DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu umeongea kwa uchungu. lkn bongo hamnaga watu kuna sanamu tupu. Yani namaanisha kuna mifano ya watu hawana maarifa wala roho za kistaarabu
Yaani mtu hatoi pesa mfukoni ni swala la kumfatilia na kumrudisha Tanzania ndugu watapatikana tu ila sasa kwa roho za hao jamaa nao ndio kwanza wanasoma hizi taarifa kama wapo China...
 
Watanzania wanapikuwa nje ya nchi ni ndugu tofauti na makabila mengine kama wasauz, ukimkuta ndugu yako kavua nguo anakataa kuvaa huwezi mwacha utatafuta watu wakusaidie kumsitiri ndo alichofanya ndugu yetu, we msaidie hata kwa mawazo tu.
 
Balozi za kwetu ni za kipumbavu sana. Hazina msaada hata chembe kwa watanzania wenzao wenye shida. Mtu katoa taarifa na ameelekezwa jimbo alipo. Wanashindwa kutrack hadi wampate na kumrjesha nyumbani. Hawa watu ni qumer sijawahi kuona.
Mambo kama haya ndio ya kuandamana mpaka Bunge liongee
 
Yeye huyo aliyekaa nae hapo bustanini Texas kwann asimuhifadhi. Huku akisubiri msaada zaidi kwa ndugu husika? Au hujui nn namaanisha?
Siyo kama amekosa sehemu ya kukaa. Ni kichaa. Nadhani unajua changamoto za watu wenye ugonjwa wa akili. Wengi wanakimbia nyumbani. BTW kuishi na mtu mwenye ugonjwa wa akili kunahitaji uangalizi wa 24/7. Nani atafanya hiyo kazi wakati majuu unatoka asubuhi na kurudi jioni? Ukikuta amechoma nyumba moto? Au amejinyonga?
 
Wewe ni mpumbavu sana. Ndiyo maana utaozea hapo Bongo kwa sababu mawazo yako ni kijinga. Unaonea wivu mpaka vichaa kwa sababu tu alisafari nje ya nchi? Unataka kila mtu akae Tanzania una kazi za kuwapa? Idiot!
 
Kuna jinga moja linaitwa GENTAMYCINE linachekelea eti ni kwa nini alienda nje ya nchi. Hebu fikiri jitu kama hili likipewa madaraka litakuwaje!
 
Ficha upumbavu wako. Narudia: ficha upumbavu wako.
 
Kuna jamaa kipindi fulani huko majuu alichanganyikiwa hivyo hivyo kwa stress tu, akaonekana chizi watu tujiunge tumsaidie kumrudisha home. Huyu jamaa alikuwa 'kajilipua'/. Ebanee akaenda kusema kwa mamlaka kuna watu wanataka wamrudishe nyumbani kwa nguvu akauawe! Kuna watu walihama nyumba. Haya mambo sio rahisi kihivyo huko nje, kumrudisha mtu bila ridhaa yake sio kazi rahisi na ukisema ana matatizo ya akili kwa mujibu wa nani?
 
Huyo amesema hana Pa kuishi, na anaishi darajani au msituni.
Sasa wee hapo Pa kukaa aliponapo na unapajua ni wapiii?
 
Ubalozi au ndugu zake wanaweza kusikilizwa kuliko mtu baki tu. Ila kuna watu wanamshambulia mlete ''alert'' eti alitakiwa amchue aishi naye. Watu wanadhani mambo yanaenda kienyeji tu. Nakumbuka huko huko USA mama mmoja na mumewe walikuta na homeless mmoja wakaamua kumchukuwa na kumpa chumba cha kuishi kwenye makazi yao. Yaani alikuwa anapata kila kitu free kama mtoto wao. Pamoja na ukarimu wote akawavizia siku moja na kuwaua wote.
 
Hii stori inawea kuwa ni ya kutunga, si halisi
Vinginevyo kana ni ya kweli, utakuwa unafanya makosa makubwa sana
Watu wa aina hii wapo wengi tu Marekani na si lazima wawe wametoka Tanzania. Wewe uanchotakiwa kufanya ni kupata details za familia yao huku Tanzania, ili Ubalozi watakapoingia kazini, wawe na uhakika kuwa mtu huyu kweli ni Mtanzania
Naamini Ubalozi wanayo pia register ya wanafunzi watanzania wanaosoma huko, na possibly kati ya walio kwenye orodha yao, huyo siyo mmoja wao

Wewe unatakiwa uwa-provie ubalozi kuwa huyu mtu kweli ni Mtanzania, halafu baada ya hapo ndiyo uweze kuwalaumu
Wewe kwa details zote ulizozitoa hapa, unashindwa nini kupata taarifa za kule alikotoka? Wenzake aliokuwa anasoma nao, je?
Isisje ikawa ulitamani tu kuweka picha za watu wakiwa nusu uchi humu kwa visingizio
Taarifa yako hii inaweza kuwa ni crap, inaweza ikawa ni ya kutunga
 
Kama makada wa ccm wanaokotwa huko na kupewa ubalozi unategemea nini
Mtu kama polepole ana mastress yake yote unampa Ubalozi unategemea atasaidia kwetu

Sababu kapewa ubalozi kama adhabu nchi hii ina safari ndefu sana
Kuna balozi alitumwa nchi flani alipofika airport hajui hadhi yake akafuatana na wasafiri wa kawaida
Anaulizwa passport anatoa ya diplomatic
Akaambiwa ilibidi uende VIP lounge yaani hata kutoka tu hawajui itakuwa kazi zao

Wengine utafikiri walikuwa wanaishi na kuku tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…