MCHAWI NI MCHAWI TU HATA AKILIA SANA MSIBANI. WEWE NI CCM HALAFU UNAJIFANYA HUNA CHAMA. MUJINGA WA MWANACCM HAUJIFICHIKila mtu ana uhuru wa kuwa na mtazamo na labda kwako umeona nimekuwa upande wa raisi Magufuli, ila ukisoma kichwa cha habari ni utaelewa ni juu ya mtazamo wangu binafsi juu ya siasa ya Tanzania na raisi Magufuli na nimeandika kama kichwa kilivyojieleza. .
Ila umehisi nimeandika kumponda Mheshimiwa Tundu Lisu, na hicho ndio ulichokiona ila la msingi wewe huyaoini, je ni kitu gani ambacho nimezungumza juu ya mheshimiwa Tundu Lisu?? Ila hujajibu hata hoja yangu moja ila kwa kuipinga kwa Hoja au kubisha tu. Kwa mtazamo wangu tu umeandika hoja nyingine ambayo pengine ungeweza kuwa uzi mwingine unaohusu safari ya Tanzania kwenye mikono ya raisi Magufuli na pengine ningekujibu ila unanitoa ndani ya mada husika. .
Samahani ila nachokiona ni public sympathy, kama kupigwa risasi kwa mheshimiwa Tundu Lisu kinakunyima chuki yake binafsi dhidi ya raisi Magufuli inajikita mpaka kwenye kutaka kuboamoa Tanzania. Leo hii mheshimiwa Tundu Lisu anaomba publicly Tanzania inyimwe misaada, Je hiyo misaada anakula raisi Magufuli na familia yake? Hiyo misaada ni kwa ajili ya kila mTanzania ikiwemo mimi na wewe. Leo naona mheshimiwa Tundi Lisu anakubali kushikana kabisa mikono na mabeberu ili kusupport ushoga, kitu amabcho ni kinyume na maadili yetu, ambapo unampelekea chuki raisi Magufuli, wakati hoja ni kuwa chuki yake haileti maendeleo kwa Tanzania. .
Sipingi kama wana chuki ziwepo ila zisiwe kuiathiri Tanzania na waTanzania. Ila kipindi kile nilikuwa napata majibu mengi sana wakati Lowasa kasimama kugombea uraisi "kwani ikulu kuna kazi ya kubeba mawe". Ila nadaharia yako uliojiwekea ni kuwa nchi hii inaendeshwa na mtu mmoja tu anayeitwa 'Magufuli'. Ila nchi hii inaongozwa na viongozi wengi kuanzia ngazi ya kijiji mpaka ngazi ya nchi ambao sio CCM wala si kwa mawazo ya Magufuli. .
Raisi Magufuli kwenye uongozi wake kuna madhaifu mengi nimeandika moja ni kuharibu taaluma, sijaundika kumfagilia raisi Magufuli ila kwa kuwa nimeandika neno Tundu Lisu, basi nachoandika hata kama cha maana unakiona si kitu. Nachotaka tujibiane hoja kwa hoja na si kufanya siasa, na kama nimeandika umeona mtazamo finyu nielimishe nini kifanyike. Nadhani hujasoma vizuri hakuna sehemu nimeandika kiongoze chama kimoja unaweka maneno kinywani mwangu, nimesema natamani sana upinzani utawale siku moja ina maana hukuona???. .
Waliotoka utumwani ni wana wa Israel na sio Tanzania. Usitufananishe sisi na wana wa Israel wala utumwa wa Misri, sawa sawa na kuchanganya maziwa na tui la nazi. Tuache ya kwenye Biblia yabaki kwenye Biblia naomba unijibu au upinge hoja zangu kwa mifano au hoja. .
UNACHOMPENDEA HUYU DUDU NI NINI HASA?tindo,
Sawa wewe mkubwa unataka nikupe shikamoo? au tuzungumze hoja yetu hapa?
