Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Nguvu3...
Ni kauli ya CCM ,kuulinda "muungano" kwa gharama yoyote iwayo.
Kubaka demokrasia ina gharama zake. Ukipiga mahesabu ya haraka, Magu amepeleka jeshi, askari polisi na vifaa Zanzibar ili kuhakikisha maigizo ya uchaguzi wa marudio yanafanikiwa kwa kiwango kile CCM walijipangia. Shilingi bilioni ngapi zimetumika hapo?
Igizo lenyewe kwa mujibu wa ZEC limegharimu shilingi bilioni 5+, kuchapisha "vikaratasi" huku CCM ikiamini serikali/ nchi haitolewi kwa "vikaratasi"/ kura. Ukichanganya na Trilioni za MCC.

Gharama hazitoishia hapo. Tunaelekea kuisoma namba vile inavyotakiwa isomeke. Hapana kazi tu.
"Maisha bora" waliyotupatia CCM wakati wa mtembeza bakuli ili tusife njaa, yanageuzwa jipu na bora kuishi katika zama za utumbuaji majipu. Huku mtaani maisha yanatishia uhai na kwa kukosa lishe majipu yameanza mwilini na majipu yanatishia uhai. Naiona Tanzania mpya ile inakuja, Tanzania ya viwanda. Viwanda vya majipu.

Kung'ang'ania madaraka ina gharama zake bana.

Tanzania Mpya ya utumbuaji majipu inaua nafasi za kazi hapo kwa miradi ya MCC kusitishwa. Ni wafanyakazi wangapi( walalahoi) watalazimika kuingia katika mbinu mpya za kupunguza ujambazi?

Magufuli ni CCM na CCM imejipa "haki miliki" ya nchi ya "wadanganyika". Hivi kati ya 45 milioni waccm ni wangapi?
Ukiondoa hao wasisiemu kati ya 45 milioni,waliobaki ni majipu. Majipu ni lazima yatumbuliwe na maumivu hayaepukiki.
Hapana kazi tu!

Ukapa unajirudia? Kila zama na mambo yake- Ali Mwinyi( Mzee ruksa)

Link US pulls Tanzanian aid worth $470m over Zanzibar vote - BBC News

Link2. Uchaguzi Zanzibar wazuia mabilioni

Fedha hizo za MCC awamu ya pili ni kwa ajili ya kuiwezesha Tanzania kusambaza umeme na kuwaunganisha wananchi wengi katika Gridi ya Taifa na uimarishaji wa taasisi zinazohusika na na sekta ya nishati.

Mambo ambayo Serikali ya Marekani iliitaka Tanzania kumaliza haraka ni suala mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar pamoja na kupata ufafanuzi wa watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni, wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.

Akizungumza na Nipashe, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema suala hilo haliisumbui serikali na ni tatizo dogo ambalo linatatuliwa.

Alisema serikali ina uhakika wa kumaliza masuala hayo kabla ya kikao hicho cha Bodi ya MCC kukaa ambao masuala hayo yatakuwa yameshatatuliwa na kupatiwa ufumbuzi.

Alisema Bodi ya MCC ilikaa kikao chake cha kwanza Septemba, mwaka huu na inatarajia kukaa tena kikao chake Desemba, mwaka huu.

Alisema serikali ina uhakika Bodi ya MCC ikikaa kikao cha Desemba, mwaka huu itapitisha pasipo na shaka yoyote. link Serikali yazungumzia tishio la Marekani


Kura laki 2 na elfu 99 alizobuni Jecha/ CCM kumpatia Urais Dr. Shein zinagharimu zaidi ya shs. trilioni 1 kwa mwaka. Hili nalo ni jipu.
 
Msikilize mtu anasema hataki msaada wakati hata matangazo ya siku ya choo yanafadhiliwa na watu wa Marekani
Je makusanyo ya Magu yatanunua dawa za ARV wanazopewa waathirika nchi nzima bure kwa msaada wa wahisani,wakati malaria inaua watu wengi kuliko ukimwi na hakuna dawa ya bure
Aah!...yako mengi mengine
 
Africa bila misaada ni ngumu kuendelea tuache mbwembwe tuwe wakweli, Kwetu ni pigo kubwa sana
Jamani tutofautishe maamuzi ya vyama na maamuzi ya nchi yaani nikiwa na maana ya maamuzi ya wananchi
 
Mkuu hushawahi kaa area Q? Sorry lakin!!!!
 
mlipokuwa mnachezea demokrasia hamkujua kuna MCC? kuna mtu humu namuunga mkono anaposema kwenye hili la mcc hawezi kuvaa uzalendo wa kinafiki. mleta uzi unaandika upuuzi wa karne eti sijui madini, mapori tele, haya yote sio mageni hapa nchini, kilitushinda nini kuendelea mpaka rais wetu aliyepita akawa anasafiri kaila siku kwenda kutuombea kibaba? propaganda kwwnye huu upuuzi wa ccm huku mkijifanya nchi kwanza kumbe pembeni ni ccm kw
 
tufike sehemu tujikubali,,ipo siku watatuonea wivu,,ndipo misaada yao haitakuwa na mashart makali,,mcc safar njema natambua ipo siku mtarud kwa jina lingine namsipe nafas kirahis kama mlivyo ingia.
 
Mkuu ile imani kali ya mwalimu enzi za ukoministi ulioshindwa unaigizwa kimagumashi na miCCM iliyomfuata kwa kuchanganyikiwa (yaani hayana dira wala mwelekeo). Wanajifaragua kwenye vyombo vya habari walivyopora na kuwadhibiti wengine wasitumie vyombo mbadala. Hawaheshimu maamuzi ya wapiga kura iwe bara au visiwani. Hawana dhamira ya kutafuta muafaka uwe wa kisiasa au wa kiutawala.

