Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Nimejaribu kuwaza na kutafakari haya yanayoendelea sasa katika madhehebu ya kisasa ya kikristo (makanisa ya manabii?) ya kugawa au kuuza visaidizi vya kiimani kama maji, mafuta, chumvi, vitambaa ili waumini wao wabarikiwe na yale yanayoendelea kwenye dhehebu kongwe zaidi la kikristo (kanisa katoliki) ya kugawa au kuuza visaidizi vya kiimani kama maji ya baraka, rosali, picha za kubuni za Yesu, Maria na Yusuph, Misalaba nk. ili waumini wake wapate kubarikiwa.
Nini tofauti yao ya kimsingi ikiwa lengo ni lile lile (waumini wapate baraka kupitia vitu hivyo) pasipo ulazima sana wa kumwamini Yesu mioyoni mwao na kumshika yeye pekee yake ili wapate baraka zake?
Nini tofauti yao ya kimsingi ikiwa lengo ni lile lile (waumini wapate baraka kupitia vitu hivyo) pasipo ulazima sana wa kumwamini Yesu mioyoni mwao na kumshika yeye pekee yake ili wapate baraka zake?