Unanishambulia kwa udogo wangu kutaka kunipoteza confidence, unaweka kuwa nimeandika mahaba kitu ambacho sijaandika hivyo pia unataka kuniaminisha nilichokiandika sicho wakati nimeandika mwenyewe. Huwezi kuzungumzia uwezo wa akili yangu ikiwa tu husomi na you put words on my mouth. Hahaha mie sijasema wala usije sema nime edit post yoyote bado husomi unajibu na unaona kitu amabcho akili yako inataka kuona. .
Sijasema mheshimia Tundu Lisu kakumbatia mashoga, nimeona anahojiwa kwenye taarifa ya habari BBC anakubali kwa kusupport ushoga kwa kauli yake mwenyewe Tundu Lisu kwa hilo sijaona mimi tu wengi wameona ila wewe hujaona. .
Ila siwezi kuendeleza mjadala na wewe hauko kunifundisha kwa madai ya ukubwa wako na unayoyazungumza ni yale yale, unajikita kwenye maneno ya fedheha na matusi kitu ambacho si siasa kwangu. Nina haki ya kusema sitaki upinzani huu, wewe una chama mimi sina chama ni haki yangu, sijakutukana au kukuponda kwa kufata siasa za upinzani ni haki yako. Unaniletea Uditekta kwenye huu uzi, alafu unadai Magufuli ni ditekta wakati wewe mwenyewe ni ditekta. Kwa kuwa una umri basi sisi wadogo hatuwezi kuwa na mawazo chanya tusihi unavyotaka wewe. .
Tatizo mtu yeyote anayeandika kuhusu raisi Magufuli basi anamnyenyekea kitu ambacho si kweli. Magufuli sio Mungu siwezi mnyenyekea, na yeye kama binadamu wote ana mapungufu mengi hata kwenye uongozi wake hajakamilika sio malaika yeye kwa hiyo sishangai akikosea. Ila mie nimeandika mtazamo wangu tu kama wewe umeona kunishambulia kuwa ni mtazamo mbovu sawa, siwezi kushambulia wa kwako na siwezi kukubaliana nao pia ni mawazo yako, sitokuvunjia heshima just because you lose mine which matters nothing for me, nikikujibu vibaya I will lose mine on respect which is worth everything to me. .
TUTAAMINIJE HICHO UNACHOKISEMA? MWAMBIE AHAMIE TUONE KAMA ATASHANGILIWA. USICHUKULIE YA LOWASA NA WENZAKE UKAFIKIRI KILA SIKU NI JUMATATU. WATU HUJIFUNZA ILA MBWEHA HAWAJIFUNZI.UKAWA ni Nzi wa kijani iliyozubaa ukitaka kujua hilo leo hii Jiwe akisema anahamia upinzani watamshangilia na kumpa kila Aina ya sifa unafiki wa Watanganyika hauna kifani dunia hii.
UNAFIKIRI NI KWANINI?Watu wanachuki bnafsi na Magufuli na wanashawishi wengne nao wamchkie bila sababu, Yaani twitter na Jf ukimtukana Magufuli unakua maaarufu ghafla....Mungu atusaidie asee
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa maelezo mazuri. Naamini atarudi vizuri.Kila mtu ana uhuru wa kuwa na mtazamo na labda kwako umeona nimekuwa upande wa raisi Magufuli, ila ukisoma kichwa cha habari ni utaelewa ni juu ya mtazamo wangu binafsi juu ya siasa ya Tanzania na raisi Magufuli na nimeandika kama kichwa kilivyojieleza. .
Ila umehisi nimeandika kumponda Mheshimiwa Tundu Lisu, na hicho ndio ulichokiona ila la msingi wewe huyaoini, je ni kitu gani ambacho nimezungumza juu ya mheshimiwa Tundu Lisu?? Ila hujajibu hata hoja yangu moja ila kwa kuipinga kwa Hoja au kubisha tu. Kwa mtazamo wangu tu umeandika hoja nyingine ambayo pengine ungeweza kuwa uzi mwingine unaohusu safari ya Tanzania kwenye mikono ya raisi Magufuli na pengine ningekujibu ila unanitoa ndani ya mada husika. .
