Mtazamo wangu kuhusu majini (mashetani/ mapepo). Uliza swali lolote nitakujibu

Mtazamo wangu kuhusu majini (mashetani/ mapepo). Uliza swali lolote nitakujibu

Ki medical majini hayatambuliki, akija mtu mwenye majini hapo ofisini kwako utamterm kama mgonjwa wa akili ,(psychosis) utamsukuma wodi ya vichaa

Ila kabla hujafanya hivyo uta request vipimo ikiwemo cha Malaria

Sasa kikawaida mtu akiwa na supply ndogo ya oxygen au glucose ktk ubobgo kupitia mzunguko wa damu hupata hallucination (japokuwa sio watu wote)

Sasa mtu mwenye afya njema mfano mganga wa jadi au yeyote mwenye majini akivukizwa ubani au kupigiwa mdundo (dufu) anaanza kupitia pattern zote za mtu anaye hallucinate

Ataanza kuona vitu ambavyo mlio pembeni hamvioni, ataanza kukuambia matatizo yako kwa usahihi (mganga) ataanza kuongea lugha mbali mbali, kucheza au anakuwa kama anatembelewa na kitu ktk mwili wake utamuona kupitia body language na movement zake

Yote hayo yatatokea akiwa hajitambui (disioriented), je utasema ubani au mdundo ni triger au precipitating factor?

Sasa turudi kwa mtu mwenye malaria kali ambaye RBC zake zinapasuka pasuka na plasmodium wanakula glucose sasa supply ya oxygen na glucose si itakuwa chini?
Akianza kuhallucinate si ndio?

Nikirudi nyuma nkasema kukiwa na gas X ambayo ina combine na haemoglobin ili kupunguza oxygen kwenye circulation na kusababisha hypoxemia kwenye tissue za ubongo na mtu kuhallucinate ntakuwa nakosea?
Maelezo mazuri natamani ueleze zaidi kuhusu Gas X Kuliko hivyo vingine existing Particles
 
Pia nasikia kuwa jini huwa haondoki mwilini mwa binadamu hata kama ukifanikiwa kulifukuza baadae hurudi tena mwilini mwako, hii imekaaje?
JINI anapokuwa ndani ya mtu anakuwa anaishi katika mazingira mazuri sana kwake anapata advantage ya chakula maji na makazi kutoka kwa host wake.
IKITOKEA AMEFUKUZWA ametolewa kutoka kwa host kiti wake .

Huenda akizunguka zunguka nyikani nchi kavu?why nchi kavu na si kwenye maji?sababu akigusa sehemu ya maji kama kisima,mabwawa,bahari,mito nk water bodies ni lango la kuzimu atavutwa na kitokea kuzimu.Akirudi kuzimu atapewa adhabu kwa kishindwa kwake ku complete mission ya kukaa ndani ya mtu.Wao waki fail mission huwa wanapewa severe punishment .
Huko nyikani huteseka na kuona KIU,NA NJAA na hukosa makazi mazuri.Hukumbuka na kuamua kurudi kwenda kumchungulia yule binadamu aliyekuwa akiishi ndani yake(nyumba/makazi yake ya zamani.

Akikuta nyumba yake imesafishwa imepambwa vizuri (KATIKA ULIMWENGU WA GIZA..wakisema mtu msafi kwao wanamaanisha ni mtu asiye na ushirika na YESU asiye na nguvu ya Yesu.Na wakisema mtu mchafu (KAFIRI)au ana damu chafu(KAFIRUNA) wanamaanisha mtu aliye na nguvu ya YESU KRISTO au mtu ambaye damu yake imechanganyika na damu ya Yesu mfano mtu anayeshiriki meza ya BWANA ile sakramenti ya meza ya Bwana au aliyeokoka huyo damu yake inaitwa ni chafu haifai katika ulimwengu wa giza .ILA katika ulimwengu wa Nuru au macho ya Mungu ni msafi..wao wako kinyume.

sasa wakikuta ni msafi maana yaks mtu mwenye dhambi kwa maana ya kinyume basi HUENDA KUWAALIKA majini wengine saba wabaya kuliko yeye pamoja na yeye HURUDI na kumuingia wote 8..NA HALI YAKE YA SASA HUWA MBAYA KULIKO ILE YA HALI ALIYOKUWA NAYO MWANZO mana anakuwa na majini mengi na mabaya kuliko lile moja la mwanzo.

