Mtazamo wangu kuhusu Mahojiano aliyofanyiwa Rais Putin

Mtazamo wangu kuhusu Mahojiano aliyofanyiwa Rais Putin

Unaweza kwenda kula bata Beijing au Moscow?
Utakula bata lipi huko wakati muziki mzuri, NBA, Football, sinema na starehe nyingine zote unazozijua viko USA na Ulaya.
Starehe kumbe umeziyakisi kwa mtindo wa kimarekani??
Mbona hata UAE/Dubai starehe zipo pia?
Pata muda katembelee visiwa vya Cappadoccia Uturuki kuna starehe zote unazozijua wewe.
 
Ni mataifa gani hayo, kama ni ya kiarabu sio kweli waarabu wengi wanakimbilia Marekani na nchi zingine za magharibi. Wachina wamejaa Marekani hadi wana miji inaitwa China Town.

Nchi inayoongoza duniani kwa visa yake kuombwa na watu wengi ni Marekani, zaidi ya watu milioni mia moja huomba kwenda Marekani kila mwaka.

Pesa ambayo Marekani inapata kwa mwaka kutokana na malipo hayo ya visa inatosha kuendesha wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo kwa mwaka tena na kubaki.

Hapa duniani katika kila watu watano wanne wanatamani kwenda Marekani na wengi wako radhi kuhatarisha maisha yao ili mradi tu wafike Marekani na hata hao waarabu waliowaletea dini hawapendi kabisa kwenda Russia, sijui Iran wala China bali wanapenda kwenda na kuishi Marekani.

Kipindi Trump akiwa rais alipotoa agizo kupunguza waislam kwenda Marekani waarabu walilia kama watoto wadogo
Bado udini unakukandamiza fikra we kijana.
1)Sababu ya waarabu kuhamia US ni ukimbizi na kwa sasa hivi wakimbizi wengi hukimbilia Turkiye na Qatar ambako uchumi umekua.
Kafuatilie idadi ya wakimbizi wa kiarabu utakuja kuona Uturuki imepokea wakimbizi wengi kuliko hiyo US.
Kuhusu CHINA TOWN UNAREJELEA KIPINDI CHA OPIUM WAR AMBAPO CHINA ILIKUA INAONGOZWA NA WARLORDS KILA KONA,Wimbi la uhamiaji likatokea kutoka China kuja US kutafta maisha na China town ilianza miaka ya Opium war,hujui historia kasome.
2)Unaowataja wewe wengi wao wakimbizi na wahamiaji haramu ndio wana ndoto za kuzamia huko.
Ila kwa watu wanaotafuta potentials asia ndio kuna potentials nyingi.
KAFUATILIE INDONESIA,MALAYSIA,QATAR,TURKIYE NA SINGAPORE NA MACAU KESHA URUDI.
Halafu usipende tu kudandia directly inapotajwa nchi kinzani na US ukakimbilia za kiarabu,japo zipo baadhi za kiarabu.
Hiyo Saudi Arabia yenyewe inatajwa kutaka kuua soko la mpira la Ulaya kwa uwekezaji wanaouweka.

Pia Trump alipiga katazo la waislam SIO WAARABU.
 
USA haina uwezo wa kulazimisha nchi yeyote kufuata sera zake wala kuingilia sovereignty yake kama iko makini.

Ni ujinga wa viongozi na wananchi wa hizo nchi kuendekeza utegemezi kwa US na washirika wake.

Nchi zinaendekeza viongozi mafisadi wasiokuwa makini kusimamia maendeleo yao kutwa kuchwa wako busy kutafuta misaada na mikopo nafuu halafu watarajie kuwa salama mbele ya super donor. Lazima wapewe masharti magumu. Ukishindwa kujitegemea ukajilegeza kwa masponsor lazima uhuru wako uwe mashakani. Ndio tatizo la nchi nyingi za Afrika hadi leo.

Kama nadharia zangu zimepitwa na wakati, sawa, isiwe tabu. Muda utaweka ukweli wazi.
Basi kuna mengi huyafuatilii ndugu.
Sio kila masharti anayoweka US katika ushirika basi ni kuwabana mataifa kisa yanaendekeza kuomba misaada.
Kuna sehemu ngapi USA alipokosa interest zake akafanya regime change katika hizo nchi??
Kuna sehem ngapi USA aliponyimwa interest zake akaziwekea sanctions hizo nchi?
Mathalan kafuatilie mzozo wa Venezuela kesha uniambie je, hiyo sio kuingilia sovereignty ya nchi husika??
 