Samahani ila nachokiona ni public sympathy, kama kupigwa risasi kwa mheshimiwa Tundu Lisu kinakunyima chuki yake binafsi dhidi ya raisi Magufuli inajikita mpaka kwenye kutaka kuboamoa Tanzania. Leo hii mheshimiwa Tundu Lisu anaomba publicly Tanzania inyimwe misaada, Je hiyo misaada anakula raisi Magufuli na familia yake? Hiyo misaada ni kwa ajili ya kila mTanzania ikiwemo mimi na wewe. Leo naona mheshimiwa Tundi Lisu anakubali kushikana kabisa mikono na mabeberu ili kusupport ushoga, kitu amabcho ni kinyume na maadili yetu, ambapo unampelekea chuki raisi Magufuli, wakati hoja ni kuwa chuki yake haileti maendeleo kwa Tanzania. .
Sipingi kama wana chuki ziwepo ila zisiwe kuiathiri Tanzania na waTanzania. Ila kipindi kile nilikuwa napata majibu mengi sana wakati Lowasa kasimama kugombea uraisi "kwani ikulu kuna kazi ya kubeba mawe". Ila nadaharia yako uliojiwekea ni kuwa nchi hii inaendeshwa na mtu mmoja tu anayeitwa 'Magufuli'. Ila nchi hii inaongozwa na viongozi wengi kuanzia ngazi ya kijiji mpaka ngazi ya nchi ambao sio CCM wala si kwa mawazo ya Magufuli. .
Raisi Magufuli kwenye uongozi wake kuna madhaifu mengi nimeandika moja ni kuharibu taaluma, sijaundika kumfagilia raisi Magufuli ila kwa kuwa nimeandika neno Tundu Lisu, basi nachoandika hata kama cha maana unakiona si kitu. Nachotaka tujibiane hoja kwa hoja na si kufanya siasa, na kama nimeandika umeona mtazamo finyu nielimishe nini kifanyike. Nadhani hujasoma vizuri hakuna sehemu nimeandika kiongoze chama kimoja unaweka maneno kinywani mwangu, nimesema natamani sana upinzani utawale siku moja ina maana hukuona???. .
Waliotoka utumwani ni wana wa Israel na sio Tanzania. Usitufananishe sisi na wana wa Israel wala utumwa wa Misri, sawa sawa na kuchanganya maziwa na tui la nazi. Tuache ya kwenye Biblia yabaki kwenye Biblia naomba unijibu au upinge hoja zangu kwa mifano au hoja. .
Kwako kuinusuru Tanzania ni kuwaweka madarakani kundi la wanasiasa wenye agenda binafsi, kwa singizio za madai ya demokrasia kupitia Tume "Huru" ya Uchaguzi ili wawe na Haki bila kuwajibika na Uhuru usio na mipaka!! Du, itageuka kuwa nchi ya kusadikikaKundi langu ni 'Tanzania' pekee. Sina bei ya ziada ya hapo.
Kwa hali inavyokwenda sasa nipo radhi hata kukipa 'kivuli' kura yangu kama itasaidia kuinusuru Tanzania.
Mkuu tindo, hapa nilipo hakika natamani kuwepo hiyo Tume "Huru" ili mbichi na mbivu za nani mshindi halali zionekane wazi.Kwani huduma bora kwa hao watu wa vijijini zinaletwa na ccm au ni kutokana na kodi za wananchi? Siasa za majukwaani hazijawahi kupitwa na wakati maana ndio siasa zenyewe. Labda kama hujui siasa ni nini. Siasa za kwenye vyombo vya habari na mitandaoni ni kutokana na nyakati, hizi ni nyakati digital, taarifa nyingi hupatikana mitandaoni.
Acha upotoshaji, wapinzani hawataki tume huru ya uchaguzi ili kuwapeleka ikulu, wapinzani wanahitaji tume huru ya uchaguzi ili mshindi apatikane kwa uhalali. Huenda unabishana kuhusu uwepo wa tume huru bila kujua hata wanaoidai wanamaanisha nini. Tatizo lililopo sio kuwa hamshindi baadhi ya sehemu kihalali, bali huwa sehemu kubwa ya ushindi wenu ni kupitia udhaifu wa tume mnayolazimisha iendelee kuwepo.
