Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Misaada ya kistaarabu ni ile ambayo haiambatani na masharti. Unafahamu kwanini Baba wa Taifa alielekea China kuomba msaada wa kujenga reli ya TAZARA? Ni kwasababu nchi za magharibi wakati ule zilitoa masharti mengi ikiwemo kutounga mkono jitihada za nchi za Kusini kujipatia uhuru wao!
Kuwa kama msomi umeulizwa specific question wewe unatoa jibu la jumla. Tafadhali jibu specific tena kwa details and supportive data.
Taja msaada na masharti yake then conclude kuwa ni wakistaarabu au sio wakistaarabu.
 
PolePole Unapozungumzia kupewa Pesa ili ikusaidie siasa haziusini hapo!. Kila kitu duniani kina Masharti. Na Mashariti yanabadilika kutegemea vipaumbele vya mtoa Masharti. Unapozungumzia Marekani kutoa ela Misri au Israel bila Masharti ivyo ni vipaumbele vyao kwa hao na sisi tuna vya kwetu. Mbona China anatoa Msaada Korea Kasikazini wakati Mataifa mengine hayatoi, au Urusi anazisaidia kinyume cha Sheria ya kimataifa Ossetia ya Kasikazini, Abkhazia pesa nyingi yajitenge zidi ya Georgia? Yote kwa sababu wana vipaumbele kwa hao. Kipaumbele cha Tanzania ni Maendeleo, kiwe kidogo au kikubwa tunakiitaji either kutoka Uchina au USA. Labda uniambie kwa sasa tumefanikiwa tayari, kama Sivyo unachoongea hapa ni Sizitaki mbichi hizi uku tunachechemea. Tumepoteza na tutaumia!!!!.
 
Tangu lini muajiriwa wa kitengo akaipinga serikali yake?? Je tunafahamu umuhimu wa fedha za kigeni kwenye mzunguko?? Je unafahamu mataifa ya nje yakiacha kutoa nsaada thamani ya shilingi itashuka dhidi ya dola?? Je unafahamu uwezo wa nchi yetu kuuza nje ili kupata fedha za kigeni upo chini sana kiasi kwamba misaada ya wahisani ndio inaongeza fedha za kigeni kwenye mzunguko wetu, je unafahamu hali hii ikiendelea ya kukosa misaada ya wahisani bidhaa za nje zitakuwa ni ghali sana kiasi cha watanzania wengi kushindwa kuzipata?
Je wajua asilimia 50+ ya bajeti inahitaji fedha za wahisani, je wajua kukiwa na mdororo wa kiuchumi hayo makusanyo yatashuka hadi aibu? Yapo mengi ila ngoja nichangie taifa hapa kwa kunywa castle lager ya baridi
Kumbe fedha za kigeni zinaletwa na MCC tu au ndio pesa yetu ingeongezeka thamani maradufu mkuu
 
Binafsi nimefurahi sana kwa kunyimwa huu msaada.

Ni wakati muafaka wa kufanya yetu bila kutegemea misaada.
Kuipa cuf zanzibar ni kukaribisha ugaidi wa waislam wenye madevu..by Samuel Six....ahahaaa..faizaaaaaaaaaa...
 
Vyandarua, Dawa ya Mseto(maleria),ARV/HIV, Condoms, Utafit, Barabara(namtumbo,Mbinga, Sumbawanga, Iringa etc), symbion Ubungo, Vyuo(Dodoma), Umeme(REA) na Power Africa, Kutupunguzia Madeni, Kutulinda dhidi ya Magaidi(FBI) Yooote hayo na Mengine mengi ni kwa hisani ya watu wa Marekani. Umoja wa Ulaya (EU) nao Umesema anakuja na ya kwao. Mtu bora duniani ni yule anaesoma nyakati, je hizi nyakati ndo za kukataa misaada??. Je ni kweli sisi ni tajiri(Kuwa na Mali nyingi ardhini ndo inamaanisha utajiri au Vinginevyo)(Japan aina malighafi yoyote ya maana ardhin lakini inaitwa tajiri na ukiingalia ni Matajiri).
 
Mi nadhani tujitafakari kama taifa, tusiwe watu wakuwa tunakurupuka tu nakutoa nukuu mbali mbali wakati ukweli ukowazi.

