Texas Tiger
JF-Expert Member
- Nov 5, 2022
- 483
- 1,100
Uchunguzi wa kibinafsi (observations) hautoshi kuthibitisha nadharia ya kisayansi. Ushahidi wa kisayansi unahitaji tafiti za kina, majaribio yanayorudiwa na mapitio ya wataalamu wengine.Mkuu hii ni jamii forum tumo humu ila hatujuwani.
Kwa vile wewe unauelewa kuhusu sayansi naomba twende taratibu
Ipo hivi kulingana na observation zangu kwa wagonjwa wa mashetami ukiwauliza wanachodai ni kuhisi wanakabwa (suffocation) pia maumivu ya kichwa kifua, moyo kwenda mbio na kuhisi kuchanganyikiwa
Kisayansi mtu anayehisi kukabwa (asphyxia) maranyingi supply ya oxygen inakuwa ndogo kwenye mapafu na damu
Ataanza kuhema haraka ili avute oxygen ya kutosha, moyo utaongeza spidi ya kusukuma damu ili kufidia oxygen ktk maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo ubongo na vital organs zingine, supply ya oxygen ikiwa ndogo kwenye muscle za moyo mtu atahisi kifua kinabana, supply ya oxygen ikiwa ndogo kwenye ubongo mtu atapata halucination
Pia ataanza kupumua kwa anaerobic respiration anakuwa na nguvu nyingi kiasi kwamba inahitaji wanaume wenye afya kumkamata akiwa ktk hali ya kutapa tapa
Sasa akipewa dawa inayochomwa ktk moto ule moshi akiunusa kifua kinaachia fahamu zinamrudia na anatulia kabisa lakini anakua hana nguvu
Hii nimeishuhudia
Kumbuka mtu mwenye majini ki medical ni unknown disease
Sasa kulingana na scenario kama hii nikawaza huenda majini ni gesi inayofanana na carbonmonoxide maana carbonmonoxide nayo humfanya mtu akose supply ya oxygen kwa sababu carbonmonoxide huea ina combine na haemoglobin mazima
Sasa inawezekana hiyo gas X ikawa na sifa kama hizo na huo ndio ukawa mwanzo wa mimi kufikiria hivyo mkuu
Tafiti zinaanza na mawazo mapya mkuu
Sijui umenielewa?
Hizo, daily kama suffocation, maumivu ya kifua au hallucinations zinaweza kutokana na magonjwa yanayojulikana kama vile
1. Anxiety/panic attacks
2. Hypoxia (upungufu wa oksijeni)
3. Poisoning (kutokana na gesi halisi kama carbon monoxide)