Pre GE2025 Mtazamo: Wanamtengenezea mazingira ya kuchukiwa na umma ili 2025, kundi kubwa la CCM lijitenge ili wamuangushe kwenye uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chura Kiziwi hawezi kusikia haya.
 
Mama Samia kaingia ndani ya box, kuna wahuni ndani ya CCM tayari washamharibia..

Ana kazi kubwa ya kufanya na muda ni mchache mno kwake

Lazima wahuni wote awateme fasta, aruhusu mabadiliko ya sheria haraka kuelekea 2025 kujinusuru.

Hawa ma.chawa wa mama hawana lolote la kumsaidia ni ma bendera fuata upepo.
 
Utakufa na stress tu!
 
Mtu anayefanya haya mambo ni yule mzee wa Tembo na vijana wake...shika hao
 
MAZURI YOOTE YANAYOFANYIKA nchi hii yananasibishwa na RAISI ,pia SIFA ZOOTE kwa Raisi ndiyo kafanya hayo kujenga choo Cha shule,hospitali,sokoni,kuleta maji,kusambaza umeme, kujenga madaraja nk yaani sifa kedekede,Swali JEE. MUAJI YOOTE na utekaji,mateso, YANAYOFANYIKA nchini tuyanasibishe na NANANI?
 
Mimi nililiona hili toka mwanzo kabisa na nikasema huyu mama hana muda wa kufanya ujinga huo kuua watu,ili wasimpinge kwa kipi na nguvu ipi waliyonayo, Tatizo CCM imejimilikisha kila kitu,police wanamiliki waoTISS wanaimiliki wao hakuna weledi kabisa katika usalama wa Taifa unakumbuka kabla ya Jiwe kufa walikufa viongozi karibu 6 na bado kama wanafurahia kumiliki vyombo vya dola visiwe huru nawaambia kwa nachojua watauana sana kabla ya 2030 huu utekaji na mauaji ni kuionesha jamii tu kuwa Mama hafai ili wapate wanaomtaka pia kosa kubwa kwa mama ni kumrudisha bashite katika system huyu alitakiwa apotezwe kabisa ila kutaka kubalance uislamu na ukiristo itamponza sana, Aandae sheria zitazounda taasisi yenge nguvu kama mataifa mengine yalivyokumbwa na changamoto za mauaji na watu kupotea waliunda taasisi kama FBI ,CID,NID n.k
 
Kile alichosema JK kuwa mgombea wa CCM 2025 ni Samia labda hapa katikati mambo yaharibike sana sasa kimeshatimia, mambo yamekwisha kuharibika sana, swali je ni nani atapeperusha bendera ya CCM 2025?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…