SULUHISHO
ndio maana YESU alipokuwa akiponya watu na kuwatoa pepo alikuwa anawaambia umeponywa ,umeokolewa,umesamehewa lakini USITENDE DHAMBI TENA (sin no more.)
Dhambi inaitwa ni mauti dhambi ni kufungua mlango wa kuruhusu kuingiliwa na maroho machafu na majini..dhambi kama UZINZI nimeto mfano huu kwa sababu ndio dhambi inayopendwa na wengi na ndio imeonekana kama ni ufahari na sifa kuwa MZINZI MALAYA..ila ni dhambi zote ....ni mauti dhambi zote zinakutenga na Mungu,dhambi zote zonafungulia lango la wewe kushambuliwa na maroho machafu/majini.
INAKUWA MBAYA ZAIDI kama ukienda kutibiwa kwa mganga wa kienyeji au manabii na mitume wa mafuta ya upako.Kwa sababu na wao wanatumia majini hayo hayo na nguvu ya kuzimu ni chama kimoja na shetani, jini hawezi kumtoa jini mwenzake ila wana alikana na kukaa ndani yako pamoja .
 
Refferences/marejeleo..

A.ELIMU YA FALAKI/ELIMU YA MAUMBO elimu ya maarifa walimu
1)SHEIKH OMARY MNYESHENI.(promover youtube tv channel)
2.SHEIKH HUSSEIN MUBARAKA(promover youbtube
3.MCHUNGAJI AMIELI KATEKELA(promover you tube
4.Askofu MOSSES KULOLA silas you tube tv channel

B.BIBLE/ BIBILIA

C:SHUHUDA -promover you tube tv channel ushuhuda/shuhuda na jaktan,msafiri...#PROMOVER YOUTUBE TV CHANNEL

Napendekeza zaidi kumsikiliza MCHUNGAJI AMIEL KATEKELA-ame narrate vizuri kwa kina ELIMU YA MAJINI na shetani japo huyu ni mwanafunzi wa sheikh omary mnyesheni ila yeye kaelezea vizuri kuliko mwalimu wake.
 
Mimi Nakuelewa Sana ila Tu sitaku Kurelay kwenye Thesis zako kwa Sababu bado hujaelezea Vya Kutosha Hujatoa Sababu za Kichemikali wala Hujatoa sababu za KIbaologia..

Though Point zako Zina matter sana Na Kuna Kiukweli kidogo japp bado hujaeleza Vizuri na Kwa kina
Mkuu nakuheshimu sana na nashukuru umekuwa mvumilivu ktk kuchangia

Lengo langu ni kupata challenge na kuwasilisha kile ninachokifikiria ili watu wengine waelewe wqkosoe watoe mawazo yao tuone panapo vuja hasa hasa wadau wanaouelewa mwili wa binadamu na migumo yake kama wewe

Ninaweza nikajua kutatua changamoto kama hizi kwa usahihi na mtu akapona kienyeji ila nikawa sijui mechanism yake

Na hii elimu ipo sana hapa Tanzania ila wanaoipractice hawana uelewe wa anatomia, fisiologia pasolojia n.k
Ila wqna practice

Hayo yalikuwa ni mawazo yangu binafsi ila ahsante sana kwa muda wqko ktk huu uzi naahidi nitaleta tena jambo jingine wakati mwingine
 
Maelezo mazuri natamani ueleze zaidi kuhusu Gas X Kuliko hivyo vingine existing Particles
Gas X nimeifikiria kwa kutumia logic tu mkuu

Ili kupata maelezo ya kisayansi na ushahidi kuna vitu vinamiss

Elimu kuhusu molecular biology na majaribio ya kimaabarq ambayo yanahitaji resources