Je lowassa alivyokuwa mgombea wa urais kupitia Chadema alivyobeba hoja ya babu Seya amkuwa mnajua ni walawiti au unajifanya umesahau kama kawaida yenu?Gily,
..hukumuona Jpm na Babu Seya na Papii wakiwa Ikulu?
..Je, Babu Seya na Papii siyo mashoga na walawiti watoto?
Mkuu tindo, hapa nilipo hakika natamani kuwepo hiyo Tume "Huru" ili mbichi na mbivu za nani mshindi halali zionekane wazi.
Hapa inabidi wamulize Lowasa awajibu wenyewe.Je lowassa alivyokuwa mgombea wa urais kupitia Chadema alivyobeba hoja ya babu Seya amkuwa mnajua ni walawiti au unajifanya umesahau kama kawaida yenu?
Wacha visingizio, thread yako imejaa mapengo kibao, hilo la Tundu Lissu lilikuwa mfano mmoja tu wa mapengo yaliyomo.Angechagua ya Tundu Lisu basi maana hilo ndio walilolishikilia uzi mzima
Kabisa mkuu 🤣Angechagua ya Tundu Lisu basi maana hilo ndio walilolishikilia uzi mzima
Why not!Kwako kuinusuru Tanzania ni kuwaweka madarakani kundi la wanasiasa wenye agenda binafsi, kwa singizio za madai ya demokrasia kupitia Tume "Huru" ya Uchaguzi ili wawe na Haki bila kuwajibika na Uhuru usio na mipaka!! Du, itageuka kuwa nchi ya kusadikika
Ujinga mtupuMimi binafsi sina chama, si kwa sababu nataka iwe ivyo, ni kwa sababu sijaona chama Tanzania chenye misimamo nayotaka mimi.
Rais Magufuli na Bunge:
Kwa mtazamo wangu nadhani si kwamba raisi Magufuli anapinga mhimili wa bunge, hili limedhihirishwa na mkataba alioingia Muheshimiwa Kangi Lugola. Kwa kauli yake kupinga mkataba ule Kwa kuwa haukushirikisha bunge wala serikali yake wala wizara nyingine husika Kama Wizara Ya Fedha. Nafikiri tu kwa raisi magufuli kukubali kupeleka mambo mengi ambayo anafanya sasa bungeni basi hayo mambo yangebaki kwenye ubishani yasingefanyika.
Kupeleka majadiliano bungeni inakuwa Kama mbwa ukimshika mkia hata afanye vipi atafanya unavyotaka wewe. Serikali yetu ingekuwa imeshikiliwa mkia ingebweka tu ila bunge lingekuwa linapoteza mda mwingi kwenye mabishano ya kisiasa yasiyo zaa matunda na mambo mengi yangesimama kama tulivyoona serikali zilizopita. Hapa tuna kubwa la kujifunza, kutokuwa Na uwiano mzuri kati ya serikali Na bunge.
Raisi Magufuli na Misimamo Yake Kisiasa:
Nakumbuka raisi Magufuli alivyoingia madarakani katika mambo aliyoyafanya mwanzo Ni kupinga siasa zisifanyike wakati uchaguzi umepita. Kwa wapinzani waliona Kama wananyimwa kuwa huru kisiasa kiasi cha kumwita Magufuli Ni ditekta. Upande wa pili kwa raisi Magufuli alipinga hili ili kupisha maendeleo yafanywe na wale viongozi waliochaguliwa, akisisitizia, siasa za majukwaa zimepita sasa waliochaguliwa wafanye siasa za ktekeleza yale waliyoyaimba kwenye majukwaa. Lakini kitu ambacho nakiwaza tu Ni kuwa raisi Magufuli aliruhusu waliochaguliwa wawe wapinzani au awe CCM anaruhusiwa kufanya siasa kwenye jimbo lake hususani madiwani Na wabunge.
