Kwa mfano , jiulize, yule mzee walishindwa kumtengeneza ajali, kumpa sumu, n.k?Kulikuwa na ulazima wa kumteka kwa style ile tena huku kelele za watu kutekwa na kupotezwa zikiwa zimepamba moto?
Kwa nini isiwe kwa lengo la "kuogopesha raia, kuwatia woga ili yeye na kundi lake waendelee kufanya wanavyo taka bila ya kupingwa?
Toka mwanzo ni huyu huyu kahimiza matumizi ya "lugha ya staha". Hana uvumilivu wa kusikia lugha ngumu ikielekezwa kwake na kwa serikali yake.
Kwa hiyo, nadharia yako inaanza kuharibikia hapa.
We. endelea kuwaaminii hao watu ila kumbuka walitaka hiyo nafasi usipate sema tu yule Mkuu wa Wajeda wa wakati ule ndio alikuokoa. Hata kama umeweka watu wako hizo sehemu nyeti, usidhani ndio uko salama hasa ukizingatia umetoka upande wa pili wa hii nchi na zaid jinsia yako ni tatizo lingine.
Huu nao ni upotezaji lengo wa maksudi kabisa.
Huyu huyu ameteua wakuu wote wa vitengo vinavyo husika na kuhakikisha usalama wa raia upo; au wanaoweza kutumia nafasi hiyo kufanya anavyotaka yeye vyombo hivyo vifanye.
Kiongozi anaye ona usalama wa raia wake unatiwa doa na akakana mbele ya vyombo vya habari kwa kuyaita maswala hayo kuwa ni "DRAMA", kwako bado haikupi sababu ya kujuwa kwamba huyu kiongozi anao utashi wa kuamua kuzuia au kuruhusu yanayo endelea?
Hao watu/kundi hilo linalo mhujumu huko ndani ya CCM litakuwa na watu wa aina gani ambao Mwenyekiti wa Chama kamwe hawezi kulishughulikia? Tutajie hata mmoja tu kati ya watu hao ndani ya hiyo CCM anayo iongoza Samia sasa hivi.
Wajumbe wa Kammati Kuu ya chama, wote wanajulikana. Tueleze wewe, hili kundi linafanya kazi zake za kumhujumu Samia likiwa wapi?
Toa mfano, angalao mmoja tu, hata kama siyo kwa kutaja majina, uonyeshe kuunga hoja mkono wa nadharia yako hii! Mbona huyo huyo Samia mwenyewe kafanya juhudi kubwa za kuwasambaratisha hata hao ambao wangedhaniwa kuwa mahasimu wake; akina Makonda..., nani mwingine? Ally Bashiru? Atafanya nini huyu nje ya CCM inayo ongozwa na Samia mwenyewe!
Akina Lukuvi, Kalamaganda na wengineo, si ndio hao unawaona wanachezewa akili kama watoto wadogo na huyo huyo Samia?
Hakuna kundi lolote linalo fanya hujuma dhidi ya Samia kwa maksudi ya kutaka kumvurugia asiendelee kuwepo kwenye uongozi hapo 2025.
Kilicho wazi katika haya yanayo endelea sasa ni kundi ambalo linapigana juu chini kuhakikisha Samia anabaki madarakani, hata ikilazimu kuondoa roho za waTanzania; na Samia ni mhusika mkuu katika mpango huo.
Acha kueneza fikra potofu kwa maksudi mazima.