1. Unaweza ukapata emergence Tanesco, mfano meter imezingua, umeme kuwaka na kuzima kutokana na nyaya flan hivi kutokaza ktk waya unaoingiza umeme sehemu ya nyumba. Unaenda kutoa taarifa saa 2 asubuh, ila Tanesco wanakuja usiku, tena hapo unakuwa unapiga simu kweli kweli, unapiga kila baada ya lisaa limoja. Imenikuta saana hii.
2. Unalipia umeme leo, anakuja jirani yako analipia umeme miezi minne mbele au hata mwaka, cha ajabu umeme anaanza kupata yeye kabla yako wewe, na hii michezo mnacheza sn, jina la mtu ktk mita flan anaenda kupewa mwingine (Hii nmeshuhudia mwenyewe) mtu alitoa laki nzima akafanyiwa huu mpango, nna jina la huyo mtu mpaka Staff aliyefanya hiyo kaz, huyo staff na namba zake ninazo.
3. Nikupe hongera kwa kujitokeza kujibu hapa JF changamoto za wadau, ila kuna mda unaonekana boya kwa kutetea upuuzi, eti unamwambia mda ataje kituo na majibu aliyopewa, unauliza hivi kwani hizi changamoto ni ngeni kwenu au? Kukubali makosa ni ujinga? Kwani ukisema tu kuwa hili tatizo lipo na tunaomba radhi kwa yanayotokea lakini punde tutatatua changamoto hii, unapungukiwa nini? Usiwe boyaboya broh. Watu tunalala Dar bila fen kisa upuuzi wenu Tanesco, tunatoa malalamiko lakini hamjali, tunakuja kusema hapa mnajifanya kujitetea.