Mtaturu: Gharama za ATCL ndani ya Tanzania ni kubwa kuliko zile za Dubai

ATCL, kama yalivyo mashirika mengine ya Serikali, hakuna watu wenye uwezo wa kuendesha shirika kibiashara.

Sijui kodi, vipuli ni sababu zisizo na msingi. Fastjet walipokuwa wanatoa ticket kwa sh 80,000toka Mwanza to Dar, walikuwa wanatengeneza vipuli nchini?

Hakuja biashara ambayo Serikali ya Tanzania imewahi kufanya kwa ufanisi.
 
Uko sahihi kabisa ndugu yangu. Yaani mimi hapa nilipo muda huu natamani angalau hata kwa muujiza fulani, hivi ningekuwa mmojawapo wa washauri wakuu kabla ndege hizi hazijanunuliwa. Unajua hili tatizo la kuwa tunahujumu mtu binafsi kwa kudhani kuwa tunamhujumu yeye wakati tunawahujumu wa-Tanzania!
 
Emirates ilianza na ndege mbili za mtumba walizonunua kutoka ‘Air India’ mwaka 1985.

Mtawala wa Dubai alikuwa ana idea na business plan ya kuitangaza na kuikuza Dubai kupitia shirika la ndege (jamaa ni business man mzuri sana duniani); the rest is history.

Sisi tunalilia ndege Kwanza kwa sababu Rwanda na Kenya wanazo; kabla ya kuwa na business plan na mkurugenzi mwenyewe alikuwa air traffic controller Ghana. Hana experience ya kufanya kazi kwenye shirika la ndege wala hana background ya business studies.

With that info unapata ideas the chances ya ilo shirika kuendeshwa kwa ufasaha ni ndogo sana; litabaki kuwa kupe siku zote linalotegemea ruzuku.
 
Effects of monopoly
 
Siyo yeye anayefanya ni serikali wakati wa Lissu serikali ilikuwa haipeleki maendeleo ili kummaliza kisiasa Lissu
Huyu jamaa ni mzalendo zaidi kuliko Lissu,

Tangu amechukua lile jimbo limepiga hatua kubwa sana kimaendeleo,

Mtaturu Chapa kazi,
 
Mkuu ebu visit hapa kisha wasaidie wabunge na ATCL kuhusu hiyo nauli unayosema: Cheap flights to Zimbabwe, South Africa and Botswana
 
Huyu jamaa ni mzalendo zaidi kuliko Lissu,

Tangu amechukua lile jimbo limepiga hatua kubwa sana kimaendeleo,

Mtaturu Chapa kazi,
Sasa Lisu anaingia vp hapo? Jamaa ameanza kuwasumbua hata hajafika🤣🤣
 
Mbunge Miraji Mataturu singida kuna uwanja wa ndege?
Nimeuliza tu
 
Hawa Wabunge wetu ni aibu tu hawajui uchumi wetu tuliamua uendeshweje au hawasomi. Tanzania tuliamua kuwa sehemu kubwa ya uchumi wetu itaendeshwa kwa ushindani kwa maana kuwa watoa huduma wawe wengi na watashindana kutoa huduma kwa wananchi. Kufikia somo hili tulijifunza baada ya Shirika la Ndege wakati wa Ujamaa kuwa na ukiritimba: wakati huo kupata nafasi ya ndege kutoka Mwanza-Dar ulikuwa uhonge. Serikali ikaamua tuwashindanishe watoa usafiri wa ndege chini ya uangalizi wa Mdhibiti. Wameshindana na nafuu tumeiona. Watanzania wengi wameweza kusafiri kwa ndege kwa sababu nauli zilikuwa zinafikika. Serikali imerejesha ukiritimba wa ATCL kwa kupunguza ushindani pia kufifisha nafasi/ uhuru/ uteuzi wa Mdhibiti. Bunge lipo na wachache wanalalamika bila kufanya utafiti wa kina. Ndiyo maana nchi zetu zinaitwa majina mabaya. Maneno mengi yasiyo na tija wala mantiki! Tunapenda kurudi kwenye matope kuliko kujikwamua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…