Mtanzania mwingine apigwa risasi Afrika Kusini

Hili ni janga la taifa. Watanzania wengi ni wavivu sana ndomaana fursa zilizopo nchini na nje ya nchi hatuzichangamkii.

Kuna clip fulan niliifuatilia miezi miwili iliyopita huko Dodoma nikaona mkuu wa polisi fulan amewakusanya wazazi wa wilaya fulan anawaeleza namna ya kuwadhibiti watoto wao ili wasiendelee au kujiingiza kwenye makundi ya kihalifu.

Kamanda huyo kuna sehemu amesema kwamba amekuwa akiwaona vijana kutoka Burundi na Rwanda wakifanya kazi kwenye mashamba na viwanda kibao vilivyopo Dodoma, huku wazawa wakiishia kushinda vijiweni wakipiga zogo na kuomba watu mia tano mia tano za kula.
Anakwambia hata wale wazawa waliokuwa wameajiriwa wengi wao wakishapata mishahara hutoweka kazini na kuonekana baada ya week mbili au tatu baada ya mshahara wao kuisha 🤣🤣🤣
 
Ni msiba mkubwa ulioje kwenda safari ndefu nchi za watu bila ya kuwa na LENGO na MIKAKATI ya kufikia lengo.
Vijana wengi wa kitanzania wameuwa ndoto zao kwa kuendekeza, viuno, pombe, bangi na mihadarati mingine.

Nchi hii ina raia wa nchi zote za Afrika. Lkn watanzania ndio wanaoongoza kwa uteja.
Ukifuatilia swala la mateja wa kigeni wanaoishi nchi hii basi 80% ni watanzania.
 
Cha kujiuliza ni hicho na wakati anasema hivo yupo kwa shangazi yake amekaa kwenye kochi anatype, kufika SA hata kwa mchongo inataka uwe na pesa nzuri tu plus accepted VISA....HIVI HIVI HUWEZI. Mwisho ujue unafikia wapi na kufanya nini.
 
Yaani nikwa Durban, nilikuwa nasikitika sana kuona vijana wa bongo, wengi hawataki kufanya shughuli zozote halali,kama walivyo jamaa toka Zim,Malawi au Mozambique...wengi wanaotaka shortcut deals tu kama vile bongo..na wengi jioni wanakwenda lala chini ya ' flyovers bridge za mabarabara...... kaazi kweli kweli.....
 
Kweli ila tushukuru mungu bongo amani ipo, si kwamba ujambazi haupo la , ila si kwa kiwango ama umbali wa crime syndcates za wenzetu, hitmens opertion ni zoezi kama lile la kumpoteza lisu pale dom , kwa maelezo ya lisu unaona kulikuwa na chain ndefu sana ya watu, utakuwa umedhulumiwa kiasi gani hadi uweze kufinance zoezi kama lile?
South africa hitman anakupoteza kwa deni la laki tu , sio rands!!! , madafu
 
Mkuu unaelezea kiuoga uoga , nimekaa hilbrow na berea gauteng south takriban miaka 7 , 8 najiua crime ya huko,,
maeneo niliyokytajia miaka ya 2000 ilikuwa ni kuokota maiti katibu kila siku sababu ya bunduki ,
hitmen kuja kuuwa bongo ni story tu , haiwezekani , Kama ilitokea ni miaka hiyo na mara chache sana , south africa kwanza wauza madawa wa kibongo hawana pesa ndefu ni kama madalali ,wenye hizo deals ni wapopo (nigerians) ukisikia mbongo kauwawa huko chances ni kuwa kazingua kwa mpopo, mpopo akitoa 500 rand kwa hitman mzimbabwe huna chako duniani.
 
Kilichomtokea baba yako mdogo ndio typical story ya wabongo wakiwa south africa!!
Tukubali tu bado tuna ushamba wa maisha !! Ndo sababu south africa tunapotezwa sana .
Enzi za waganga kupiga pesa south ziliambatana ma enzi za "wazee wa chaka" hawa walikuwa ni wezi wa international calls kutoka Tellekom, jamaa walikuwa wana pesa za hatari , wengi waliingia kwenye starehe na vyupi pesa ikapotea na tellekom wakaziba mianya ya uhalifu ule , wengi niliowajua ni marehemu kwa sasa..
 
Uvivu bongo umesababiswa na kufata sera za ujamaa,
Watu wanaona hata wasipofanya kazi watakula tu , ukijitima unapewa majina kama mtu wa dili , mchawi n.k ukienda mikoa ya pwani, kwenye mikorosho miembe na minazi hali ni mbaya zaidi, vijana hataki kabisa kufanya kazi, yet wanataka maisha mazuri , shida inaanzia hapo.
Kijana anayejituma bongo anaonekana nuksi kwenye kundi la vijana wenzake.
 
Wasukuma wakatazwe kuchangia madame ona huyu sasa
 
Ni aibu sana, imagine hata wamalawi wanatushinda namna ya kuendesha maisha nchi hii.

Ukienda kwenye deal la mashamba ya wazungu utawakuta wamalawi, ukienda kwenye garden boy ni wamalawi na wana make money kinoma, deal la kuuza laini za sim ambazo zina data au bando limehodhiwa na wamalawi huku wabongo wakiishia kuvizia wanaoweka sim vibaya ndan ya begi wapige ndole.

Sasa hivi wamalawi wamejaa sana katika kazi ya delivery kwa kutumia gari au piki piki. Hiyo kazi ina pesa ndefu maana kwa mwezi mtu wa piki piki peke yake hakosi R12,000 hadi 15,000 ambayo thaman yake ni karibia milioni 2 za bongo. Mbongo anataka auze bangi au unga mwisho wa siku ajikute anabwia mwenyewe na kuwa teja la kutupa.
 
Yah ni kumshukuru Mungu kwa kutuweka na crimes kubwa kubwa kama hizi za nchi zingine.
 
Swadakta kabisa. Umenikumbusha enzi za call za mchongo. Kweli wale jamaa waliokuwa wanapigisha sim asilimia 98% ni choka mbaya na wengi wao ni mateja wa kutupa.
 
Kweli mkuu, pamoja na kwamba vijana wengi wanalalamikia serikali kuwa kazi hakuna. Lakini ukweli ni kwamba hata hizo kazi zingekuwepo wasingefanya.

Huko pwani unakuta vijana wanashinda kwenye drafti, bao nk huku wakisubiri nazi zikomae wakaokote au kutungua wauze maisha yaende. Swala la kujituma ili kutengeneza maisha yao haliwahusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…