All in all hata wewe unaweza kuendelea kufikiria nilipoishia
 
Sayansi na ushirikina majini ni vitu vinavyopingana.
Kwasababu kitu chochote kinachopingana na LAWS Za PHYSICS ni miujiza mfano rahisi law of gravity mfano mshirikina akishirikiana na majini wanaweza kufanya miujiza mingi ambayo iko against laws of physics..mfano mtu kuingia ndani kwako kwa kupenya ndani ya ukuta ukuta kufunguka halafu akaingia ndani halafu akaufunga ,kupaa angani au hata kusafiri ndani ya kijiko,ndani ya ungo ungo mmoja unaweza ukapakia zaidi ya watu washirikina zaidi ya wawili,
UCHAWI kama uchawi ni art /craft ya peke yake inayojitegemea na kuna vyuo vinavyofundisha uchawi MAJINI kama masomo yanayojitegemea
HITIMISHO
SAYANSI na mambo ya kiroho majini/ushirikina/uchawi ni vitu viwili tofauti..vinavyopingana.
 
OMOYOGWANE swali langu kwako. Umesema hawapendi harufu ya mikojo, jasho Kali n.k
Je mtu mwenye jasho au harufu ya mikojo hawezi kuingiliwa na hao viumbe? Na je Kama anavyo, akiwa na jasho kali au mikojo hivyo viumbe vinaweza kutoka au vinaendelea kubaki?
 
kwa uelewa wangu uchafu wa mwili mfano ulevi,mkojo,kinyesi,nguruwe,uzinzi sigara,bangi,ushoga,uchafu wowote hauwezi kuwazuia majini yasimuingie mtu.TENA infact chooni ni mlango wa kiingiza na kiyaita majini,tena worse enough ushuhuda wa wachawi /washirikina washirikinwa majini wenyewe huwa wakiishiwa nguvu za kishirikina zikipungua katikati ya vita vya kiroho hukimbilia CHOONI na kuyavuta kinyesi chooni kimiujiza na huanza kula kinyesi chooni ili kujiokoa wasife wakizidiwa nguvu katikakati ya vita ,pona yao ni kukimbilia chooni na kuanza kula mavi.

Tena kuna majini ukiwa nayo yanakupelekea uwe shoga,uwe mlevi wa pombe,madawa ya kulevya ,sigara bangi uwe mwizi ,uwe msagaji,
HITIMISHO..uchafu wa mwili hauzuii majini yasikupate ,na hakuna watu wachafu kama wafuga majinj ule usafi wanaigiza mchana machoni pa watu alnadhifu ni usanii.Backstage katika ushirikina wao wanakula uchafu sana na uchafu mwingi wanakula makaburini wanakula (MAKABURINI+ na CHOONI).
AISEE hakuna jini msafi..mana wao ni ROHO CHAFU asili yao ni uchafu...hata walipofukuzwa ja Yesu waliomba waingie kwa nguruwe na wote tunajua nguruwe ni miongoni mwa wanyama WACHAFU.
 
Uwezekano ni mdogo sana sana sana

Maana mikojo sometimes humika kuyafukuza mapepo pia baadhi ya mimea yenye harufu kali nayo hutumika

Pia mtu wa namna hiyo akitaka jini la kupandikiza lazima limkatae maana ni mchafu
 
kwa uelewa wangu uchafu wa mwili mfano ulevi,mkojo,kinyesi,nguruwe,uzinzi sigara,bangi,ushoga,uchafu wowote hauwezi kuwazuia majini yasimuingie mtu.TENA infact chooni ni mlango wa kiingiza na kiyaita majini,tena worse enough ushuhuda wa wachawi /washirikina washirikinwa majini wenyewe huwa wakiishiwa nguvu za kishirikina zikipungua katikati ya vita vya kiroho hukimbilia CHOONI na kuyavuta kinyesi chooni kimiujiza na huanza kula kinyesi chooni ili kujiokoa wasife wakizidiwa nguvu katikakati ya vita ,pona yao ni kukimbilia chooni na kuanza kula mavi.

