MTAZAMO: Nini tofauti ya vifaa vya upako vya manabii (maji, mafuta, chumvi) na vifaa vya baraka vya kanisa Katoliki (maji, misalaba, rosali, picha)?

MTAZAMO: Nini tofauti ya vifaa vya upako vya manabii (maji, mafuta, chumvi) na vifaa vya baraka vya kanisa Katoliki (maji, misalaba, rosali, picha)?

Wote ni sawa wanachotofautiana ni approach tu.Hawa kwa vile ni watoto wadogo wanaendesha kitoto sana lakini RC wenyewe wanapiga kisirisiri kwa hekima.Hayo maji wanatoa bure lakini wanatoza sadaka na michango kibao ikiwemo huduma za ndoa,komunio,kipaimara na michango ya hijja tegemeza oarokia,tegemeza Jimbo nk.Hizo tasbihi,rozali,vidani,sanamu za Yesu,Bikira Maria,Yusuph,ving'ombe,mbuzi vya mtoto Yesu wa Krismas vyote ni Hela tu.Katoliki ni mama na hao wengine wote ni binti zake.Hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake.Ni kama Marekani inavyojifanya kusimamia demokrasia
Kanisa katoliki halitozi fedha kwa huduma za kiroho. Michango, ni jambo kawaida maana kuna mahitaji mengi ya kibinadamu yanayohitaji fedha.

Zaka na sadaka, ni sehemu ya ibada, hivyo kila mtu anatoa kwa kadiri anavyotaka japo kuna miongozo. Lakina anayeweza kujinywa huduma za kiroho kwa vile hana pesa.

Mapadre wa Katoliki wanabariki maji, matawi au kitu kingine chochote ambacho muumini ataomba, lakini hakuna malipo kwaajili ya huduma hiyo ya kuombea baraka.
 
Manabii na mitume wa sasa hawana tofauti na wachawi na waganga wa kienyeji wanaosaka utajiri kwa kivuli cha kueneza injili ,ukitaka kujua hilo nenda kwenye makanisa au mahema yao kwa siku 14 mfululizo
 
Wakatoliki na hao manabii wanatumia Biblia moja ila Ila wana mitazamo tofauti kabisa!

Kujibu Swali:

Kila kitu ni tofauti, ni jukumu la mlaji kuamua nini kinamfaa:

Comment Binafsi:

Wakatolic - systematic utapeli.
Manabii - Watapeli wa Wazi!

Mafuta ya upako na maji ya baraka zote ni tafsiri zisizo sahihi!

Epuka kutapeliwa, soma Biblia mwenyewe, jaribu kuielewa na mwombe roho Mtakatifu akusaidie!
Kwanza unapotosha Biblia ya kikatiki inavita 73 wakati hao wengine 66. Walikataa vitabu kwa sababu wanaozijua wao. Kumbuka mwanzilishi wa Biblia ni wakatoliki. Hivyo wanapiga kwa sababu wanaozijua wenyewe. Pia Kuna baadhi ya Aya zimebadilishwa au kufutwa au kuongezea kwenye biblia zao. Hivyo hawafanani.

Pili kuhusu maji, mafuta, msalaba picha n.k.

Moja maji kanisa Katoliki hayauzwi hata mara Moja na kazi yake ni kutakasa. Pale unapohisi hapako salama unasali na kupatakasa kwa maji.

Mafuta katika kanisa nayo hayauzwi na kazi yake ni kuponya au kuweka wakfu na yanatofautiana ya wakfu na ni kasisi au aliyeteukiwa humpaka anayewekwa wakfu au anayehitaji mpako wa wagonjwa au sakramenti husika. Wao wanauza mafuta yao haijulikani hasa ni uponyaji, kutakasa, wakfu(hawana), lakini pia unaweza kujipaka kama Rays/YU/ au Vaseline TU. Kitu ambacho sicho kwenye ukatoliki.

