Nguvu3...Mkuu watu kama PolePole nilisema ni hatari kwa ustawi wa Taifa, wanaishi kwa uongo na ubabaishaji. ......Tumevunja uhusiano kwasababu ya kumweka Shein madarakani.Yaani kundi la Wahafidhiana wasiozidi kumi limeweka nchi ya watu milioni 45 rehani.
Kundi halina uzalendo wakati Jecha anatumbikiza Taifa la watu milioni 4 matatizoni.
Wakati Shein anagomea matokeo kwa kigezo cha demokrasia ya Afrika.
Wanatuaminisha kilichofanyika ZNZ ni demokrasia tuungane nao katika uzalendo wa kihuni. Wanajua watakaposema sisi ni mazezeta tutawaunga wamkono!
Hapana! Wazalendo wa nchi hii tusimame pamoja na kumwambia Magu, ameliweka Taifa rehani kwa interest za Shein na wahafidhina wanaoishi 'peponi kwa sasa''
Masilahi ya watu wasiozidi 10 ni bora kuliko masilahi ya watu milioni 45!!!
Hapana tukatae na kumwambia Magu uzalendo huo ni kundi lake .
Uzalendo wetu ni kwa masikini milioni 40 wa Taifa hili.
Tunasema wazi, hili MCC wapo sahihi, wananchi milioni 45 wapo sahihi.
Waliokosea ni Magufuli akitetea watu wasiozidi 10 kwa gharama ya watu milioni 45
Tuweke siasa kando, tukemee Wazalendo ni milioni 45 wanaoteseka kukosa MCC ni muhimu kuliko watu wasiozidi 10
Hili ni la Magufuli! Hakuna uzalendo isipokuwa wa watu milioni 45!
Milioni 45 ndio wazalendo.
Tusimame na kumwabia Magufuli hapana! hili na wenzake wachache hautukubali
Ni kauli ya CCM ,kuulinda "muungano" kwa gharama yoyote iwayo.
Kubaka demokrasia ina gharama zake. Ukipiga mahesabu ya haraka, Magu amepeleka jeshi, askari polisi na vifaa Zanzibar ili kuhakikisha maigizo ya uchaguzi wa marudio yanafanikiwa kwa kiwango kile CCM walijipangia. Shilingi bilioni ngapi zimetumika hapo?
Igizo lenyewe kwa mujibu wa ZEC limegharimu shilingi bilioni 5+, kuchapisha "vikaratasi" huku CCM ikiamini serikali/ nchi haitolewi kwa "vikaratasi"/ kura. Ukichanganya na Trilioni za MCC.
Gharama hazitoishia hapo. Tunaelekea kuisoma namba vile inavyotakiwa isomeke. Hapana kazi tu.
"Maisha bora" waliyotupatia CCM wakati wa mtembeza bakuli ili tusife njaa, yanageuzwa jipu na bora kuishi katika zama za utumbuaji majipu. Huku mtaani maisha yanatishia uhai na kwa kukosa lishe majipu yameanza mwilini na majipu yanatishia uhai. Naiona Tanzania mpya ile inakuja, Tanzania ya viwanda. Viwanda vya majipu.
Kung'ang'ania madaraka ina gharama zake bana.
Tanzania Mpya ya utumbuaji majipu inaua nafasi za kazi hapo kwa miradi ya MCC kusitishwa. Ni wafanyakazi wangapi( walalahoi) watalazimika kuingia katika mbinu mpya za kupunguza ujambazi?
Magufuli ni CCM na CCM imejipa "haki miliki" ya nchi ya "wadanganyika". Hivi kati ya 45 milioni waccm ni wangapi?
Ukiondoa hao wasisiemu kati ya 45 milioni,waliobaki ni majipu. Majipu ni lazima yatumbuliwe na maumivu hayaepukiki.
Hapana kazi tu!
Ukapa unajirudia? Kila zama na mambo yake- Ali Mwinyi( Mzee ruksa)
Link US pulls Tanzanian aid worth $470m over Zanzibar vote - BBC News
Link2. Uchaguzi Zanzibar wazuia mabilioni
Fedha hizo za MCC awamu ya pili ni kwa ajili ya kuiwezesha Tanzania kusambaza umeme na kuwaunganisha wananchi wengi katika Gridi ya Taifa na uimarishaji wa taasisi zinazohusika na na sekta ya nishati.
Mambo ambayo Serikali ya Marekani iliitaka Tanzania kumaliza haraka ni suala mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar pamoja na kupata ufafanuzi wa watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni, wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
Akizungumza na Nipashe, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema suala hilo haliisumbui serikali na ni tatizo dogo ambalo linatatuliwa.
Alisema serikali ina uhakika wa kumaliza masuala hayo kabla ya kikao hicho cha Bodi ya MCC kukaa ambao masuala hayo yatakuwa yameshatatuliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Alisema Bodi ya MCC ilikaa kikao chake cha kwanza Septemba, mwaka huu na inatarajia kukaa tena kikao chake Desemba, mwaka huu.
Alisema serikali ina uhakika Bodi ya MCC ikikaa kikao cha Desemba, mwaka huu itapitisha pasipo na shaka yoyote. link Serikali yazungumzia tishio la Marekani
Kura laki 2 na elfu 99 alizobuni Jecha/ CCM kumpatia Urais Dr. Shein zinagharimu zaidi ya shs. trilioni 1 kwa mwaka. Hili nalo ni jipu.