Mtazamo: Taasisi na mashirika ya Serikali ambayo yana huduma mbovu kwa wateja Tanzania

Mtazamo: Taasisi na mashirika ya Serikali ambayo yana huduma mbovu kwa wateja Tanzania

Tanesco wamenitoa kwenye huduma ya umeme wa bei rahisi bila sababu. Kwa hilo tu sitawasamehe kamwe
 
Je ulijibiwa ambavyo haujaridhika ofisi gani? Nani alikujibu na alikujibuje? Tafadhali tupatie namba yako ya simu na siku uliyojibiwa tufatilie

Hata akimtaja hakuna hatua itakayo chukuliwa….mnabebana sana kuogopa kulaumiana….mm yalinikuta 2019 na sio mm tu karibia mtaa mzima lkn cha ajabu mkamsimamisha tu kazi wakati ameniingiza hasara ya kulipa faini,kuanza upya maombi,kulala giza mwezi mzima nk
 
Shida nyingine
1. Kumekuwa na muingiliano kati ya walinzi wa mataasisi na maafisa wa ofisi husika za serikali.
Walinzi wa makampuni na Suma Jkt wamekuwa wakiacha majukumu yao ya ulinzi na kuanza kufanya kazi za huduma za mataasisi wanayoyalinda huku hawana misingi ya elimu ya huduma hizo.
2. Maafisa wa mataasisi kujiona wafalme humfikii hadi uanike shida yako kwa sekretari au mlinzi mlangoni hii inaondoa mantiki ya kuwa taasisi za umma.
 
Wanaweka contacts na address kwenye page zao. Jaribu sasa kuwafikia au kuwatafuta, hapo ndio utaona maajabu ya ulimwengu!

*Simu haipokelewi hata upige kutwa mzima! Pale kuna ma-secretary (customer care/service), vi-bibi
havielewi chochote kuhusu umuhimu wa mteja.


Email zenye domain za shirika haziendi. Utaletewa meseji'
'Your message wasn't delivered because the address couldn't be found, or unable to receive mail.'

*Barua hazijibiwi

*Ukienda ofisini hawatojali.
Huwa nashindwa kabisa kujua kuwa wanaweka namba za nini.

Sijui ni Ushamba au Uzembe tu.

Tanzania Sucks.
 
Tunamaanisha TANESCO tupo vizuri na kama unachangamoto yeyote tafadhali ilete tusaidiane kuitatua, TANESCO ni yenu, ni mali ya uma mnawajibu wa msingi wa kuisaidia kuwahudumia vema kwa kutoa taarifa sahihi, ushauri nk
Hebu jibu hili swali kinagaubaga bila maneno mengi :

''Ni kwanini umeme unakatika kila mara maeneo mengi ya nchi hata sasahivi? ''
 
Back
Top Bottom