DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Waafrika tunapigana vita nyingi sana, mtu uhangaike kusoma, kutafuta pesa, huku wengine wanakuroga na ukifa pia hakuna kupumzika unageuzwa mzimu aise, mungu amsimamie maskini binti wa watu
Dah mkuu we acha tu yani ni balaa umeongea ukweli mtupu
 
Ni mwaka wa saba (7) sasa tangu hili tangazo lilipo tolewa kwa mara ya kwanza.
Anyways, tuombe ndugu zake wapatikane mkuu, maana huko US hata rafiki hawezi akawa radhi kumuhifadhi mtu alie na shida ya akili.
Kumbe ni muda mrefu sana. Aiseeeeee. Dkt. Gwajima D tunaomba mumsaidie dada yetu anayedharirika huko USA. Najua mama yetu unaweza fanya jambo au ukawa ni sehemu ya kuanzia kumsaidia binti yako ndio maana tumekuomba. Tunaomba uanze na kitu kwani tunajua wewe ndio Waziri unayefikika kwa urahisi pia una respond nzuri. Fanya kitu kwa Dada yetu na Mungu atakulipa.
 
Comment kama hii ndio inaonyesha maana halisi ya utanzania.
 
Kuna binamu yangu naye ni binti alipiga six fresh kwa ufaulu mzuri pale msalato girls miaka ya 97, akakacha kwenda chuo, akaenda Marekani, alikaa huko zaidi ya miaka 10 hakuna mafanikio yoyote ukizingatia wenzake waliamua kupambana hapa Bongo wengi wapo kwenye position na maisha mazuri , so ndugu zake wameamua kumrudisha Bongo baada ya kupata Sonoma na kurun mental health, siku hizi anafungiwa tu ndani maskini, ukimuona na urembo wake utasikitika sana.
 
Sasa hapo kuna issue nyingi, miaka 10 Marekani huna makaratasi ni uzembe.

Halafu usikute aliingia kwenye drug abuse.

Ujuwe yule Whitney Houston alikuwa demu smart sana lakini alipokutana na Bob Brown ndio alimfundisha kubwia unga hadi kifo chake.
 
Ninachofahamu mimi Marekani hata uwe huna hata mia utatibiwa kwanza mambo mengine baadaye.

Huyu aliyeleta hizi taarifa ameshindwa vipi kukutana na Watanzania wachache kumsaidia huyu dada kupelekwa kwenye matibabu?
Akaita tu police akapelekwa kwa nguvu
Nashangaaa na huko texas watz ni wengi sana
 
Hatuwezi kusaidia MTU aliyepo US, wakati kuna wenye shida kibao zaidi ya hiyo huku nyumbani,Mbwa anahudumiwa vzr UK/US kuliko Bongo,
Trust me, huko US yupo salama zaidi kuliko akirudishwa bongo katika Hari hiyo
 
Acha ujinga Kaka.

We mchawi nini? 🤣🙈
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…