Tena kuna majini ukiwa nayo yanakupelekea uwe shoga,uwe mlevi wa pombe,madawa ya kulevya ,sigara bangi uwe mwizi ,uwe msagaji,
HITIMISHO..uchafu wa mwili hauzuii majini yasikupate ,na hakuna watu wachafu kama wafuga majinj ule usafi wanaigiza mchana machoni pa watu alnadhifu ni usanii.Backstage katika ushirikina wao wanakula uchafu sana na uchafu mwingi wanakula makaburini wanakula (MAKABURINI+ na CHOONI).
AISEE hakuna jini msafi..mana wao ni ROHO CHAFU asili yao ni uchafu...hata walipofukuzwa ja Yesu waliomba waingie kwa nguruwe na wote tunajua nguruwe ni miongoni mwa wanyama WACHAFU.
Unasemea mapepo ndiyo hupenda mtu aharibikiwe ila akinywa pombe au kuvuta bangi itatokea reaction ktk circulation ya damu (hypersensitivity) lazima achizike au kupata madhara makubwa na kupona ni mziki
 
uchafu hauna madhara yoyote kwa majini machafu,majini yenyewe ni machafu(roho chafu),uchawi na uganga wa kienyeji ni uchafu,kuzimu ni kuchafu dhambi ni uchafu...YANI uchafu ndio sifa ya kuzimu.

Huo usafi wa majini na wachawi washirikina waganga wa kienyeji ni wa MAIGIZO ila kwa ground/chini ya carpet,back stage ni MACHAFU..na huko CHOONI ni moja ya maskani na mavi ni chakula chao kinachowasaidia kuongeza nguvu za kishirikina hasa wanapozidiwa nguvu ili wajiokoe wasife wanakimbilia chooni kula mavi,
nguruwe ni maskani yao,pombe ,bangi,uzinzi tena uzinzi name any uchafu kwao hauna madhara bali ni advantage hata uzinzi unawasaidia kuchukua mbegu shahawa za wazinzi na wanaojichua masterbate shahawa zao zinachukuliwa na majini kwa ajili ya kazi za kishirikina..pia majini mahaba yanaweza kufunga ndoa na wanaojichua punyeto au zini ndotoni..

HITIMISHO
UCHAFU ni sifa ya shetani,majini ,wachawi,waganga wa kienyeji washirikina na kuzimu..sema huwa wanaigiza USAFI kwa nje fake/bandia/maigizo ila kiundani uchafu ni asili yao.

Hakuna uchafu wowote unaoweza kuwafukuza majini sio mfupa wa nguruwe,sio bangi ,sio kinyesi wala mkojo wala sio chooni,wala sio harufu ya maua wala myth nyingine zote...wala sio pombe nk.

KITU AMBACHO KUZIMU Majini shetani na wachawi,waganga washirikina wanaogopa ni kimoja tu..
JINA LA YESU

WALOKOLE WA KWELI wenye nguvu za Mungu sio waenda kanisani WALOKOLE HALISI WA KWELI ambao wana Roho wa Mungu na ulinzi wa malaika ,nguvu ya Yesu wana mamlaka na nguvu kubwa sana ya kuangamiza na kuharibu hata kuua ufalme wa kuzimu.
 
Nikweli mkuu mimi nina mwaka wa 7 huu napambana kuyafukuza majini mwilini mwangu ila bado yananisumbua

Nimekesha sana kwa waganga, nimekesha sana kwa manabiii nyumba zote za ibada nimeshiriki sana lakini wapi hadi manusura nikufuru utadhani sijaumbwa na Mungu...
 
naunga mkono hojab
si kweli majini wanaweza ishi eneo lolote mwilini.
si kweli majini wanaweza ishi eneo lolote mwilini.
naunga mkono hoja ,majini yanaweza kukaa sehemu yeyote mwilini na katika kiungo chochote cha mwili kwa kazi maalumu iliyokusudiwa,hayana mipaka.

