Ipo haja kwa Watanzania kabla awajaenda USA wapewe seminar nini cha kufanya pindi wakisimamishwa na police USA wafanye nini, maana act yeyeto kwa mafunzo ya police wa USA unakula bullets. Maana hata wao wanauliwa Sana na wahalifu wakishangaa, so action yeyeto utakayofanya wanaamini unataka kuchomoa gani. Salama ya police USA ni kutii au lala chini, au wageuzie mgongo huku umenyoosha mikono juu ukiwa umetulia.
Pana Mtanzania aliuliwa by mistake sababu ya kutojua codes za police wa USA.
Alisimamishwa na police bahati mbaya simu yake ikaita mfukoni kitendo tu cha kuingiza mkono mfukoni Ili achukue simu apokee, ndo ikawa mwisho wa uhai wake pale alipigwa risasi, police waliamini anataka kutoa bastola awashuti, ni vitu vya kuangalia Sana USA hivi. Ukiwa unaendesha ukasimamishwa na police park pembeni tulia kwenye gari usitoke shikilia usukani au toa mikono yote miwili nje hadi waje.
Kwa any act wape ushirikiano usijibizane nao wala kujifanya mjuaji,wakikuona umewapa ushirikiano hawa shida na wewe.
Hakuna police atokae alipotoka aje tu ampige mtu risasi.