Mtazamo: Taasisi na mashirika ya Serikali ambayo yana huduma mbovu kwa wateja Tanzania

Mods njooni Tanesco wamevamia humu
 
TANESCO ya sasa sio ya zamani na ya kesho inaonesha dira ya mabadiliko makubwa sana kwenye utoaji wa huduma, tunakuhakikishia kuwa kwa huduma zetu zimeboreshwa sana na wateja wamekuwa wakionesha hilo.

Hebu twende kwa data au taarifa kamili ya wapi unapendekeza paboreshwe zaidi ili ufurahie huduma zetu
Bwana TANESCO hii ni siasa unaleta
Kukatika umeme hovyo ndiyo maboresho?
Inachukua mda gani toka kulipia mpaka kuunganishiwa umeme?
 
Huu ni mtazamo wangu kutokana na uzoefu wangu wa kupitia huduma mbali mbali katika mashirika hayo kwangu naona Hawa WATANO Wafuatao kwao mteja ni "boya" na Wala sio mfalme
5. TRA
4. Polisi
3. Maji
2. Nida
1. Tanesco

Kama umewahi kwenda ofisi hizo hapo juu utaona jinsi unavyopokelewa mpaka kuhudumiwa mpaka unajisemea moyoni..
'kungekuwa na mbadala ningeenda"

Anyway ni mtazamo tu..
Naomba kote mpinge ila sio hapo kwa Tanesco🤣🤣
  1. NEMC wameshindwa kudhibiti kelele chafuzi na mitetemo wakisingizia hawana askari wa kuwakamata wahusika
  2. TBS wameshindwa kudhibiti bidhaa fake madukani
  3. LATRA wameshindwa kudhibiti nauli holela kwenye mabasi
  4. PCCB wameshindwa kabisa kuwakamata traffic polisi wanaokula rushwa waziwazi barabarani, raia wanaona PCCB hawaoni
 
TANESCO ya sasa sio ya zamani na ya kesho inaonesha dira ya mabadiliko makubwa sana kwenye utoaji wa huduma, tunakuhakikishia kuwa kwa huduma zetu zimeboreshwa sana na wateja wamekuwa wakionesha hilo.

Hebu twende kwa data au taarifa kamili ya wapi unapendekeza paboreshwe zaidi ili ufurahie huduma zetu
Namba zenu za huduma kwa wateja pamoja na emergency mmehakikisha zinafanyakazi zote? Nyingi ya namba hizo ni unreachable
 
Tafadhali tujulishe ni namba ipi unaikosa, tunakusihi kutumia namba 0748550000
 
Kwa mkoa gani

Kuna orodha ndefu ya namba za Regional Managers mlitoa, hiyo ndiyo watanzania wengi wanaifuata na wanakosa huduma kwakuwa namba hizo nyinhi dead
 
Tafadhali tumia hii tutakuhudumia
 
Asilimia kubwa huwa ni vidada na ukichunguza kama ni mwanaume ni waliokuja mjini wakubwa.
Nadra Sana kukuta police aliyezaliwa na kukulia mjini akawa mnoko.
 
Halafu vingi vina sura za chuma cha pua
 
TANESCO ya sasa sio ya zamani na ya kesho inaonesha dira ya mabadiliko makubwa sana kwenye utoaji wa huduma, tunakuhakikishia kuwa kwa huduma zetu zimeboreshwa sana na wateja wamekuwa wakionesha hilo.

Hebu twende kwa data au taarifa kamili ya wapi unapendekeza paboreshwe zaidi ili ufurahie huduma zetu
Ni uongo. Watu wa Kibaha, eneo la Pangani tulileta maombi ya umeme tokea mwaka jana mpaka sasa hatujapewa huduma. Miezi mingi imepita tunaendelea kutumia vibatari. Tanesco ni jipu hapa nchini. Wananchi wanawalalamikia lakini hamtaki kujirekebisha. Mmeweka pamba masikioni. Mnaendelea kufanya kazi kwa mazoea
 
hivi wale wanao toa hati za kusafiria maarufu kama (PASSPORT) [emoji118](English) hivi wale ni shirika,idara au kitengo katika wizara ya mambo ya ndani? wale nao wanazingua sana maswali ni mengi sana [emoji22] ikitokea umeenda kuomba PASSPORT wakati ni haki ya mwananchi ile.Ndio maana Tz tunaambiwaga sisi ni woga hatutoki nje kutafuta miaka yote tupo home tu kumbe watu wanaghairi sababu upatikanaji wa vielelezo kama hivyo ni mtihani. [emoji706]
 
6
Huu ni mtazamo wangu kutokana na uzoefu wangu wa kupitia huduma mbali mbali katika mashirika hayo kwangu naona Hawa WATANO Wafuatao kwao mteja ni "boya" na Wala sio mfalme
5. TRA
4. Polisi
3. Maji
2. Nida
1. Tanesco

Kama umewahi kwenda ofisi hizo hapo juu utaona jinsi unavyopokelewa mpaka kuhudumiwa mpaka unajisemea moyoni..
'kungekuwa na mbadala ningeenda"

Anyway ni mtazamo tu..
Naomba kote mpinge ila sio hapo kwa Tanesco🤣🤣
6. Rita
7. Uhamiaji
 
Sina maslahi na TANESCO ila wameanza jielewa...
Nchi yetu huduma kwa wateja ni mbovu sana, hatujafundishwa kumjali mteja, haya mashirika na hizi taasisi zinasumbuka sababu waajiriwa wake wana mikataba ya kudumu, kifo ndio humuondoa mtu kazini.

Serikali inapaswa badilika
 
Back
Top Bottom