya vizuri zaidi ya leo... last year alikuwa wa 5 sasa hivi kawa wa 3 .tutarajie makubwa kutoka kwake. Hongera saana.
 
Hizi mbio si mchezo, simbu anahitaji mapokezi ya heshima na kuandaliwa mazingira ya kushindana mbeleni


Mwakyembe haujafika Airport tu?
Mwakyembe bado yupo msibani, wanyakyusa msiba kwa mtu mzima ni mwezi, ukoo wa kichifu miezi sita. Wanyakyusa wanajua kulia we acha bhana!!
 
Back
Top Bottom