Mimi binafsi niko wilaya ya Ubungo Na nimepita sana Pwani huko na hata mkoani Kilimanjaro ambapo ni nyumbani, lakini sijaona madiwani au wabunge walioita mikutano kujadili lipi lifanyike kuleta maendeleo (nimeuliza maeneo mengi ila hiki ndicho kinachoendelea). Nani kaenda kufanya mikutano ya hadhara kakataliwa kwenye jimbo lake?
Magufuli na Tundu Lisu:
Kwanza kabisa nasikitika Sana kwa mheshimiwa Tundu Lisu kupigwa risasi mchana kweupe na jambo hili kupelekwa kisiasa. Ila nimeona jambo ndani ya Mheshimiwa Tundu Lisu na chuki yake dhidi ya raisi Magufuli. Binafsi wanasiasa wanachukiana ila chuki zao ni za kisiasa wakiwa kwenye mziki wanacheza pamoja, binafsi sijui chuki hizi zililetwa na nini ila wao binafsi wanaelewa kindaki ndaki sio tunashabikia tu. Ila nasikitika sana kitendo cha mheshimiwa Tundu Lisu kwenda kuichafua Tanzania ili tusipewe misaada kwa chuki yake binafsi dhidi ya raisi, bila kujali anachikiomba anawaathiri vipi wa Tanzania.
Mheshimiwa Tundu Lissu anazunguka sehemu nyingi duniani kutaka wajitenge Na Tanzania wakati familia yake, ndugu zake Na ukoo wake wapo Tanzania. Amezunguka akiomba mabeberu watunyime misaada kitu ambacho hajui kingemuathiri kila mTanzania. Amediriki kukubaliana Na mabeberu tena nimesikitika Sana kusikia mheshimiwa Tundu Lisu akisapoti ushoga kabisa kwa mdomo wake mwenyewe na kuikandia serikali ya Tanzania ka kukataa ushiga ilihali anajua tamaduni hizi kwetu hazipo. Mbali na kuichafua Tanzania hao mabeberu bado wamekuwa mstari wa mbele kuleta misaada na kuikopesha Tanzania.
Mheshimiwa Tundu Lisu amekosa uzalendo kuhusu Tanzania juu ya chuki yake dhidi ya Magufuli. Kama alikuwa na mashtaka binafsi juu ya Magufuli sikatai ila hana ulazima wa kuichafua Tanzania na kuchinganisha na nchi rafiki, hata Magufuli akitoka madarakani uhusiano uliopo kati ya Tanzania na nchi nyingine utabaki, anapotaka kuuvuruga hata aje raisi mwingine lile doa litakuwepo tu ..
Raisi Magufuli hata Kama anayoyafanya analazimisha Kwa wananchi wa Tanzania na yatabaki kwa wananchi wa Tanzania. Hizo ndege si zake Ni za waTanzania, Na juhudi hizi zinaonekana ni za kujenga Tanzanua; huku Tundu Lisu anabomoa kile kinachojengwa kwa wa Tanzania. Tanzania inasonga mbele Kwa shida kwa raha ila inasonga mbele.
Siasa na Taaluma:
Kwa mtazamo wangu tu nchi yetu imeshindwa kutofautisha siasa na taaluma, hapo mwanzo tulikuwa tuko kwenye shimo dogo tu ila kwa sasa tuko kwenye shimo kubwa sana. Raisi Magufuli kwa kuchagua viongozi wenye taaluma zao kwa asilimia kubwa ameua nguvu nzito kwenye taaluma yetu. Kila m Tanzania sasa amekuwa mwanasiasa kitu ambacho kimekuwa sana katika utawala huu wa awamu ya tano. Ukienda chuoni, mashuleni, jeshini na maofisini watu wengi wamekuwa wanaacha taaluma zao na kuingia kwenye siasa. Baadhi ya viongozi au taaluma (mfano maprofesa, madokta, wanajeshi) ambao wamechaguliwa na raisi wetu wangeweza kuwa walimu wazuri wazalishe wanasiasa wazuri ila wameacha kuzalisha wanasiasa na wamekuwa ndio wanasiasa wakubwa. Sasa kumekuwa na taaluma mbovu kwa sababu ya siasa za kupita, ila manufaa ya taaluma si ya kupita.
