Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

dawa chungu ndio inaponyesha - hii itasaidia kuondoa ukurunzinza - chama kikifika wakati wa kung'atuka kitoke kwa Amani na ushirikiano.
 
Kumbe kina Lowasa waliosema Serikali hii haina maono waliona mbali sana ,
 
MCC is just the beginning. Let's wait and see the bigger picture.


Hakuna cha bigger picture Marekani huwa hamumunyi maneno, kwa hali ya kawaida tayari sasa hvi Balozi angeshaongea na kutoa tamko rasmi la nchi yake kwanza sia ajabu kesho ukamuona yuko Chato wanakula samaki na Magufuli!
 
Bwana Pole Pole wewe ni mjinga kama CCM wenzio!

Sijui kama uwezo wako wa kufikiri uko sawa sawa!

Yaani wewe kazi yako ni kutetea kitu chochote cha CCM, kiwe kizuri au kibaya!
 
Na watakapo sitisha utoaji wa dawa za UKIMWI, TB na kutochangia gharama za dawa za Malaria ndipo hawa watu Jamii ya Polepole ndio watajua athari juu ya kudharau maoni ya nchi wahisani pale wanapotaka nchi iwe na Demokrasia huru na utawala bora ili hata wakitoa fedha zao ziwafikie walengwa.
 
Mamistari meengi. ...kwa kifupi waache hao mabepari waende na hela zao. ..

Hatutaki samaki wa kupewa. ..tunajifunza kuvua
 
tufike sehemu tujikubali,,ipo siku watatuonea wivu,,ndipo misaada yao haitakuwa na mashart makali,,mcc safar njema natambua ipo siku mtarud kwa jina lingine namsipe nafas kirahis kama mlivyo ingia.
Duh!!! Marekani aionee wivu Tanzania hili litakuwa ajabu La 9 la Dunia kwa kipi hasa? Mijitu kama nyie ndio mliotufanya tuwe hivi yaani masikini halafu mnatetea upuuzi wa CCM Nyambaaaafu!
 
Waheshimiwa, Watanzania wenzangu.
"...Hii haiingii akilini..."
Mie sio mchumi, wala mwanasiasa, walakini najua maana ya uzalendo.

Tunalumbana for and against na hili, ni sawa ndio domokrasia tuliopewa. Zaidi ya hapo wao, "Wamarekani" demokrasia yao ipo kwenye matata. Fuatilia kinyang'anyiro cha urais huko mifano ipo huko na usikie domokrasia yao huko. Hakuna democracy ya kweli. Inakuwaje waje watueleze namna ya kufanya uchaguzi? Kwa domokrasia? wakati kuna demokrasia na sheria mbadala Tanzania?

Mbali na hayo, hizi karoti zimepitwa na wakati, zimeoza na hatuzitaki.

And for Domocracy sake take your money and shove it up "...I dont know where..." your choice! You have banks, flint and so on and forth. Urgh!

Kwa wananchi wenzangu, hili tulikubali kwa kukataa. Tunajua nani wametufikisha hapa. Angalieni kura zenu uchaguzi ujao. Walakini, masharti kama hayo hayana pahali kwake katika katika karne hii wala zijazo Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Ni maoni yangu.
 
We mch...ia tumbo kumbuka unaongea hii hadithi ukiwa bado na pesa ulizotumbua wakati wa rasimu hewa ya Warioba na ile uliyolipwa kumchafua Lowassa. Watoto wa wakulima wala huwezi fahamu maisha wanayoishi huko vijijini. Ni bora ukanyamaza usubiri hiyo zawadi yako
152c3e730c2b00a6dbcf292edc8653c5.jpg
 
Na watakapo sitisha utoaji wa dawa za UKIMWI, TB na kutochangia gharama za dawa za Malaria ndipo hawa watu Jamii ya Polepole ndio watajua athari juu ya kudharau maoni ya nchi wahisani pale wanapotaka nchi iwe na Demokrasia huru na utawala bora ili hata wakitoa fedha zao ziwafikie walengwa.
Aka kajamaa huwa ninakasikiaga kanapigapiga propoganda mfu - ni kazaliwa ka wapi na kamesoma hadi darasa la ngapi vile? Maake wakati mwingine twawezajikuta tunabishana na vihiyo hapa ambapo ni upotezaji wa muda na nguvu.
 