Nchi inalaumiwa kwakukiuka misingi ya Demokrasia, tena wazi wazi kabisa hata mtoto mdogo ambaye hata shule hajaanza hili ukimuuliza stakupatia jibu. Tusijidanganye, tutakaoumia nisisi wenyewe. Walichofanya Ccm kinapaswa kulaaniwa nakila mtanzania anayeitakia mema nchi yake.

Kujipa Moyo huku hakutatufikisha popote nisawa na kuota umejenga ghorofa naumehamia ndani tayari, lakini ujue utakapozinduka usingizini Tembe hilo ndo lililo lako.
 
Watanzania tumekuwa watu wa kulalamika kila wakati hasa panapotokea tatizo libalogusa mstakabali wa taifa letu. Lakini tunasahau kuwa kulalamika tu bila kuchukua uamuzi tatuzi haisaidi hata chembe. Hii nisawa namethali ya wa zee wetu kuwa dua la kuku halimpati mwewe. Ni wakati muafaka kutafakari kwa kina tuliweza vipi kupata mamilioni ya Mcc hapo nyuma na tumeshindwa vipi kupata mamilioni hayo na kitu gani kifanyike.

Siku zote wazee wetu wanatuasa kuwa sikio likikua halizidi kichwa. Tanzania tunaweza kuwa namaendeleo yetu na mipango yetu mizuri lakini haiwezi kutuletea maendeleo bila kushirikiana na nchi zilizoendelea.

Mwanzo wa ngoma ni lele. Akumulikae mchana usiku atakuchoma. Muungwana akivuliwa nguo huchutama.

Je sisi tuchukue uelekeo upi kama nchi na tukishupaa shingo a.k.a kukomaa na maamuzi ya MCC au tuchutame na kufikia muafaka? Unasemaje???
 
KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Well said mkuu!! [emoji106]
 
Swala la kujitegemea ni swala la heri na zuri sana, na hili lazima kama nchi tulipiganie na tujitahidi ili ndoto yetu itimie.
Kuhusu suala la pesa za MCC, hizi pesa kwa hali hii tuliyonayo nahisi tunazihitaji, kwani zilisaidia sana kujenga miundo mbini ya nishati na barabara, sehemu kubwa ya Tanzania vijijini ilipata umeme, mie nimefika vijijini ndani ndani kule watu wananiambia huu ni umeme wa REA, hivyo ulikuwa na manufaa sana.
Kuhusu masharti yake nahisi sio magumu kivile, hata kabla ya kupewa na kusign huu mkataba nahisi serikali ya Tz iliyapitia masharti yote na ikakubali, moja ya mambo hayo ni pamoja na kudumisha democrasia nchini, ambalo pia ni jambo la heri, kama mkataba ungelikuwa na mambo ya udhalilishaji wa utu wa MTZ au uavunja unachochea kuvunjika kwa muungano wetu au mapigano, machafuko au mambo ya ndoa ya jinsia moja basi nina uhakika tusingekubali mkataba wa aina hiyo, sasa kwa leo hii tukija tukasema eti waende tu misaada yenyewe ina masharti kama hiyo tunakuwa hatueleweki, kwa nini hatukataa mapema? tungewaambia sisi tuna mpango wa kujitegema hivyo misaada kama hii hatuhitaji.Tujifunze ku implement kitu ambacho tuna kisign au tunakisema, wachina wanasema PRACTICE WHAT U SAY. Kama tuliamua twende na democracia basi tukifanye kitu kwa umahili zaidi, democrasia maana yake ni haki, haki inapofuatwa basi hiyo ndo democrasia, nahisi tukibadilika na tukaacha kuwa tunachukulia vitu juujuu na kuangalia chanzo cha tatizo bila kuoneana haya wala kuleta issue za vyama tutafika mbali.
Issue ya maendeleo pasipo misaada ya USA , inawezekana sana, lakini sio kwa kipindi hiki, bado tunahitaji kujipanga, mapato mengi tunayokusanya ndg zangu hayatoshi, hivi leo hii tunauza nini katika soko la dunia? hiyo china yenyewe ambayo ni largest export in the world soko lao kubwa lipo USA, haya mambo yalitokea enzi za china , wakajidanganya kuwa hii nchi bila wawekezaji, donors toka USA na europe tutaweza, lakini walishindwa, hivyo mwaka 1978 raisi wa china DENG XIAOPING akaanzisha issue za economy restructure na akamkaribisha raisi wa USA, NIXON kwenda china , na wakatenga maeneo ya uwekezaji china kutoka nchi za magharibi, at the same time china ilianza kudebate issue za human rights na comparison between ujamaa na ubepari ili kupunguza makali ya USA aweze kuingia china kuwekeza na pia kuendelea kutoa misaada wanapjipanga. Hivyo binafsi naona tuangalie mahali tulipojikwaa rujirekebishe tunapojipanga, hatuwezi kujietegema kwa staili ya kuongea kwenye TV ,radio ,wala magazetini tukiwa hatuna hata kiwanda cha maana Tanzania.
 