Mfano mwanamke mmoja yalikaa katika kizazi yakawa kama multiple leiyomyoma /multiple uterine fibroids mauvimbe mengi kwenye kizazi ndivyo yalivyokuwa yanaonekana kwenye picha za ultrasound na dalili alikuwa nazo clinically ikiwemo kutoka damu na maumivu
.Mchungaji SHEMDOE anaweza akashuhudia hapa.
Sasa ikaonekana anatakiwa atolewe kizazi kama sehemu ya matibabu yake.
Na kazi maalumu ya haya majini yaliyokaa kwenye kizazi kwa mfano wa mauvimbe lengo lake yalikuwa yamfanyike mwanamke huyu awe mgumba na yalikuwa yanataka yaondoke na kizazi ili asizae maishani mwake,mana pia alikuwa hana hajawahi kupata mtoto na yalikuwa yanataka asizae na asipate mtoto kamwe...NDiyo mission yao.
Kabla ya kwenda kufanyiwa upasuaji wa kutoa kizazi mana ndio ilikuwa matibabu yake

,huyu mama alikuwa na appointment ya kwenda kuombewa na mchungaji shemdoe..lakini siku ya appointment ya kwenda kuombewa akahairisha akaenda hospitali kutolewa kizazi kama sehemu ya matibabu mana piabalikuwa ana bleed sana kutokana na hayo mauvimbe(ni dalili mojawapo ya hayo ma uterine fibroids yaliyokuwa yamezunguka kizazi chote kwa kiwango kikubwa .

Baada ya kutolewa kizazi baada ya wiki kadhaa kupita akaja kwenda kwa mchungaji tena alikwenda si kwa ajili ya kuombewa alikwenda kumsalimia classmate wake kumbe classmate wake ni mke wa mke wa mchungaji ndio akakutana na mchungaji hakujua kuwa mchungaji ni shemeji yake...akaanza kulia akasema sikuja kuombewa
Mchungaji na mkewe na mwenyewe wakaanza kuomba pamoja yale mapepo yakalipuka ndani ya yule dada..YAKAANZA KUCHEKA yakasema mumeshachelewa tumeshachukua tulichokuwa tunakitaka MISSION COMPLETED...hataweza kuzaa tena tumeshachukua kizazi chake.
Wengine huwa wakiombewa wanapona na wakirudia kupima uvimbe hauoneknani tena kwenye picha mana inakuwa si uvimbe kiuhalisia ila ni mazingara,hata yeye kama angeombewa kabla ya kutolewa kizazi majini yangetoka hapo kwenye kizazi na huo uvimbe bandia ungetoweka.
 
Eeeh wakuu mpo?

Ktk huu uzi nitazungumzia kuhusu majini kiimani na kisayansi kulingana na experience niliyonayo ila pia mtu yeyote anaruhusiwa kuchangia kulingana na kile anachokijua au alichoeahi kukiona

Majini ni nini?

Majini kiroho ni viumbe hai wanaoweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu, sehemu wanazoweza kuweka makazi ktk mwili wa binadamu ni kifuani na kichwani namaanishq ndani.

Kisayansi majini ni gesi (molecule) inayofanana na carbonmonoxide, hii hewa huweza kuingia ktk mwili wa binadamu kupitia mfumo wa hewa yaani ukivuta hewa ndani ukaivuta hiyo gesi kama ipo eneo ulilopo ikaaingia kwenye mapafu na na kupenya ktk mfumo wa damu basi tutasema umepata majini. Hii gesi inatabia ya kuvibrate na hujishikiza ktk haemoglobin kwa muda kisha kubaki ktk mzunguko wa damu

Hii gesi ni mtizamo wangu kulingana na uchunguzi wangu naomba unayesoma hapa uelewe mapema kabisa haya maelezo ni mawazo yangu binafsi. Nitaiita gas X ktk uzi huu, hii gesi X ina exist ktk form mbali mbali yaani gesi X zipo za aina mbali mbali.

Mtu mwenye majini huwa anapata dalili zifuatazo ila sio lazima ziwe zote ni moja kati ya zifuatazo

Kuhisi kama unakabwa usiku, kuhisi kitu kinatembea mwilini, maumivu mwili mzima, kuwa na nguvu kupita kiasi na kukakamaa, kuchizika, kupandisha mapepo, kutoa miungurumo wakati wa kuvuta na kutoa hewa, kuumwa mwili mzimq, kuumwa miguu, macho kuwa meusi au kama ya paka yaani yanakuwa yanatisha.