Kanisa Katoliki haliuzi Rozari, picha, msalaba Bali wao wanavibariki TU ili mtumiaji atumie kukiwa kimetakaswa. Wanauza vitu hivyo ni watengenezaji ambao wanaweza kuwa waamini, vyama vya kitume, au mradi wa parokia. Ukinunua bila kubarikiwa hicho ni kifaa kama vifaa vingine vikashatakaswa au kubarikiwa ndio vinakuwa visakrament. Kumbuka kubariki nako ni Bure. Na matumizi ya vifaa hivi sio kama uganga, Bali ni nyenzo TU ya kukusaidia katika Sala na maombi na uchaji wa Mungu. Ila upande ule ni kama hirizi, ukiweka aukivaa au nyunyizia mapepo... (Sitaki kutoa hukumu).

Mwisho ili kuwa kuhani/Padre au Askofu lazima upitie mafunzo mbalimbali na upakwe mafuta wekwa wakfu. Lakini upande ule unaanza stand ya bus, baadae inakuwa saidia nanihii kesho kutwa unafungua kanisa. Tumeishia kuona wadada wakiombwa wapeleke chupi, sidiria zipate upako, watu wanauziwa maji, mafuta ili wapate upako, tumeona wengine waogeshwa madhabahuni, wangine wakikanyagwa na mchaungaji wao eti, wengine wakilipishwa fedha nyingi kumwona na kuombewa (kiboko ya wachawi), wengine kukaa vitu vya mbele unalipia.

Kanisa Katoliki unaweza kukaa popote isipokuwa sehemu ya kwaya na sehemu ya masista TU na kule altareni. Waamini wote ni sawa hata ingekuwa na cheo Gani. Kule kwengine hapako hivyo.

In short, wale wengi wameiga mambo mengi kutoka kanisa Katoliki lakini kwao wameyafanya kama washirikina na kuifanya uinjilishaji kama biashara.
 
Wote ni sawa wanachotofautiana ni approach tu.Hawa kwa vile ni watoto wadogo wanaendesha kitoto sana lakini RC wenyewe wanapiga kisirisiri kwa hekima.Hayo maji wanatoa bure lakini wanatoza sadaka na michango kibao ikiwemo huduma za ndoa,komunio,kipaimara na michango ya hijja tegemeza oarokia,tegemeza Jimbo nk.Hizo tasbihi,rozali,vidani,sanamu za Yesu,Bikira Maria,Yusuph,ving'ombe,mbuzi vya mtoto Yesu wa Krismas vyote ni Hela tu.Katoliki ni mama na hao wengine wote ni binti zake.Hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake.Ni kama Marekani inavyojifanya kusimamia demokrasia kwenye nchi zingine.
Unachokosea ni kitu kimoja kanisa katoliki halina kiwanda kutengeneza hivyo ulivyosema wanaotengeneza ni wajasiriamali, which is fine. Kanisa linavibariki TU.

Kuhusu sadaka, kanisa ni taasisi inahitaji kujiendesha kwa michango ya hiari ambayo ndio sadaka. Sasa sadaka hizi zipo katika makundi mawili

Sadaka zinazoelekzwa na kitabu kitakatifu yaani Biblia Zaka, malimbuko, na sadaka zingine.

Michango ya maendeleo: Tegemeza/mavuno, michango ya ujenzi wa kanisa, parokia Jimbo n.k

Michango ya hija ni kama unavyosafiri kwenda mahali zile gharama za usafiri, malazi, chakula, usafi wa Mahalia, maandalizi mbalimbali n.k infact hizi huchangwa na kutumika zote kwa walengwa na sio chanzo Cha mapato.

Lakini kanisa linatoka elimu mbalimbali kupitia taasisi za elimu awali mpaka Chuo kikuu, huduma za afya, vituo vya kulea yatima na wasiojiweza, n.k vyote hivyo vinatokana na sadaka, majitoleo binafsi, michango n.k kutoka KWA waamini.