Mnawaita wasiofikiri nje ya sanduku wanaoututaka tutafute namna ya kutafuta Maendeleo yetu wenyewe kwa kuwa watoa misaada wanataka tuwapigie magoti,sijaona hata jibu la mmoja wenu kuhusu kinachotokea Misri,Israel( japo mimi ni muumini wa baraka za Waisrael),hakuna aliyejibu chochote kwa mahusiano yaliyovunjika baina yetu na Wajerumani,Waingereza na rafiki zao. Naomba niongezee na kuwakumbusha tena tija ya ushauri na maamuzi ya Marekani kwa Libya,Misri,Syria nk. Je mnaamini tunaweza kuendelea kwa misaada ? mimi siamini hivyo.Naamini tunaweza kuendelea kwa kushirikiana na wengine na wala si kwa kusaidiwa na wengine. Ni kweli tutaumia lakini maumivu yanapaswa kutufikirisha na kutafuta mbinu za kutatua;Vinginevyo ubinadamu wetu una kasoro.

Wanaoshangilia pia wajiulize wao na wanaoamini wameonewa ndipo tukaadhibiwa na miungu hii ya wapenda fedha za bure wanijulishe je mifukoni mwao zitaongezeka?

Tuitetee na tuijenge nchi yetu wenyewe,MUNGU alituumba wakamilifu hatujapungukiwa na chocho,!te walichonacho ngozi nyeupe.
*
 
wamekazana kutamba eti hatutishiki wakae na hela zao. nafananisha tukio hili na baba mwenye familia ambae aliambiwa alime shamba lake kama sharti la kupewa mbolea ya msaada badala ya kulima yeye akaendekeza na uroho wa anasa na uvivu akashndwa kulima lile shamba hivyo kupoteza sifa ya kupewa mbolea ya msaada badala ya kujionea aibu kwa uvivu wake anaanza kujitutumua na kujifanya hana haja na hiyo mbolea huku akijua fika kua hakuna namna hayo mazao yatasitawi bila mbolea pia akijua fika hiyo familia inaingia kuishi maisha magumu si kwa sababu ya ubabe wa mtoa mbolea bali uroho uvivu na uzembe wake ndivyo vinaiingiza familia kwenye dhiki. nadhani ni busara sasa huyu baba avae uhusika aone jinsi gani watoto watakavyoteseka na njaa kwani ni ukweli ulio wazi kua hata huyu baba hatapungukiwa chochote nadhani ndio msingi wa jeuri yake
 
Polepole inaelekea unapotea kwa mwendo wa Polepole. Na kazi liyokabidhiwa inakupozeza na kufuta Ujasiri na umahiri uliokuwa nao ktk uchambuzi wa masuala mbalimbali.

Inasikitisha sana Bwana Polepole kujifanya hamnazo kwa kushabikia kubakwa kwa Demokrasia ktk Taifa Jirani la Zanzibar. Hivi wale Wasimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya waliowapa vyeti vya ushindi Wawakilishi kutoka CUF walioshinda uchaguzi wa Mwezi Octoba 2015 walikuwa Majuha ?.

Leo wakiamua kwenda kutafuta haki yao Mahakama kwa kunyanganywa Uwakilishi wao na ushahidi mkubwa ukiwa ni vyeti vya ushindi, utakuja na hoja kuwa wanatumiwa na watu wa nje ?.

