Mtazamo wa vijana wa Afrika kuhusu China waendelea kuboreka

Mtazamo wa vijana wa Afrika kuhusu China waendelea kuboreka

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111255268459.jpg
Elias Gebreselassie alilelewa Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, na kama wenzake, amekuwa na fikra kuwa kwamba majengo marefu, maduka makubwa na barabara kuu zinaweza kuwa maonyesho tu katika sinema za Hollywood.

Lakini katika kipindi cha muongo mmoja uliopita Gebreselassie amejionea kwa hakika mji wa Addis Ababa ukibadilika kwa muonekano na kwa miundo mbinu.

Bila shaka sio sinema tena lakini ni ukuaji unaowezeshwa na ushirikiano wa China na Ethiopia katika sekta ya uwekezaji .

Na sasa Gebreselassie mwenye umri wa miaka 34 anasifu uwekezaji wa China katika miundombinu ya kisasa kama vile barabara na vituo vya kijamii, ambayo ilifanya mji mkuu kuwa jiji kuu la kimataifa linalopendeza na makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Yeye ni mfano wa jinsi watu wa Afrika na hasa vijana wanavyoendelea kubadili mitazamo yao kuhusu China.

Gebreselassie anasema ufahamu wake kuhusu China umeongezeka sana baada ya kushuhudia mchango wake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Afrika kupitia ujenzi wa maeneo ya viwanda, majumba makubwa ya biashara na reli za umeme.

“Hii imewahamasisha vijana wa Ethiopia kufahamu zaidi kuhusu China na watu wa China. Vijana wengi, kama vile wadogo zangu sasa wamechagua kusoma nchini China, na wengine wengi wanapendelea kwenda vyuo vikuu vya Ethiopia kusoma Kichina kupitia Taasisi za Confucius, "Gebreselassie anasema.

Anasema kuwa sinema za Kung Fu alizokuwa amezitazama akiwa mtoto zilimpa ufahamu wa utamaduni wa Wachina. Lakini pia anasema uelewa wake umejikuza zaidi kupitia uwezo wa kiteknolojia wa China na maendeleo ya haraka ya kiuchumi.

"Hivi karibuni, idadi inayoongezeka ya vijana wa Ethiopia pia wamepata uelewa mpana kuhusu China na mtindo wa maisha wa Wachina kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii kama TikTok pamoja na sinema za jadi,", anasema Worku, kijana mwingine wa Ethiopia.

Maoni ya vijana hawa wa Ethiopia ni sawa na wengine wengi kote barani Afrika.

William Douglas, kijana Mtanzania mwenye umri wa miaka 21, anasema kuwa vifaa vya nyumbani, vifaa vya ujenzi na mashine zinazotengenezwa nchini China ni maarufu miongoni mwa wateja nchini humo sababu ya ubora na bei nafuu.

"Hapa Tanzania, chapa za simu kama vile Huawei na Oppo ni maarufu sana," anasema Douglas.

"Tunatazama sinema nyingi za China," Anasema Nurdin, mwenye umri wa miaka 25, na kuongeza kuwa ufahamu wake wa utamaduni wa China umekua mwaka hadi mwaka kutokana na mabadilishano ya watu kwa watu.

Naye Ibrahima Diao, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop cha Dakar nchini Senegal, anaamini kuwa vijana wa Senegal sasa wanajua mengi zaidi kuhusu utamaduni wa Wachina kuliko walivyokuwa miaka michache iliyopita, akibainisha kuwa nchi hizi mbili zimekuza ushirikiano thabiti.

Vijana wa Kiafrika wamechangia pakubwa katika uhusiano wa kitamaduni na kiuchumi kati ya Afrika na China, kupitia kujifunza lugha ya Kichina na mabadilishao mengine ya kitamaduni na kiteknolojia.