Magufuli na Wananchi Wake:
Kwa mtazamo wangu kuna wananchi wanakubali Sana kazi na mwenendo wa serikali ya raisi Magufuli. Ila pia kuna wananchi wanachukia sana mwenendo wa serikali hii ya awamu ya tano kwa mitazamo yao mingi tu. La kusikitisha kipindi hiki cha miaka mitano wananchi wamepandikizwa chuki mbaya ambazo Ni kinyume Na utamaduni wetu Kama waTanzania. Chuki hizi zinaonekana mpaka baina ya ndugu Na ndugu huku watu wakiwa wamesahau siasa si chuki. Mfano tu humu ndani ya JF nimesoma nyuzi nyingi humu ndani watu wameshindwa kabisa kubishana kwa hoja majibu yao yanakuwa mfano “nenda kachukue buku saba lumbumba”, huku jukwaa hili la siasa likikosa sifa kabisa kwa kuwa na matusi mengi ambayo nashindwa kuyaandika hapa kwa maadili yangu yalivyo. Nahimiza tu watu wawe CCM, CHADEMA, au chama chochote kile siasa sio ‘Matusi’ “Hoja Hupingwa Kwa Hoja”
Siasa za Upinzani:
Kwa mtazamo wangu tu siasa zimebadilika Sana Kwa wapinzania Kwa sasa zile siasa za kusema tutajenga mashule, hospitali, barabara, tutaleta maji nk Kwa sasa hazisikiki. Nimekuwa najiuliza Sana Kwa nini hazisikiki? Nimegundua kuwa Kwa sasa vitu vingi vimejengwa au kuboreshwa Na serikali hii ya awamu ya Tano. Wapinzani wa raisi Magufuli kwa asilimia kubwa kazi zao zimekuwa ni kuponda tu huku huku hawawi mbele kusema kipi kifanyike. Kwa akili ya kawaida tu huwezi kuwa mmekaa kibarazani aje mwenye nyumba awaulize ‘mmekula nataka kuwaletea chakula’ alafu mmoja wenu ajibu “sie tumeshiba” huku mnakuta wengine wana njaa kali amewasemea bila kuwauliza kama wanahitaji kula. Kwa sasa siasa zimekita kwenye udikteta wa raisi Magufuli na kuponda yale anayofanya huku wakiwa hawasemi nini kifanyike tusonge mbele..
Kwa mtazamo wangu tu Wapinzani kuleta maendeleo si lazima wawe wamechaguliwa: Kwa jinsi nilivyoona wapinzani wakiwa msatri wa mbele kuomba michango ya kuwatoa wenzao gerezani au kuomba hela za hospitali za mheshimiwa Tundu Lisu basi wangeweza kutumia njia hizo hizo kukusanya michango kwa waTanzania ili kuleta maendeleo. Hata Kama hili lingepingwa wapinzani hawa wangeweza kuanzisha utaratibu Kwa viongozi waliowachaguliwa ndani ya upinzani kuleta maendeleo Kwa michango ya wananchi wenyewe ILA zingeonekana Ni juhudi zao ndio zimeleta maendeleo. Wapinzani wanaonekana kuwa wamesahau kabisa kuwa ‘Maendeleo Hayana Chama”
La mwisho ningependa sana kuona siku moja upinzani umeshika madaraka Tanzania ila si kwa upinzani huu naouona sasa. Na ningependa sana kuona CCM inavunjwa Na kuanzishwa chama kipya chenye wanasiasa mahiri wanaoweza kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania Kwa wananchi wake. Ningependelea sana kuona siasa zenye tija na maendeleo kwa waTanzania wote bila kujali wametokea vyama gani vya siasa. .