Mtaturu: Gharama za ATCL ndani ya Tanzania ni kubwa kuliko zile za Dubai

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2020
Posts
1,588
Reaction score
956

Mbunge Miraji Mataturu alia na bei za ATCL

MTATURU PIC
===
Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu ameitaka Serikali kutafuta suluhisho la bei kubwa ya usafiri katika ndege za Shirika la Ndege Nchini (ATCL) ambapo amezifananisha gharama hizo na gharama za kwenda Dubai.

Mtaturu ameyasema hayo jana Jumanne Februari 15, 2022 wakati akichangia taarifa ya shughuli za Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Amesema Shirika la ATCL limekuwa likifanya vizuri baada ya Serikali kulinunua ndege lakini limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Amesema bei ya tiketi ya ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma inafikia Sh400,000 hadi Sh700,000, gharama ambayo ukiangalia ni kama abiria anakwenda Dubai.

“Tumekuwa na changamoto kubwa kwa maana ya bei za tiketi. Ukiangalia tiketi ya kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma ni Sh400,000 hadi Sh700,000 ukiangalia wengine ni kama umeenda Dubai kumbe uko Tanzania hapa kumekuwa na changamoto lakini hakuna majibu,”amesema.

Mtaturu ameiomba Serikali kuangalia changamoto hiyo ya bei ya usafiri wa ndege.

Aidha, kumekuwa na malalamiko makubwa katika masuala ya mabando na kwamba mara nyingi wamewaeleza Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) waweze kuwasimamia watoa huduma kuhusu changamoto hiyo lakini haijafanyiwa kazi.

“Leo unaweka bado la wiki moja ikiisha fedha zinaondoka wakati ulilipia mwenyewe. Wananchi wanalalamika, tunaiomba Serikali iwasaidie wananchi waweze kuwa na haki yao ya msingi katika wanapoweka bando,”amesema.

Amesema licha ya kuwasilisha changamoto hiyo TCRA limekuwa ni tatizo isiyokuwa na majibu hata wanapoulizwa watu wahuduma kwa wateja wamekuwa hawana majibu ya moja kwa moja.

Ameiomba Serikali kulifanyia kazi ili kuwapa haki wateja.
 
Usafiri wanga yaani, kwanza ni gharama kubwa lakini sasa poor services.

Tunasafiri tu kwa sababu hatuna namna lakini luna baadhi ua mabasi yana services nzuri na za uhakika kuzidi wao.

Kuhusu mabando, inaonekana kuna watu wako serikalini wanafaidika nayo.
 
Si ana mshahara mzuri huyo? analia lia nini sasa. Sisi wanyonge tunaziona angani tu.
 
Pale ATCL kitengo cha masoko kuna dada kajaza umbo tu akili ya kulisaidia shirika hakuna. Sijui wanawapaje kazi hawa. ATCL wajiangalie mbeleko inaanza kuchanika.
 
Hao wabunge wangeomba mchanganuo wa gharama za uendeshaji ili waishauri vizuri Serikali sio tu kupiga porojo bila kujua kuan nini humo ndani ya bei za ndege. Afrika yote ndege ni ghali sana kutokana na gharama kubwa za uendeshaji maana bima ziko juu, hakuna viwanda vya spare na mrundikano wa kodi za serikali.

Wabunge waache unafiki wajiongeze watueleze ni sababu gani ATCL wanakuwa na nauli za juu na pia watupe mlinganisho na Precision maana nauli ziko mtandaoni. ATCL fanyeni biashara acheni siasa za majukwaani. Seriakli ikitaka isiwatoze kodi na tozo nyingine lukuki zilizopo.
 
Wachukue CEO kutoka Ryan Air, Fastjet wawaulize mode of business waliyokuwa wanatumia.