MAJINI HAWAPENDI NINI?

majini hawapendi uchafu mfano harufu ya mkojo, au harufu yoyote kali mfano jasho linalotoka wakati wa ngono na maji maji ya uke au uume ile harufu hawaipendi,

Hawapendi harufu ya pombe, sigara au bangi.

Hawapendi vitu vichachu kama vile ndimu n.k

Kisayansi ni kwamba vitu nilivyotaja hapo juu vinaweza kufanya exchange ya gesi X ikqtoka ktk mzunguko wa damu ndio maana hawaipendi.

MAJINI WANAPENDA NINI?

majini wanapenda damu, usafi, harufu nzuri ya marashi kama vile gift of zanzibar, Al wood n.k pia wanapenda harufu ya ubani na udi

Kisayansi wanapenda damu kwa sababu kuna kiasi kingi cha haemoglobin, pia harufu ya ubani na udi hutoa oxygen ktk haemoglobin na kuifanya gas X ijipachike. Hapa maana yake ni kwamba kiasi cha oxygen ktk damu (oxygen saturation kitakuwa below 98% mtu atahisi kifua kinabana ataanza kuhema kwa kasi na hata kupoteza fahamu au kuwa kama amechangamyikiwa (halucination) kimtaa mtaa mnaita kupandisha yaani ansingia kwny anaerobic respiration akija kushusha anakuwa kachoka sana

Baada ya utangulizi nakaribisha maswali ya kiroho na kisayansi.

Ahsante
🤣🤣🤣
 
Nikweli mkuu mimi nina mwaka wa 7 huu napambana kuyafukuza majini mwilini mwangu ila bado yananisumbua

Nimekesha sana kwa waganga, nimekesha sana kwa manabiii nyumba zote za ibada nimeshiriki sana lakini wapi hadi manusura nikufuru utadhani sijaumbwa na Mungu...
Pole kaka kwa changamoto hiyo,umeshatambua tatizo lako linalokusumbua basi hivyo kwa kutambua kwako tatizo tu ni nusu ya kutatua tatizo.
1)TATIZO NI MAJINI YANAKUSUMBUA

2)Dawa ni Yesu,unampataje huyu Yesu aweze kukusaidia..kwanza TUBU dhambi ona kwamba wewe ni mwenye dhambi ,omba toba(msamaha)kwa kumaanisha kuacha dhambi zote ikiwemo kuiendea miungu ,kutegemea msaada kutoka kwa viumbe badala ya Muumbaji wa viumbe vyote hata shetani ni kiumbe tu cha muumba,kutegemea msaada wa wanadamu,mizimu/majini ya waganga wa kienyeji na jini hawezi kumtoa jini mwenzie n.k omba rehema kutoka kwa huyu Yesu .

1)Amua sasa kwa moyo wa dhati kwa kudhamiria kuweka tumaini lako lote kwa Yesu 100% bila kuwa na mashaka
,bila hofu na mashaka moyoni mwako amini YESU pekee ndiye anayeweza kukuokoa na kukuponya. kata shauri sio kwa kujaribu /kubahatisha..
kutoka moyoni mwako dakika ileile moyo wako umeumimina kwa Yesu umemkabidhi Yesu maisha yako akusaidie..ukaomba msaada na uponyaji toka kwa Yesu wewe mwenyewe bila hata kuombewa Yesu ataona Rohoni mwako..atakusikia atakusaidia atakuponya unaweka maagano kati yako wewe mwenyewe na Yesu wako mnazungumza nyie wawili peke yenu..anakusikia hata mawazo yako moyoni mwako anayaona, anasikia ukimwita atakuitikia atakusikia ukimuomba atakuasaidia

..lakini ni vizuri pia baada ya kusali hivyo ukafungulia na fm redio yoyote ya dini ya injili ya Yesu Kristo ..utapata muhubiri anahuburi kwa redio..ataomba na wewe kwa redio au tv utapoea uponyaji...
Pia Kesho amani ya moyo ile nguvu ipo moyoni mwako itakuongoza kanisa la kweli la kwenda kusali na naamini haitakuwa kanisa maarufu au la mitume na manabii wa upako wa mafuta n.k linaweza lisiwe marufu sana au lisiwe kubwa sana au lisiwe la kifahari kisasa sana ,na wachungaji wake wanaweza wasiwe hawa maarufu sana wanao onekana kwenye ma tv au vyovyote vile roho wa Bwana atakavyokuongoza moyoni mwako nenda hapo sali..ombewa hapo.