..... ukuu wa wilaya utawatoa roho wachumia tumbo wa lumumba
 
Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.
Hizo dola bil 3 kwa Egypt & billion 6 kwa Israel ni za mfuko wa MCC? Acha kuchanganya mambo na kujivua ufahamu. Mmeshawapora waZNZ haki yao ..endeleeni tu kusheherekea na kupeana nyadhifa
 
blah! blah! mineno ya mkosaji. trillion 1.2 zileeeeee
 
MTIZAMO WANGU KUHUSU BODI YA MCC KUSITISHA

MSAADA WA MCC 2 KWA SERIKALI YA TANZANIA


C:\Users\toshiba\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif
I

Na Alexander Mhando

Inasikitisha sana Kwa Kuwa Na Rais ambaye Ta alnzania anajitahidi sana, Na Kabla ya hata Kuwa Rais alikuwa ndiye Kiongozi almost pekee aliyefanya Kazi Kwa bidii na Kusaidia Taifa katika Maswala ya Uchukuzi/Ujenzi na sasa akiwa Rais anajitahidi, Katika Huduma za Jamii na kupingana na Ufisadi.

Hata Hivyo, Haihitaji hata cheti cha Darasa la Saba Kujua inapokuja kwenye Demokrasia, Chaguzi, Madaraka ya Umma, CCM Ni Wezi, Wapuuzi, Na Ni mfumo wa Udictator na Ukandamizaji wa hali ya juu. Kuwa na Taifa linaloongozwa na Chama chenye Tabia kama ya CCM, Ni aibu kwa Taifa na Kwa Dunia.

Porojo za Polepole hazina maana yoyote. Tanzania ina Bahati sana, Kwa Tabia za CCM, Tanzania ilistahili sio Kunyimwa huo msaada wa MCC, Bali Tanzania hasa kwa Uhuni CCM iliyofanya Zanzibar, Tanzania inatakiwa Iwe kicked out ou UN, Na Iwekewe Vikwazo vya uchumi. Na Kisha Waliohusika Kufuta Uchaguzi wa Zanzibar, Kama ikitokea machafuko yoyote as the result wanatakiwa Kukamatwa Na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binaadamu.

Utangulizi;

Tukianza na nukuu ya Baba wa Taifa alisema “…….Inapotokea taifa kuuza uhuru wake kwa ajili ya misaada ya kiuchumi au kukubali kukaliwa na majeshi ya nje, taifa hilo linakuwa limepotea na litanyonywa na watu wake watakuwa wanakandimizwa popote pale……” alisema Mwalimu.

Katika swala la msaada wa pesa za Millenium Challenge Corporation’s (MCC) ambazo huwa tunapewa nchi zinazoendelea kama msaada kwa ajili ya Maswala ya maendeleo kwa Nchi zetu, Pesa hizi hutolewa na Bodi ya Shirika la changamoto za Milenium (MCC) ambayo inamilikiwa na serikali ya marekani ili kusaidia nchi zinazoendelea.

Katika kikao cha Bodi ya MCC kilichokaliwa jana tar 28/3/2016 kimefikia uamuzi wa kutishia kusitisha pesa za msaada za MCC kwa Tanzania kwa sababu walizozitoa wao ambazo ni swala la uchaguzi wa Zanzibar na swala la sheria za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii katika uchaguzi wa Zanzibar na wa mwaka jana.

Tukikumbuka Katika kikao cha tar 16 December mwaka jana cha Bodi ya MCC, Bodi ya MCC katika kikao chake ilijadili pendekekezo la mkataba mpya na serikali ya Tanzania wenye thamani za Dola za Kimarekani Millioni 472.8 na kuamua pesa hizo zitolewe baada ya Tanzania kutimiza kigezo cha kuzuia Rushwa. Msaada huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuimarisha secta ya umeme nchini, likiwa lengo ni kuwawezesha watanzania wengi zaidi kupata nishati hiyo kwa uhakika na kwa bei nafuu. Lakini pia kuimarisha taasisi zinazohusika na usambazaji wa nishati ya umeme na usimamizi wake.

Katika hali ya kushangaza swala la Rushwa limeshafanyiwa kazi na serikali ya awamu ya Tano kwa kasi kubwa kupambana na Rushwa na Ufisadi lakini bado Bodi ya MCC wanakuja na hoja nyingine nakuaacha ile ya kwanza ya Swala la Rushwa na ufisadi. Sasa swali la kujiuliza je, MCC wanataka tuuze uhuru wetu na utu wetu kwa pesa za msaada??