Dora sijui tawala ni wale wale, Kila kitu na zama zake, ilikuwepo vikings,Rumi, Persia, Ottoman, Ufaransa Uingereza Hispania Ureno na makoloni yao. Sasa hivi .ukoloni umerudi Kwa jina la washirika wa Marekani.. Sasa shida Iipo Kwa baadhi ya nchi zinapokataa neo colonialism ya Marekani. Ndo kama vile Urusi, Irani China etc zinapigwa vikwazo na majina ya ugaidi yanapewa
Kwa nini nao hawa-reciprocate? Vikwazo vya Marekani ni unilateral - vinazuia ushirikiano na Marekani na washirika wake (wanaokubali). Sio vya kimataifa kama vya UN.

Nchi zilizopigwa vikwazo nazo zinaweza kuiwekea Marekani vikwazo unilateral zikitaka.

Btw, hivi karibuni Urusi, China, Mexico, Canada na EU wameshawahi kuiwekea Marekani vikwazo vya kibiashara kujibu mapigo.
 
Basi kuna mengi huyafuatilii ndugu.
Sio kila masharti anayoweka US katika ushirika basi ni kuwabana mataifa kisa yanaendekeza kuomba misaada.
Kuna sehemu ngapi USA alipokosa interest zake akafanya regime change katika hizo nchi??
Kuna sehem ngapi USA aliponyimwa interest zake akaziwekea sanctions hizo nchi?
Mathalan kafuatilie mzozo wa Venezuela kesha uniambie je, hiyo sio kuingilia sovereignty ya nchi husika??
Unafikiri US wanaweza kufanya regime change North Korea, China au Iran? Ya Venezuela, Cuba na South America yote nayajua vizuri sana. Nchi yeyote ikijilegezalegeza wako wahuni watakajaribu kuiingilia.

Uzuri wa US serikali yao inapofanya mambo ya ovyo nje ya nchi habari zake zikivuma ndani ya nchi, wananchi huanzisha harakati nzito kupinga na kupambana na serikali. Mfano ni vita ya Vietnam, Korea, Iraq, hata vita ya Urusi na Ukraine na ile ya Gaza Wamarekani hawako pamoja wao kwa wao na wao na serikali yao.

Angalia Rwanda inachofanya huko DRC na kwa majirani wengine. US ina interest zake ambazo kusema kweli nyingi sio njema kwa mataifa husika. Ikipata mwanya inajipenyeza. Mataifa mengi yenye uwezo hufanya hivyo. Ni juu ya kila nchi kuwa makini kujilinda. Ndizo kazi za TISS na majeshi mengine.
 
N.korea alitaka ila kashindwa maana N.Korea iko backed na China since vita za mgawanyo 1959.
Iran alijaribu pia mpaka sasa na anajaribu na aliposhindwa kufanya regime change akaiwekea economic sanctions kibao Iran pamoja na hiyo N.Korea hata hiyo Venezuela alitaka fanya regime change akafeli akaishia kuwawekea economic sanctions pia.
China hawezi maana ni taifa lenye nguvu sawa na yeye US kiuchumi na kisiasa za kidunia,ndio maana hata Ursula Vonder leyen aliwaambia US wazungumze na China wayamalize juu ya mzozo wa Taiwan maana ikilipuka vita dunia itaumia kwa namna ambayo haikuwahi kabla.

Hata hao wananchi wanapolalamika juu ya mambo ya hovyo ya ufadhili wa vita zinazoteketeza kodi zao je lini walisikilizwa?
Si mpaka leo US inapanga package mpya ya msaada wa kivita Ukraine na Israel?
Mataifa mengi hufanya hivyo ila mtindo wa USA and allies ni mbovu na unaoacha makovu.
Bora hata mtindo wa China wa kung'ata na kupuliza atleast kuna mutual benefits.
 
Tangu dunia imeanza kumekuwa na “tribal nations” na tawala za kifalme baadaye republics lakini bado za kikabila zaidi. Dola za Waajemi, Warumi, Ottoman, n.k.

Marekani sio dola ila ndio taifa pekee unaloweza kuliita “taifa la dhana mpya” (concept nation) liliowazi kwa watu wa mataifa yote waliopania kuiishi “ndoto ya Marekani” (the American Dream).

Bado hawajafanikiwa kuweka sawa misingi yote ya hiyo dhana lakini wamefikia hatua ya kuvutia mamilioni ya watu wa mataifa yote kutaka kuhamia huko, kusoma huko, kununua majengo huko, kuweka matrilioni ya dola huko na kununua hati fungani za hazina ya Marekani. China ina hatifungani za dola karibia bilioni 900.

