Mtazamo: Taasisi na mashirika ya Serikali ambayo yana huduma mbovu kwa wateja Tanzania

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Huu ni mtazamo wangu kutokana na uzoefu wangu wa kupitia huduma mbali mbali katika mashirika hayo kwangu naona Hawa WATANO Wafuatao kwao mteja ni "boya" na Wala sio mfalme
5. TRA
4. Polisi
3. Maji
2. Nida
1. Tanesco

Kama umewahi kwenda ofisi hizo hapo juu utaona jinsi unavyopokelewa mpaka kuhudumiwa mpaka unajisemea moyoni..
'kungekuwa na mbadala ningeenda"

Anyway ni mtazamo tu..
Naomba kote mpinge ila sio hapo kwa Tanesco🤣🤣
 
Wanaweka contacts na address kwenye page zao. Jaribu sasa kuwafikia au kuwatafuta, hapo ndio utaona maajabu ya ulimwengu!

*Simu haipokelewi hata upige kutwa mzima! Pale kuna ma-secretary (customer care/service), vi-bibi
havielewi chochote kuhusu umuhimu wa mteja.

Email zenye domain za shirika haziendi. Utaletewa meseji'
'Your message wasn't delivered because the address couldn't be found, or unable to receive mail.'

*Barua hazijibiwi

*Ukienda ofisini hawatojali.
 
TANESCO hawa ni wapuuzi kinoma.....na wenzao polisi
 
Utumishi wa serikalini ungeekua na target au ajira zote za serikali zingekua na mikataba ya muda (lets say 3 years) huku wakiangalia nini ume deliver, nadhani tungekua mbali sana.

Watumishi wa umma wamejisahau sana kutokana na ajira zao kua permanent, na hata wakikosea kwenye ajira zao wanahamishwa tu eneo la kazi.
 
Msisahau EWURA au iwe ujafanya nao kazi, wapuuzi sijapata kuona hapa duniani.
 
Huu ni mtazamo wangu kutokana na uzoefu wangu wa kupitia huduma mbali mbali katika mashirika hayo kwangu naona Hawa WATANO Wafuatao kwao mteja ni "boya" na Wala sio mfalme
5. TRA
4. Polisi
3. Maji
2. Nida
1. Tanesco

Kama umewahi kwenda ofisi hizo hapo juu utaona jinsi unavyopokelewa mpaka kuhudumiwa mpaka unajisemea moyoni..
'kungekuwa na mbadala ningeenda"

Anyway ni mtazamo tu..
Naomba kote mpinge ila sio hapo kwa Tanesco[emoji1787][emoji1787]
TANESCO ya sasa sio ya zamani na ya kesho inaonesha dira ya mabadiliko makubwa sana kwenye utoaji wa huduma, tunakuhakikishia kuwa kwa huduma zetu zimeboreshwa sana na wateja wamekuwa wakionesha hilo.

Hebu twende kwa data au taarifa kamili ya wapi unapendekeza paboreshwe zaidi ili ufurahie huduma zetu
 
Wanaweka contacts na address kwenye page zao. Jaribu sasa kuwafikia au kuwatafuta, hapo ndio utaona maajabu ya ulimwengu!

*Simu haipokelewi hata upige kutwa mzima! Pale kuna ma-secretary (customer care/service), vi-bibi
havielewi chochote kuhusu umuhimu wa mteja.

Email zenye domain za shirika haziendi. Utaletewa meseji'
'Your message wasn't delivered because the address couldn't be found, or unable to receive mail.'

*Barua hazijibiwi

*Ukienda ofisini hawatojali.
Tupo kukuhudumia
 
Tafadhali shauri ni nini kiboreshwe zaidi ufurahie huduma zetu

Suala kubwa ni kubadili mentality ya watoa huduma wetu, waone kuwa tunahitajiana wote. Si kuwa shirika halina shida bali wateja ndo wanaohitaji shirika zaidi.

Kama ulivyojitokeza na kutoa majibu hapa, inaonyesha utayari wa kutoa huduma kwa mteja. Hongera kwako.

Pamoja na matatizo yetu ya kutojitosheleza kwa mahitaji kutoka kwenye shirika, kutoa jibu mwafaka kwa wakati bila kona kona/njoo kesho/ nenda kwa huyu naye anakurudisha pale au maelezo halisia ni muhimu kwa mhitaji.
 
Suala kubwa ni kubadili mentality ya watoa huduma wetu, waone kuwa tunahitajiana wote. Si kuwa shirika halina shida bali wateja ndo wanaohitaji shirika zaidi.

Kama ulivyojitokeza na kutoa majibu hapa, inaonyesha utayari wa kutoa huduma kwa mteja. Hongera kwako.

Pamoja na matatizo yetu ya kutojitosheleza kwa mahitaji kutoka kwenye shirika, kutoa jibu mwafaka kwa wakati bila kona kona au maelezo halisia ni muhimu kwa mhitaji.
Je ulijibiwa ambavyo haujaridhika ofisi gani? Nani alikujibu na alikujibuje? Tafadhali tupatie namba yako ya simu na siku uliyojibiwa tufatilie
 
Back
Top Bottom