"Vijana wa Afrika hakika wanaendelea kuwa na kiu ya kufahamu China na kushirikiana nayo tofauti na hapo awali. Wanavutiwa sana na maendeleo ya miundombinu yalioletwa na China katika nchi nyingi za Kiafrika, ” anasema Ndiye Kidet, mwanafunzi wa elektroniki katika Chuo cha Uhasibu cha Botswana.

Kidet alisema kuwa vijana wa Kiafrika wamepuuza hadithi za uwongo kwamba fadhili za China kwa Afrika ni zenye nia mbaya, na kuongeza kuwa China imethibitisha kuwa mshirika wa kuaminika katika harakati za Afrika za kujitegemea.

Utafiti uliofanywa huko Gaborone, Botswana mapema mwaka huu ulionyesha kuwa vijana wa nchi hiyo walithamini ushirikiano na misaada ya China kwa Afrika, kwani inasaidia sekta za kilimo, sanaa, michezo na utengenezaji.

Clifford Mboya, mtafiti wa Kenya aliyesomea siasa za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Fudan mjini Shanghai, China anasema kuwa maisha yake nchini China yalikuwa ya kipekee kwa njia nyingi.

Anasema licha ya kuwa nchi hiyo ina changamoto zake kama nchi nyingine yoyote duniani lakini pia kuishi huko kulimsaidia kupanua mawazo yake katika maswala mengi.

“Nadhani ni nchi ambayo imejikita katika kufikia malengo yake. Ninapenda jinsi wanavyofuatilia ndoto zao na miradi yao na kuifanikisha", anasema Mboya.

Mboya anasema kuwa ripoti nyingi kwenye vyombo vya habari kuhusu China zilikuwa hasi kabla ya kwenda nchini humo.

"Lakini, ilivutiwa na kile nilichokiona, kwa sababu hakuna tofauti yoyote na hapa, ni kwamba tu wana mfumo wao wa kisiasa, maadili ya kazi yao na utamaduni ni tofauti. Lakini mara tu unapoelewa jinsi mifumo inavyofanya kazi huko, unaanza kuthamini utamaduni wao na njia yao ya kufanya mambo.”anaongeza.
 
Fucking propaganda

Long term goal ya macho madogos ni kucolonize the entire african continent.
 
Mkoloni mpya wa Afrika ni CHINA,Wazambia now ndiyo wanatia huruma Sana!!
 
China sio na hajawahi kuwa rafiki wa Africa na hatakuja kuwa..!!! Anachoangalia ni maslahi yake tuu

Hii siyo china ya Mao.mchina kagundua wazungu miaka hiyo walifanikiwa kwa kupitia africa kwa ukoloni na yeye kaja na style yake ainue uchumi wake awe super power kupitia africa.
 
Hii siyo china ya Mao.mchina kagundua wazungu miaka hiyo walifanikiwa kwa kupitia africa kwa ukoloni na yeye kaja na style yake ainue uchumi wake awe super power kupitia africa.
Sahihi [emoji817][emoji736]
 
China sio na hajawahi kuwa rafiki wa Africa na hatakuja kuwa..!!! Anachoangalia ni maslahi yake tuu

kiuhalisia mambo ya undugu tunaendekeza sisi tulioathiriwa na ujamaa, wenzetu wanaangalia maslahi tu. Sio majirani hadi nchi za east ama west, wote wanaangalia interest za kizazi chao na huwezi walaumu kwa hilo
 
China sio na hajawahi kuwa rafiki wa Africa na hatakuja kuwa..!!! Anachoangalia ni maslahi yake tuu
Muulize hiyo Ethiopia wananchi wake wana hali gani kiuchumi?Wanakimbia nchi Kama wakimbizi wa Vita.
Reli, barabara,mandege sio tafsiri ya maendelo.

Mchina ni mhuni tu, hawezi kukupa ndoano uvue mwenyewe, atakupa Samaki ili uwe mteja wake wa kudumu.
 
Mchina ni mhuni tu kama wahuni wengine..

Africa tuache kupendapenda vya bure...
 
Back
Top Bottom