Sasa sijui nani anaweza kuwa mbadala wa hilo concept nation. Kama sijaeleweka just ignore me.
Usichokijua ni kwamba kila muda linapoanguka taifa fulani kubwa hua zinakuja na ideology mpya au namna ya kuendesha dunia

Kulikua na mataifa yaliitawala dunia miaka na miaka ila yalianguka na maisha yakaendelea kama kawaida yaani

Hata Americant ikitokea likaanguka maisha yataendelea kama yalivyoendelea huko nyuma ila kutakua tu na mabadiliko fulani fulani basi
 
Putin anaamini yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kuilinda Urusi dhidi ya ubeberu wa madola ya magharibi hasa Marekani (kosa kubwa hilo).

Ule uasi mfupi wa Wagner ulionyesha namna Urusi isivyokuwa na udhibiti kamili wa kiutawala na kisheria. ....ni taifa kubwa tajiri wa rasilimali ila limekosa uongozi mzuri.

Putin akiondoka, Warusi wasipokuwa makini ni rahisi kuwepo Vita ya kugombea madaraka au mgawanyiko miongoni mwa Idara za Usalama, Jeshi na Oligarchs.

T14 Armata
Ndio mlivyo karirishwa na MSM kama
 
Usichokijua ni kwamba kila muda linapoanguka taifa fulani kubwa hua zinakuja na ideology mpya au namna ya kuendesha dunia

Kulikua na mataifa yaliitawala dunia miaka na miaka ila yalianguka na maisha yakaendelea kama kawaida yaani

Hata Americant ikitokea likaanguka maisha yataendelea kama yalivyoendelea huko nyuma ila kutakua tu na mabadiliko fulani fulani basi
Obvious. Ni kama kuelewa kuwa mwaka 2095 wote tunaochangia hapa JF mwaka huu hatutakuwepo.

Anyway, watakaobahatika kuwapo Marekani ikianguka watashuhudia hilo anguko.

Wenye kupata tabu hivi leo ni wale wanaotarajia anguko la US litakuja upesi; kwamba lipo karibu sana kutokea. Kitu ambacho siamini.
 
USA haina uwezo wa kulazimisha nchi yeyote kufuata sera zake wala kuingilia sovereignty yake kama iko makini.

Ni ujinga wa viongozi na wananchi wa hizo nchi kuendekeza utegemezi kwa US na washirika wake.

Nchi zinaendekeza viongozi mafisadi wasiokuwa makini kusimamia maendeleo yao kutwa kuchwa wako busy kutafuta misaada na mikopo nafuu halafu watarajie kuwa salama mbele ya super donor. Lazima wapewe masharti magumu. Ukishindwa kujitegemea ukajilegeza kwa masponsor lazima uhuru wako uwe mashakani. Ndio tatizo la nchi nyingi za Afrika hadi leo.

Kama nadharia zangu zimepitwa na wakati, sawa, isiwe tabu. Muda utaweka ukweli wazi.
Us ipi ambayo haiwezi kuingilia nchi nyengine na nchi makini kwa mtazamo wako inakaaje

Us hii hii iliwachagulia mpaka rais wa mchongo wale Venezuela baada ya kuona rais aliepo hatakua kwa maslahi yao
 
Obvious. Ni kama kuelewa kuwa mwaka 2095 wote tunaochangia hapa JF mwaka huu hatutakuwepo.

Anyway, watakaobahatika kuwapo Marekani ikianguka watashuhudia hilo anguko.

Wenye kupata tabu hivi leo ni wale wanaotarajia anguko la US litakuja upesi; kwamba lipo karibu sana kutokea. Kitu ambacho siamini.
Nadhani hakuna anaetarajia anguko la Americant litakuja lini hili suala umesema wewe

Ila uhakika nikwamba hata kama mwaka 4000 Americant itaanguka na maisha yataendelea bila ya uwepo wa Americant na hii ndio system ya maisha ama dunia ilivyo
 
Obvious. Ni kama kuelewa kuwa mwaka 2095 wote tunaochangia hapa JF mwaka huu hatutakuwepo.

Anyway, watakaobahatika kuwapo Marekani ikianguka watashuhudia hilo anguko.

Wenye kupata tabu hivi leo ni wale wanaotarajia anguko la US litakuja upesi; kwamba lipo karibu sana kutokea. Kitu ambacho siamini.
In reality US ishaanguka ila theoretically bado super power wa mchongo.
 
Back
Top Bottom