Hapa hakuna haja ya kupepesa macho, ukweli ni kuwa waliokupa kazi ya kupiga Chapuo ujinga wao "Magamba" ndio wanaotaka kutulaza na njaa ya maendeleo huku wakihubiri kauli tata "HAPA KAZI TU".

Kazi zina mahusiano makubwa na Utawala Bora wenye misingi imara ya Demokrasia.
 
Alafu wanajinasibu eti tuna raslimali za kutosha kama madini,gesi,samaki,mbuga za wanyama,bandari,mlima k/njaro n.k mfano mdogo tu, leo unaweza mueleza mwananchi wa kawaida toka tugundue madini yeye kanufaika vipi?au kama Taifa tunanufaika vipi ,Bandari tunayo tumeona hujuma zilizokuwa zinafanyika kuhujumu mapato ya ndani na yote haya yanafanyika chini ya serikali ya CCM,kuhusu mbuga za wanyama nako si haba tunashuhudia wanyama kila leo wakisafirishwa tena kwa baraka za wakubwa toka serikali ya CCM,sababu ndio wako madarakani na madudu mengi ambayo yameibuliwa hivi karibuni yote hayo yamefanyika chini ya utawala wa CCM,angalia mikataba yote mibovu ya raslimali zetu ni serikali ya CCM ndio imeingia na hao wawekezaji linapokuja suala la utaifa kila mtu ni mtaifa mbona haya madudu yote yaliyotekelezwa na serikali ya CCM utaifa ulikaa kando mkabariki raslimali zetu kutwaliwa kwa mikataba ya ovyo ambayo inamuumiza Mwananchi, kwa mfano huu wa IPTL ni mkataba uliopata baraka za serikali ya CCM,wakati wa mfumo wa chama kimoja tuliamini katika Ujamaa na Kujitegemea na kweli tulijitegemea kwa mambo mengi hatuungi mkono taifa kuwa tegemezi kutokana na raslimali tulizonazo, lakini tujiulize waliotufikisha hapa na kuwa omba omba nini akina nani?
 
Nilidhani unasema tuachane na misaada yote kumbe umejitutumua na MCC tu, kama tutaendelea kupokea misaada mingine tutakwepa vipi masharti??????

CCM mmebaka demokrasia Zanzibar halafu mnataka mkinge mikono kupokea misaada ya watu shame on you ccm!!!!!
 
Misaada ya kistaarabu ni ile ambayo haiambatani na masharti. Unafahamu kwanini Baba wa Taifa alielekea China kuomba msaada wa kujenga reli ya TAZARA? Ni kwasababu nchi za magharibi wakati ule zilitoa masharti mengi ikiwemo kutounga mkono jitihada za nchi za Kusini kujipatia uhuru wao!
Unapotaka missada ya kistaarabu nawe fanya ustaarabu kwa wananchi wako. Swali rahisi kwanini wazanzibari wanadhulumiwa chaguo lao kwa mtutu?!
 
Nimekuambia usiseme "watanzania"! Mimi na wengine kama milioni 30 hatuna mawazo kama ya kwako! Semea NAFSI yako na siyo kujumuisha watanzania wengine!
Jaribu kupitia magazeti na vyanzo vya habari uone maoni ya watanzania wenzako kuhusu Jecha na sheria ya makosa ya mitandao
 
Unapotaka missada ya kistaarabu nawe fanya ustaarabu kwa wananchi wako. Swali rahisi kwanini wazanzibari wanadhulumiwa chaguo lao kwa mtutu?!
Haya maneno ya kuweka UWINGI ndiyo yanaleta ukakasi. Nani amekuambia "Wazanzibari wote"? Sema BAADHI yao!
 
Jaribu kupitia magazeti na vyanzo vya habari uone maoni ya watanzania wenzako kuhusu Jecha na sheria ya makosa ya mitandao
Mimi ninachokataa ni kuweka UWINGI kwa kitu kinachofanywa na watu wachache! Kati ya Watanzania milioni 45 ni wangapi wamechangia katika hayo magazeti? Sana sana hawazidi hata laki moja ukijumlisha CUF na UKAWA Bara!
 
Back
Top Bottom