Mtizamo wangu;

Hatutakiwi tudharau misaada yoyote tunayopewa lakini tusikubali katu kuuza uhuru wetu au mali zetu kwa sababu ya msaada, tukikumbuka mwalimu Nyerere mwaka 1964 alikubali kuvunja uhusiano na Ujerumani Magharibi pale walipotaka kuingilia umoja wetu na Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar. Lazima tujue kuwa MCC ni sehemu tu ya Bodi inayojitegemea na sio serikali ya Marekani japo inasimamiwa na serikali ya Marekani, kwa hiyo kukosa msaada wa MCC hautatuathiri chochote katika uhusiano wetu na Taifa la Marekani kwani kauli ya MCC sio Kauli ya Serikali ya Marekani. Uhusiano wetu na Taifa la Marekani bado uko palepale na hautatetereka kwa sababu ya pesa za MCC.

Tukikumbuka AZIMIO LA ARUSHA la mwaka 1967 chini ya TANU lilikuwa na maudhui mbalimbali, moja lilikuwa ni swala la Pembe tatu za ukombozi ambapo lilitambua kwamba uhuru wanchi hautakuwa na maana wala hatutakuwa salama kama tukiendelea kuwa tegemezi , yaani kutegemea misaada , mikopo na uwekezaji kutoka nje. Kwa sababu mikopo haitapatikana ya kutosha na hiyo kidogo itakayopatikana itaambatana na masharti yatakayodidimiza nchi zaidi. Isitotoshe hata kama tungepata misaada, mikopo na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo vitahatarisha uhuru wetu. Mwalimu Nyerere katika kitabu cha Azimio la Arusha amesema, “Kujitawala ni kujitegemea, kujitawala kwa kweli hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo kutoka Taifa jingine kwa maendeleo yake” mwisho wa kunukuu.

Pia tuambue kuwa Serikali ya Tanzania kwa awamu hii ya Tano chini ya Raisi Dr John Pombe Magufuli, imejipanga kikamilifu katika kukusanya kodi na kutafuta pesa kwa ajili ya kuendesha serikali bila hata kutegemea misaada ya wahisani ambayo ina masharti magumu na yenye ukandamizaji na unyonyaji ndani yake. Katika Pesa hizi za MCC lazima tujiandae kisaikolojia na sio kupotosha kwani Tukipatiwa pesa hizi au Tusipopatiwa pesa hizi bado tunaamini tutaweza endesha serikali yetu na maisha yetu kama kawaida. Tukumbuke kuwa pesa hizi zilianza kutolewa mwaka 2008 , Je, kabla ya hapo serikali ilikuwa inajiendesha vipi? Kama Tuliweza kujiendesha maisha yetu na serikali kwa kipindi hicho , hata sasa tutaweza. Hatudharau pesa za msaada na za wahisani lakini tusitumie kama kigezo cha kuondoa uhuru wetu na utanzania wetu kisa pesa za misaada. Lakini pia tutambue kuwa pesa za MCC sio marekani pekee anayechangia zipo nchi nyingine .

Lakini pia Vyama vyetu vya siasa nchini vijifunze utaifa na uzalendo, Ni aibu kuona chama cha Siasa cha Tanzania kinaungana na maadui wakutoka nje wasioitakia mema nchi yetu kwa kushabikia kila nia yao ovu juu ya maendeleo ya nchi yetu, tutambue kuwa si kila nchi kwa sasa inafurahia mafanikio ya Tanzania mfano uwepo wa Gesi, Madini yakutosha aridhini, wanyama pori wa kila aina, mlima Kilimanjaro,samaki wakutosha ziwani na baharini, ardhi ya kutosha, Bandal, misitu mikubwa, n.k hivi vyote tutambue si kila taifa litafurahia sisi kuwa navyo wanatamani tuvunje amani yetu ili waje wachukue mali zetu.

Rai yangu kwa Vyama vya upinzani nchini jaribuni kuweka utaifa kwanza na siasa baadae, swala la kukaa kushabikia vibaraka weupe wenye lengo la kutukandamiza sio jambo zuri hata kidogo na huo sio uzalendo. Katika Tamko lililotolewa na CHADEMA lenye kichwa cha Ujumbe “Hatma ya msaada wa Fedha za MCC kwa serikali ya Tanzania” ni tamko linaloonesha kushabikia swala la MCC kuikandamiza Tanzania. Tusilete siasa kwenye maswala ya kitaifa na maendeleo ya wananchi. Na hii inaonesha kuwa vyama hivi kama vitapewa dora vitaongoza nchi kwa kutegemea kuombaomba kwa wazungu na mwishowe vinaweza hata kuuza mali za nchi ili kutafuta msaada nje, kwa hili upinzani badilikeni wekeni utaifa mbele na sio tamaa ya uongozi.