2)njia ya pilia ukishaamua kwa dhati toka moyoni kuamua kumfuata Yesu na kumuamini Yesu kuwa ni mkombozi wa ulimwengu kuwa anaweza kukusaidia mpigie namba ya mchungaji LAIZER huyu ni mtumishi wa Mungu mwenye nguvu ya Mungu akuombee...lakini inatakiwa ianzie moyoni mwako
..wewe mwenyewe uwe tayari sio leo unaombewa lakini bado kesho unaenda kwa mganga wa kienyeji maana itakuwa ni kukosa imani thabiti..(imani isiyo na mashaka )kukosa imani thabiti inaweza ikawa kikwazo kupokea uponyaji)

anayeokoa ni Yesu na sio wachungaji ,wao wachungaji wanatumika na Yesu,na hata wewe mwenyewe ukiomba kwa Yesu anakusikia vile vile kama anavyowasikia wachungaji
lakini mkiomba pamoja na mtumishi wa Mungu pia ni vizuri zaidi
,pia sikiliza kwaya na mahubiri,soma biblia ,pia ishi maisha ya haki,na jitenge na dhambi..
Mungu atakusaidia usikate tamaa ndugu yangu Mungu anakupenda ndio mana amekupa wokovu bure kupitia Yesu ,
Mungu hajakusahau ndio mana upo hai.leo..
Mshukuru Mungu na kumsifu..upo hai Yesu anakupenda sana alikufa msalabani ili kwa kupigwa kwake yeye sisi wote tupate kupona na uzima kwa gharama aliyoilipa kwa kuteswa kwake yeye Yesu na damu yake ikawa kafata ya kutukomboa kwa ajili yetu ukimwengu wote tusipotee tusionewe,tupate uponyaji na uzima na wokovu
Yesu anakwenda kukuponya leo sasa hivi.
Namba ya simu ya mchungaji LAIZER -
0754383650
 
Nimesemq gas X ina exist ktk form mbali mbali kimtaa mnaita majini

Yapo majini ya utambuzi na ya maradhi

Tuseme kuna gas X1 na gas X2 Sasa ktk hayo majini la utambuzi liwe X2 (Kumbuka majini yana majina mfano subiani makata n.k)

Sasa ili mganga apandishe majini inabidi supply ya oxygen ktk mzunguko wa damu iwe chini atalazimika kufanya mambo yafuatayo

Kujivukiza ubani ktk chetezo akiwa ktk shuka nyekundu au nyeupe shuka inayoreflect mwanga

Akijifykiza ule moshi utakavoanza kupita kooni na kuingia keny mapafu nyingine kwenye tumbo ataicheua kwa kutoa muungurumo , moshi wa mapafu utaingia ktk mzunguko wa damu na kuifukuza oxugen ktk haemoglobin na kuifanya gas X2 ikae kwenye haemoglobin

Suply ya oxygrn ktk damu yaani oxygen saturation ita drop

Supply ikiwa chini ktk ubongo ataanza kuhallucinate na kuanza kuona mambo ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyaona yaani hallucination na illusion

Ataanza kukuambia matatizo yako na anakuwa hajitambui inabidi awepo mtu wa pili ambaye ni msaidizi wa mganga
Mkuu kwa experience yangu sio kila anayepandisha jini na kuanza kuongea huwa inakuwa yeye mwenyewe hajitambu wakati huo na hajui anachoongea, nishaona mfano waganga hupandisha majini(huitwa waalimu) anakuwa anaufahamu wake unaongea nae kama unavyoongea na mtu ila anakuwa anaweza kueleza vitu ambavyo hawezi kuvijua akiwa hajapandisha hao majini.
 
Hawa majini wana asili moja tu ya Kiarabu pekee, au wapo waafrika, na Wazungu pia? Je Huko Ulaya, na amerika nako yakpo majini au ni Afrika na Middle east pekee?
 
Back
Top Bottom