Ndege inatakiwa ijae kwa bei zao ni ngumu kujaza, ila wangeweka Cap ya 100K kwa route kama ya Dar Dom kwa siku wangeweza piga route zaidi ya 10

Mwanza ikiwa 250K go return watajaza mno na kwa siku wanaweza beba pax zaidi ya 2000
 
Operating costs ni kiasi gani? Kwa nini Precision wasingefanya hivyo miaka yote hiyo au wao hawataki kujaza? ATCL waendelee na biashara waachane na hizi siasa za populism. Ndege gharama
 
“Leo unaweka bado la wiki moja ikiisha fedha zinaondoka wakati ulilipia mwenyewe. Wananchi wanalalamika, tunaiomba Serikali iwasaidie wananchi waweze kuwa na haki yao ya msingi katika wanapoweka bando,”amesema.
Kuna wizi wa hovyo kabisa

Unagonga *147*00#
Mteja anaweka muda wa maongezi wa shilingi 10,000, anajiunga na kifurushi cha kupiga kwa siku kadhaa kwa shilingi 3,000, lakini muda ule ukiisha kampuni inalamba salio ambalo mteja hakuliunga kwenye kupiga wala hakutaka litumike bila ridhaa yake, sasa maana ya kugonga *147*00# iko wapi?
 
Mmekuwa mkitetea nchi kuwa na ndege zake badala ya kuruhusu usafiri wa ndege ushamiri kwa ushindani kwa kuruhusu mashirika/kampuni mbalimbali ziingie katika biashara ya ndege nchini (usafiri wa ndege za ndani). Matokeo ndiyo hayo, ATCL kupanga nauli kubwa wakijua kuwa watu hawana uchaguzi(choice), anayetaka kusafiri kwa ndege atakwenda na ATCL tu pasipo kuchagua kampuni nyingine kama ingekuwepo ambayo ingekuwa na nauli nafuu.

Hoja hapo ni kusema serikali iruhusu ushindani wa usafiri wa ndege wa domestic ili mlaji (mtanzania) afaidi ushindani katika biashara hiyo kwa maana ya huduma bora na nafuu.
 
Kuna wizi wa hovyo kabisa

Unagonga *147*00#
Mteja anaweka muda wa maongezi wa shilingi 10,000, anajiunga na kifurushi cha kupiga kwa siku kadhaa kwa shilingi 3,000, lakini muda ule ukiisha kampuni inalamba salio ambalo mteja hakuliunga kwenye kupiga wala hakutaka litumike bila ridhaa yake, sasa maana ya kugonga *147*00# iko wapi?
Hoja ya Msingi kabisa,
 
Mbunge Miraji Mataturu alia na bei za ATCL​

MTATURU PIC

===
Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu ameitaka Serikali kutafuta suluhisho la bei kubwa ya usafiri katika ndege za Shirika la Ndege Nchini (ATCL) ambapo amezifananisha gharama hizo na gharama za kwenda Dubai.

Mtaturu ameyasema hayo jana Jumanne Februari 15, 2022 wakati akichangia taarifa ya shughuli za Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Amesema Shirika la ATCL limekuwa likifanya vizuri baada ya Serikali kulinunua ndege lakini limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Amesema bei ya tiketi ya ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma inafikia Sh400,000 hadi Sh700,000, gharama ambayo ukiangalia ni kama abiria anakwenda Dubai.

“Tumekuwa na changamoto kubwa kwa maana ya bei za tiketi. Ukiangalia tiketi ya kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma ni Sh400,000 hadi Sh700,000 ukiangalia wengine ni kama umeenda Dubai kumbe uko Tanzania hapa kumekuwa na changamoto lakini hakuna majibu,”amesema.

Mtaturu ameiomba Serikali kuangalia changamoto hiyo ya bei ya usafiri wa ndege.

Aidha, kumekuwa na malalamiko makubwa katika masuala ya mabando na kwamba mara nyingi wamewaeleza Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) waweze kuwasimamia watoa huduma kuhusu changamoto hiyo lakini haijafanyiwa kazi.

“Leo unaweka bado la wiki moja ikiisha fedha zinaondoka wakati ulilipia mwenyewe. Wananchi wanalalamika, tunaiomba Serikali iwasaidie wananchi waweze kuwa na haki yao ya msingi katika wanapoweka bando,”amesema.

Amesema licha ya kuwasilisha changamoto hiyo TCRA limekuwa ni tatizo isiyokuwa na majibu hata wanapoulizwa watu wahuduma kwa wateja wamekuwa hawana majibu ya moja kwa moja.

Ameiomba Serikali kulifanyia kazi ili kuwapa haki wateja.
Bila kuwa na upinzani imara hakuna serikali ya maana
 
Back
Top Bottom