Hawa wababe tuwaiteje sasa? Wanapanda migongoni mwetu kutuumiza na kutunyima misaada toka nje kwa maslahi yao. Angalau humu JF tunaweza kuweka maoni mbadala. Wamejazana humu kuhoroja kwa maslahi ya watawala wababe na kujiita wana akili ya kuielewa dunia. Hili LA MCC ni racking ya kijeshi tusubiri shambulizi halizi
 
Mimi Niliweke wazi Jambo hili bila kupepesa Macho, japo mimi siungi Mkono Misaada ya wageni. Maana nchi hii ni Tajiri sana.

Tusi jifichie Maovu yetu kuwatukana hawa mabeberu, bali Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu. Tanzania na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi watende Haki waache Michezo michezo yao ya ujanja ujanja, Taifa lisimame kwenye misingi ya Ukweli na haki "HAKI UINUA TAIFA"

Tuache Michezo, maana siyo mizuri isije ikatugharimu kutuondolea Amani yetu jamani, maana ugumu wa maisha unavyozidi mitaani inapelekea chuki na kuzalisha makundi ya ualifu.

Mwisho. Tujenge nchi yetu kwenye misingi ya taifa linalojitegemea jamani, Hembu tujiulize hao wamarekani na wachina wao wanakopeshwa na waisani gani?

Mbona Kanali muhamar gadaffy aliweza kuiendesha libya bila kutembeza bakuli kwa wazungu na wachina? Sisi katuroga nani?

Hembu turudi kwenye misingi ya haki tuache uroho wa madaraka, kama ccm kimeshindwa kuwaletea watanzania maendeleo kwa miaka 50 basi kwa moya mweupe wawape na wenzao nao waendeleze gurudumu.

Tuige basi mazuri ya wenzetu, democrat na republcan vyama shindani vya marekani, vinabadilishana madaraka kwa demokracy kabisa, umeshindwa kaa pembeni baada ya miaka 4 wananchi wataamua, wenzetu wameondokana na ujima wa kutaka wewetu ndiyo utawale hata kama uwezo wako wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi umefikia ukomo.

Wenzetu wanathamini sana Maendeleo, ndiyo maana hata wafuasi wa vyama vyao hawashabikii chama kama vilabu vya soka. Bali upima hoja na uwezo wa chama na mtu husika.
 
Yani polepole anaona kidonda kimetokana na kung'atwa na nyoka aitwaye moma halafu anasema hakkiwezi kufanya mguu ukatwe kwasababu mguu umeungana na tako na kiuno hivyo kidonda cha Kansa ya nyoka kitaondoka kiuache mguu hata kama hakitibiwi. Sijui anajua kule kwao kondoa ule umeme utaongezwa bili?sijui hajui kama yale maji ya 50 yatakuwa 2000 kwa ndoo kule kijijini?sijui anawazaje kuhusu elimu vijijini ambayo serikali ilitegemea miradi hii ili ijiendeshe?Ukiwa na uwezo wa kufikiri kasha ukaamuungaa mkono polepole lazima utakuwa umelaaniwa kwa kumchungulia mzazi wako akiwa anaoga
 
Mtizamo wangu pia nikuwa, Tanzania siyo kisiwa, kiasi cha kujifanya tunaweza kujitegemea. Tuwe wakweli juu ya hili. Tusidhani ni hili tu bali litakwenda kutuharibia hata mahusiano yetu mengine. Mimi ninaamini Tanzania tukiingia wenyewe mkataba huo na sasa tumeshindwa masharti hivyo tunastahiki kufanyiwa hivyo wala yusijifari kwa kunakili maneno ya mwakimu ili kutupa public support. Miradi mingi itasimama na sisi hatuna ujanja wa kuiendeleza. Mimi ninamuomba Mh. Rais Magufuli asidanganyike na washauri wasioitakia mema nchi hii . Ajitajihidi kushughulkia suala hili kwa hekima kwakuwa ninajuaana hekima hiyo. Fedha hizo za MCC tunazihitaji sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote ule, ukizingatia chama chetu kimeahidi mambo mengi kuwafanyia wananchi. Mwalimu pamoja na kauli zake lakini aliizita nchi hizi ni giant kama hatutashikana nazo sisi wadogo tuta umia. Hivyo huo ndy wito wangu. Tuache kupotosha ukwelu
 
Hadi standard VII wanajifanya wataalamu wa uchumi, wanabeza misaada ya nje kwamba hatuihitaji...eti tuna uwezo wa kujitegemea.

Endeleeni kijidanganya, maana mnaongea msichokijua.
 
yaani nilivyo ona haraka haraka ndo mchambuzi nimeishia hapohapo....
 
Eti MCC naomba mh rais mstaafu jk atoe mtizamo wake juu ya hli I hope itasaidia
 
ukitaka kuona ujinga wa watanzania soma Uzi kama huu...eti Wao ndio wanajiita wazalendo.....
 
Kama Taifa tutasonga mbele mcc na madudu yake weka pembeni. We are great natiö. Hawatuwezi wala kamwe hawato tuweza. Mungu yupo upande wetu.
 
Umeenda mbali huko kwenye matangazo ya vyoo kutegemea wahisani halafu watu humu wakijidai kuwa tutaweza kwa kutegemea wanyamapori, madini n.k, huu ni Uzuzu kwani hata vita tu ya kupambana na majangili kwa wanyama wetu tunategemea Wahisani, madini waamuzi wa bei ni hao hao wanaoitwa wahisani wakati mwingine watz tuacheni mbwembwe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…