Tangu dunia imeanza kumekuwa na “tribal nations” na tawala za kifalme baadaye republics lakini bado za kikabila zaidi. Dola za Waajemi, Warumi, Ottoman, n.k.
Marekani sio dola ila ndio taifa pekee unaloweza kuliita “taifa la dhana mpya” (concept nation) liliowazi kwa watu wa mataifa yote waliopania kuiishi “ndoto ya Marekani” (the American Dream).
Bado hawajafanikiwa kuweka sawa misingi yote ya hiyo dhana lakini wamefikia hatua ya kuvutia mamilioni ya watu wa mataifa yote kutaka kuhamia huko, kusoma huko, kununua majengo huko, kuweka matrilioni ya dola huko na kununua hati fungani za hazina ya Marekani. China ina hatifungani za dola karibia bilioni 900.
Sasa sijui nani anaweza kuwa mbadala wa hilo concept nation. Kama sijaeleweka just ignore me.