Habari za leo wapendwa, Katika muendelezo wa ziara za mh.Rais katika kanda ya ziwa ,mengi yanatokea,na mengi yataendelea kutokea.
Hii inashaabiana moja kwa moja na kauli ya wahenga inayosema "kwenye wengi kuna mengi"
Binafsi sishangazwi sana na mijadala mbalimbali inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vijiwe vya kahawa kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotokea kwenye ziara hii haswa matukio pamoja na kauli tofauti tofauti zinazotolewa.
Kimsingi,ni mambo ya kawaida haswa kwenye siasa zetu changa.
Turudi kwenye mada, moja ya kwenye kauli ya mh. Rais ambayo imezua mjadala mkubwa ni hii aliyosema, "TUSILAZIMISHE VYOMBO VYETU VYA ULINZI NA USALAMA VIKAFANYA MENGINE"
Kauli hii imeleta ukakasi kwa kuwa mh.Rais ajasema ni mambo mengine yapi,hivyo kutoa mwanya kwa kila mtu aliyesikia kauli hii kuja na mitazamo tofauti.
Kwa upande wangu nadhani kauli hii ya mh.Rais inapaswa kusikilizwa kwa masikio ya hekima ,bila kuweka hisia.
Binafsi naiona kauli hii kama kauli ya kiongozi anayejua uzito wa majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama, kwa hiyo anapigania hadhi na morali yao.
1. RAIS ANATETEA MOYO WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA
"Kauli ya Tusilazimishe" ni kama kusema ,"wapendwa vyombo hivi vina kazi maalumu ya kulinda taifa, dhidi ya maadui wa ndani na wa nje,kwa hiyo tusiwapeleke kwenye kazi ambazo siyo za kwao hadi wakachoka na kuvunjika moyo"
2. NI KAULI YA HURUMA NA UELEWA WA MZIGO WALIONAO WATUMISHI WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA
Watu wengi husahau askari ni binadamu pia hivyo wanahitaji heshima,faraja na msaada wa kihisia ,hivyo Mh.Rais anasisitiza ,tusiwasukumie kila mgogoro kwao,tuwaache wafanye kazi zao kwa weledi na heshima bila kuwaingiza kwenye masuala ya kisiasa.
3. NI KAULI INAYOZUIA KUTUMIWA KWA VYOMBO HIVI KWA MALENGO BINAFSI.
Mh.Rais anapozungumza hivi anaonya juu ya watu au makundi yote yanayojaribu kutumia vyombo hivi kwa maslahi yao,hii inalinda taasisi hizi zisije kupoteza uadilifu wake na kupoteza uaminifu mbele ya jamii.
4. NI KAULI YA KULINDA UTAALAMU NA WELEDI WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA
Kimsingi vyombo hivi ni vya kitaalamu,vyenye mafunzo ya kutosha juu ya kushughulika na usalama wa kitaifa,,kazi za propaganda za kisiasa si sehemu ya mafunzo yao,hivyo Rais anatoa wito kwamba "tusipotoshe taaluma yao kwa kuwaingiza kwenye matope yasiyo wahusu.
Wito wangu, naomba tuvilinde vyombo vyetu visikate tamaa,visichoke na tusivihukumu kwa mambo yasiyo wahusu,tuwaache wafanye kazi yao kwa heshima na weledi.
Samialization, OCTOBER TUNATIKI.