Je hao wenzetu wanafanya nini? Tunasikia TU waamini wao wamepokea au wameokota magari na nyumba
 
  • Usijitengenezee sanamu ya kuchongwa au mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni au kilicho chini duniani au kilicho ndani ya maji chini ya dunia. Usiviinamie wala kushawishiwa kuviabudu, kwa sababu mimi, Yehova Mungu wako, ni Mungu ninayetaka watu waniabudu mimi peke yangu.”—Kutoka 20:4, 5. a
  • “Sanamu zao ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya mwanadamu. Zina kinywa, lakini haziwezi kuongea; zina macho, lakini haziwezi kuona; zina masikio, lakini haziwezi kusikia; zina pua, lakini haziwezi kunusa; zina mikono, lakini haziwezi kugusa; zina miguu, lakini haziwezi kutembea; hazitoi sauti yoyote kwa koo zake. Watu wanaozitengeneza watakuwa kama sanamu hizo, na pia wote wanaozitumaini.”—Zaburi 115:4-8.
  • “Mimi ni Yehova. Hilo ndilo jina langu; sishiriki utukufu wangu na yeyote, wala kuzipa sanamu za kuchongwa sifa yangu.”—Isaya 42:8, maelezo ya chini.
  • “Ikimbieni ibada ya sanamu.”—1 Wakorintho 10:14.
  • “Jiepusheni na sanamu.”—1 Yohana 5:21.
Wanasoma Bibilia kila siku lakini wamejaza Masanamu kila mahali🙄🙄🙄
 
Wakatoliki na hao manabii wanatumia Biblia moja ila Ila wana mitazamo tofauti kabisa!

Kujibu Swali:

Kila kitu ni tofauti, ni jukumu la mlaji kuamua nini kinamfaa:

Comment Binafsi:

Wakatolic - systematic utapeli.
Manabii - Watapeli wa Wazi!

Mafuta ya upako na maji ya baraka zote ni tafsiri zisizo sahihi!

Epuka kutapeliwa, soma Biblia mwenyewe, jaribu kuielewa na mwombe roho Mtakatifu akusaidie!
Maji ya baraka kwenye makanisa ya Wakatoliki hutolewa BURE. Ningependa kujua Wakatoliki wanatapeli vipi na wamemtapeli nani? Jibu bila jazba.
 
Maji ya baraka kwenye makanisa ya Wakatoliki hutolewa BURE. Ningependa kujua Wakatoliki wanatapeli vipi na wamemtapeli nani? Jibu bila jazba.

Nikisema systematic utapeli uelewe ndani ya neno systematic kuna nini!!!!! Na maji ya Baraka sio only interaction unayokuwa nayo na wakatoliki
 
Kwenye Imani viliitwa vishikiza Imani na Lilikua ni neno la mara Moja sio kuirudia rudua kwa mfano ilikua mtu unaambiwa shika maji yanaombewa anapewa mwenye tatizo Fulani, au mafuta yaliyopo yanabarikiwa anapakwa mtu. Au nguo iliyopo hapo inabarikiwa anaenda kuwekewa mtu ni neno la Imani linalotoka mara Moja tu .Ndio maana ukiona katika habari za Yesu Kuna muda alitengeneza tope kwa mate kisha akampaka mtu akapona lakini huoni Yesu au yule mtu aliendelea kutembea na Yale mate. Tukirudi kwa Hawa manabii sijui haya mafundisho na hizi biashara wameyatoa wapi na watu wanapelekwa wapi😂😂
uko sahihi
 
Mtoto anaiga kwa mama. Hao wote ni watoto na wajukuu wanaoeneza kazi za mama yao.
Yesu anasisitiza watu wa amini Neno pekee linauwezo mkubwa kuliko vifaa.

Yesu alimwambia mzungu mwanajeshi ndiye mwenye imqni kuliko israel wote pale alipomwambia Yesu "sema neno" kule mgonjwa atapona. Neno lina nguvu kuliko vifaa tiba vya na miungu ya kiroho.

Kwamba msingi wa hoja ni imani siyo?

Hudhani ni upunguani kuzozana, kujishasha au hata mtu kudhani imani yake ndiyo iliyo bora zaidi kuliko za wengine?
 
Kwamba msingi wa hoja ni imani siyo?

Hudhani ni upunguani kuzozana, kujishasha au hata mtu kudhani imani yake ndiyo iliyo bora zaidi kuliko za wengine?
Ubora wa imani unapimwa na compliance na neno sio imani waliyokubalianq kikundi flani.
 
