Wewe ndio huelewi dunia inaendaje. Marekani sio taifa la “kikabila”; inashikiliwa na wadau na wataalamu toka dunia nzima chini ya magenius maalum. Wako Wayahudi, Warusi, Wachina, Wahindi, Waarabu, Wajapan, Waajemi, Wajerumani, Waingereza, n.k. Hakuna anayetaka wala kuweza kuiangusha.
Sana sana watu wanagombania nafasi ya kuiiongoza Marekani kama ilivyo. Si rahisi kuisuka nchi ikaendeshwa na “MFUMO” tu kama ilivyo Marekani. Kasome mikakati ya “systems” labda ndipo utaielewa Marekani. Nchi zinazoongozwa kidikteta haziwezi kuchukua nafasi ya Marekani zikaaminika kushikilia nguzo kuu za uchumi na usalama wa dunia. Itakuwa chaos from day one.
Katika hizo nchi ulizozitaja, Iran ndiyo tofauti. Wao hawana interest na maisha ya duniani. Hivyo kuanguka kwa Marekani ndiyo kuanguka kwa dunia na mwisho wake. Wao wanawaza maisha ya peponi tu. Hao ndio kweli wanataka sana anguko la Marekani. Sio hao wengine wenye hamu kubwa ya maisha mazuri hapa duniani.