Mwisho;

Lazima tujue kuwa msaada mtu anahiyari yake akusaidie au la. Vile vile misaada ni silaha kubwa kwa nchi za magharibi kulidumaza bara la afrika na kuhakikisha haliwezi kujitegemea bali liwategemee wao kwani misaada mingi inayotolewa na nchi hizi hailengi sehemu za maendeleo ya nchi na wananchi wake, na siku zote riba zake huishia kuwa kubwa kuliko misaada yenyewe na kwa kweli nchi yenye kujitambua haiwezi kujiendesha kwa kutegemea misaada hasa kutoka nchi kama marekani utanynyasika tu.


COPIED AND PASTED

Ni mtizamo wako juu ya MCC , binasfi namuunga mkono aliyeandika huu waraka kiukweli sio muda wa kumbembeleza msaada , bora tupambane tujitegemee.

tufike sehemu tujikubali,,ipo siku watatuonea wivu,,ndipo misaada yao haitakuwa na mashart makali,,mcc safar njema natambua ipo siku mtarud kwa jina lingine namsipe nafas kirahis kama mlivyo ingia.
o
 
Sipo tayari kuvaa koti la uzalendo wa kipuuzi linalotangazwa na CCM! MCC haiuzi uhuru wa Tanzania bali inapambana na uhuni wa CCM na watu wake! Mimi simo kwa wana CCM wanaoungana kujifariji na matokeo ya uhuni wao kule Zanzibar! Hilo ni la wana CCM na kamwe msihusishe watanzania wengine!
Hayo ndo matokeo ya kuwa tegemezi. Mfano huu wa MCC unafaa kufundishia watoto wetu mashuleni ili wakue waki uchukia utegemezi na hasa wa nchi yetu kwa nchi za magharibi. Uingereza ilishawahi kutamka wazi kuwa haitatoa misaada kwa nchi itakayopinga ushoga. Na kauli hiyo ilisumbua sana Africa lakini hatukuwa na la kufanya zaidi ya kukubali.
Kwa hiyo Mkuu unapaswa kuuchukia utegemezi na hapa uanze na utegemezi wa kipato yaan uchumi wako.

Ndan ya miezi sita tutakuwa tumepata hela hiyo hela na zaidi. Ni hela ndogo sana hiyo. Ni asilimia 80% tu ya makusanyo ya mwezi. Ni vizuri kujitambua na kutoharibu nchi kwa minajiri ya kuwafurahisha wazungu.

Hata waliodai uhuru walipambana hawakuogopa kuwa mzungu akiondoka nchi itapata shida. Waliamua kumfukuza mzungu no matter what. Walifanikiwa na nchi zimeendelea kuwepo.
 
Uzalendo Gani wa Kupongeza Wezi wa Madaraha Tena Bila ya aibu. Na ati Niliona Jaji Mkuu, aliyekula Kiapo cha haki na Bible,au Msahafu, ati Akimwapisha Mtu aliyepora Madaraka Waziwazi. Sisi Watanzania Tunatakiwa tuone aibu kuwa badala ya Sisi Kuona Kinyaa, Wageni wa Mataifa Mengine wanaona Kinyaa kwa Niaba yetu, aibu!
 
Hayo ndo matokeo ya kuwa tegemezi. Mfano huu wa MCC unafaa kufundishia watoto wetu mashuleni ili wakue waki uchukia utegemezi na hasa wa nchi yetu kwa nchi za magharibi. Uingereza ilishawahi kutamka wazi kuwa haitatoa misaada kwa nchi itakayopinga ushoga. Na kauli hiyo ilisumbua sana Africa lakini hatukuwa na la kufanya zaidi ya kukubali.
Kwa hiyo Mkuu unapaswa kuuchukia utegemezi na hapa uanze na utegemezi wa kipato yaan uchumi wako.

Ndan ya miezi sita tutakuwa tumepata hela hiyo hela na zaidi. Ni hela ndogo sana hiyo. Ni asilimia 80% tu ya makusanyo ya mwezi. Ni vizuri kujitambua na kutoharibu nchi kwa minajiri ya kuwafurahisha wazungu.

Hata waliodai uhuru walipambana hawakuogopa kuwa mzungu akiondoka nchi itapata shida. Waliamua kumfukuza mzungu no matter what. Walifanikiwa na nchi zimeendelea kuwepo.
Uhuru Gani CCM wanaopigania? Wa Dunia Kuwanyamazia Wanapoiba Madaraka? Uhuru huo Mkautafute Jehanamu!
 
Back
Top Bottom