Ubora wa imani unapimwa na compliance na neno sio imani waliyokubalianq kikundi flani.

Tatizo ni kuwa kila mmmoja yuko na aliposhikilia kutoka kwenye neno hilo hilo.

Bila shaka vitakavyowaokoa watu siyo nitty gritty za compliance bali vitokavyo mioyoni mwao.
 
Tatizo ni kuwa kila mmmoja yuko na aliposhikilia kutoka kwenye neno hilo hilo.

Bila shaka vitakavyowaokoa watu siyo nitty gritty za compliance bali vitokavyo mioyoni mwao.
Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Yeremea 17:9,10
 
Nimejaribu kuwaza na kutafakari haya yanayoendelea sasa katika madhehebu ya kisasa ya kikristo (makanisa ya manabii?) ya kugawa au kuuza visaidizi vya kiimani kama maji, mafuta, chumvi, vitambaa ili waumini wao wabarikiwe na yale yanayoendelea kwenye dhehebu kongwe zaidi la kikristo (kanisa katoliki) ya kugawa au kuuza visaidizi vya kiimani kama maji ya baraka, rosali, picha za kubuni za Yesu, Maria na Yusuph, Misalaba nk. ili waumini wake wapate kubarikiwa.

Nini tofauti yao ya kimsingi ikiwa lengo ni lile lile (waumini wapate baraka kupitia vitu hivyo) pasipo ulazima sana wa kumwamini Yesu mioyoni mwao na kumshika yeye pekee yake ili wapate baraka zake?
Dini ni aina ya ushirikina na zote zimejengwa katika misingi ya woga na ujinga
 
Kanisa Katoliki lina maji ya baraka tu na ambayo hutolewa bure Kanisani baadavya kuombewa na Padre. Rozali na misalaba kwenye Kanisa, navyo ni vitu viwili tofauti.
Vyote hivyo ni visaidizi vya imani na vinauzwa kanisa linaingiza pesa kwa kuviuza
Sacramenti zenyewe ni biashara kubwa kanisa hununua huko huko ndani ya kanisa kwa sadaka za waumini kitengo cha kupika Sacramenti cha masista na kugawia waumini na hiyo biashara ya kupika na kuuza Sacramenti hailipiwi kodi TRA
 
Vyote hivyo ni visaidizi vya imani na vinauzwa kanisa linaingiza pesa kwa kuviuza
Sacramenti zenyewe ni biashara kubwa kanisa hununua huko huko ndani ya kanisa kwa sadaka za waumini kitengo cha kupika Sacramenti cha masista na kugawia waumini na hiyo biashara ya kupika na kuuza Sacramenti hailipiwi kodi TRA
Kweli usilolijua, ni sawa tu na usiku wa giza.
 
Kwanza sahihisha, hakuna kanisa katoliki linalouza maji.

Kwa wakatoliki, maji, msalaba, rozari, picha, havina kitu chochote kwa asili yake kama vilivyo.

Vitu hivyo hupewa thamani baada ya ibada maalum au sala fupi ya mtu inayofanywa na aliyewekwa wakfu (padre, askofu, kadinali, papa). Na hakuna malipo hata ya shilingi moja. Maji kwa kuwa yanachotwa bure, yakishabarikiwa, mtu yeyote huweza kuyachukua bila ya malipo yoyote. Rozari, msalaba, matawi, nyumba yako, gari lako, pikipiki yako, au kitu kingine chochote unachotaka kibarikiwe, wewe unayetaka kibarikiwe, unajua jinsi ulivyokipata, kama umenunua, umepewa bure au umetengeneza mwenyewe, hilo halimhusu kasisi wa kanisa. Lakini yeye atafanya ibada ya kunariki bure.
Misalaba, rozari, picha… vinatolewa bila malipo? Unafahamu idadi na kiasi cha michango wanayochangishwa waumini wakatoliki kupitia kinachoitwa jumuiya ndogo ndogo za kikristu (JNNK)?
 
Back
Top Bottom